Baba Mtakatifu Francisko tarehe 21 Machi 2024 alikutana na kuzungumza na Rais George Vella wa Malta. Baba Mtakatifu Francisko tarehe 21 Machi 2024 alikutana na kuzungumza na Rais George Vella wa Malta.  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Rais wa Malta George Vella Akutana na Papa Francisko Mjini Vatican

Katika mazungumzo yao, Baba Mtakatifu Francisko pamoja na mgeni wake, wameridhishwa na uhusiano wa kidiplomasia uliopo kati ya Vatican na Malta. Baadaye, wakajielekeza zaidi katika masuala ya Kimataifa, huku wakijikita zaidi katika mazingira ya Bahari ya Mediterrania, changamoto kubwa ya wakimbizi na wahamiaji; Vita kati ya Israeli na Palestina pamoja na vita kati ya Ukraine na Urusi.. Changamoto ya wimbi kubwa la wakimbizi na wahamiaji inahitaji mpango mkakati

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S., Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko tarehe 21 Machi 2024 alikutana na kuzungumza na Rais George Vella wa Malta, ambaye baadaye alibahatika kukutana na kuzungumza na Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican aliyekuwa ameambatana na Monsinyo Mirosław Stanisław Wachowski Katibu mkuu Msaidizi wa Mambo ya Nchi za Nje, Ushirikiano na Mashirika ya Kimataifa.

Uhusiano wa kidiplomasia kati ya Vatican na Malta unaridhisha
Uhusiano wa kidiplomasia kati ya Vatican na Malta unaridhisha

Katika mazungumzo yao, Baba Mtakatifu Francisko pamoja na mgeni wake, wameridhishwa na uhusiano wa kidiplomasia uliopo kati ya Vatican na Malta. Baadaye, wakajielekeza zaidi katika masuala ya Kimataifa, huku wakijikita zaidi katika mazingira ya Bahari ya Mediterrania, changamoto kubwa ya wakimbizi na wahamiaji; Vita kati ya Israeli na Palestina pamoja na vita kati ya Ukraine na Urusi. Wimbi kubwa la wakimbizi na wahamiaji sehemu mbalimbali za dunia, ni kati ya mada zilizovuta hisia za viongozi hawa wawili.

Malta
26 March 2024, 13:34