Tafuta

Askofu Luis Manuel Ali Herrera, ameteuliwa kuwa Katibu wa Tume ya Kipapa ya Ulinzi wa Watoto Askofu Luis Manuel Ali Herrera, ameteuliwa kuwa Katibu wa Tume ya Kipapa ya Ulinzi wa Watoto 

Papa ameteua Katibu na Katibu Mwambata wa Tume ya Kipapa kwa ajili ya Ulinzi wa Watoto

Baba Mtakatifu ameteuwa Katibu wa Tume ya Kipapa kwa ajili ya Ulinzi wa Watoto Askofu Msaidizi Luis Manuel Alí Herrera,wa Bogotá na wakati huo huo akamteua hata Katibu Mwambata Dk.Teresa Morris Kettelkamp,wote wawili hadi uteuzi huo walikuwa ni Wajumbe wa Tume hiyo hiyo.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Ijumaa tarehe 15 Machi 2024, Baba Mtakatifu amemteua Katibu wa Tume ya Kipapa kwa ajili ya Ulinzi wa Watoto  Askofu Msaidizi Luis Manuel Alí Herrera, wa  Bogotá Nchini Colombia  ambaye hadi uteuzi huo alikuwa ni mjimbe wa Tume hiyo. Vile vile  Baba Mtakatifu Francisko akamteua Katibu Mwambata wa Tume hiyo Dk. Teresa Morris Kettelkamp, ambaye hadi uteuzi huo alikuwa pia mjumbe wa  Tume hiyo.

Wasifu  

Askofu Luis Manuel Ali Herrera, alizaliwa huko Barranquilla, nchini Colombia, mnamo mwaka 1967, na alifundwa katika Seminari ya Conciliar ya Bogotá akapewa daraja la upadre mnamo mwaka  1992. Baada ya kuhitimu elimu ya Taalimungu katika Chuo cha Kipapa cha Javeriana,  Bogotá (2003), alipata shahada ya saikolojia kutoka Chuo Kikuu cha Kipapa cha Gregoriana Roma (2007). Askofu Herrera ni mshirika mkuu wa Chuo cha Colombia cha Kisaikolojia. Mnamo 2015, Papa Francisko alimteua kuwa Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Bogotá, na mako yake ya kiaskofu Giubalziana. Pia kunako mwaka 2015 aliteuliwa kuwa Tume ya Kipapa ya Ulinzi wa Watoto. Askofu Msaidizi na Mwanasaikolojia  ni Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki nchini Colombia. Aidha Askofu Alí Herrera aliwahi kuwa mkurugenzi wa Eneo la Mwelekeo wa Kisaikolojia katika Seminari ya Jimbo Kuu la Bogotá (2007 - 2015), ambapo pia alifundisha saikolojia ya maendeleo ya binadamu, saikolojia ya kijamii, na saikolojia ya kichungaji.

Wasifu wa Dk. Morris

Dk. Morris Kettelkamp alizaliwa tarehe 13 Februari 1952 huko Chicago, Marekani. Baada ya masomo na Shahda ya Sayansi za sera za Kisiasa  Chuo Kikuu Quincy  alijiuna na Kikosi cha Polizi katika Serikali ya Illinois, ambapo alistaafu na cheo cha Kanali.  Alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Sekretarieti ya Ulinzi wa Mtoto na Vijana wa Baraza la Maaskofu Katoliki nchini Marekani. Alifanya kazi ya kuandaa miongozo kwa ajili ya Ulinzi wa Watoto na Watu wazima walio katika mazingira magumo ya Tume ya Kipapa kwa ajili ya Ulinzi wa Watoto na mnamo 2018 aliteuliwa kuwa Mjumbe wa Tume hiyo hiyo.

Uteuzi huo mpya ulitangazwa Ijumaa na Ofisi ya Wanahabari ya Vatican

Baada ya taarifa hiyo, Kardinali Seán O’Malley, Rais wa Tume hiyo, albanisha kuwa “uteuzi huo unaashiria hatua muhimu muhimu katika kulifanya Kanisa letu kuwa mahali salama zaidi kwa watoto na watu walio hatarini. Wakati tunatoka katika malezi tofauti na kuwa na karama za kuwekwa katika ulinzi, Katibu mpya na Katibu Mwambata wanashiriki shauku ya pamoja kwa ajili ya ustawi wa watoto na watu walio katika mazingira magumu, kwa maisha ya huduma kwa Kanisa  katika uwanja huu.”

Rais wa PCPM pia alitoa shukrani zake kwa Katibu anayemaliza muda wake, Monsinyo Andrew Small, (OMI) kwamba: “Kwa maono na ushupavu, Padre  Small amesaidia mipango muhimu ambayo Tume imekumbatia.” Na kwa  Kardinali O’Malley alihitimisha taarifa yake kwa kuakisi uthibitisho wa Papa Francisko wa “jukumu lililopanuliwa” la Tume pamoja na mwelekeo wake kwamba: Kwa tangazo la leo la uteuzi mpya, Tume inaendelea katika njia hii ya kufanya ulinzi kuwa sehemu thabiti ya kila kipengele cha maisha na huduma ya Kanisa.”

Uteuzi makatibu wawili wa Tume ya Kipapa ya Ulinzi wa Watoto
15 March 2024, 15:48