Shirika la Kipapa la Utoto Mtakatifu:kuwa tayari kutoa ushuhuda wa imani yetu!

Tunachapisha maandishi na video ya Sista Roberta Tremarelli,katibu mkuu wa Shirika la Kipapa la Utoto Mtakatifu,aliyowaandikia watoto na vijana wamisionari katika Maadhimisho ya Juma Takatifu na Pasaka!Mkuu huyo anabainisha kuwa:"Tuna hakika:tunataka kuwa marafiki wa Yesu!Kwa sababu hiyo wakati wa Juma Takatifu tujishughulishe kukaa pamoja Naye,kushikamana Naye.Kama wamisionari tujitolee kujibu wito,urafiki na uaminifu wetu kwa Mungu.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Katika fursa ya Maadhimisho ya Juma Takatifu ambalo tunakumbuka mateso, kifo na baadaye ufufuko wa Bwana wetu Yesu Kristo, Sista Roberta Tremarelli, Katibu mkuu wa Shirika la Kipapa la Utoto Mtakatifuamewandikia watoto na vijana wamisionari katika Maadhimisho haya. Kwa njia hiyo tunachapisha maandishi na video yake. Wapendwa watoto wa kimisionari, salamu njema kutoka La Verna, mahali ambapo Mtakatifu Francis wa Assisi alipokea ishara za upendo wa Yesu Msulubiwa(madonda). Kwaresima inakaribia mwisho na Dominika ya Matawi itaanza; ni Juma muhimu zaidi la mwa wa Kanisa Katoliki. Mungu ni rafiki mwaminifu aliyefanya agano nasi na hatatusaliti. Yesu, mwana wa Mungu, ni rafiki mwaminifu, rafiki bora zaidi katika maisha yetu na ni lazima kushika nafasi ya kwanza katika mioyo yetu, kwa sababu sisi ni katika moyo wa Mungu na tuna nafasi ya upendeleo ndani yake, kama kila mmoja wetu  alivyo mmoja na wa kipekee.

Kwa hivyo tukianza na upendo huu mkubwa na kutoka kwa urafiki huu mwaminifu, maombi yetu yanazaliwa. Maombi yetu ni sifa na shukrani kwa Bwana, kwa Yesu kwa uaminifu wake kwetu. Mungu, Yesu hatutupi kamwe; Hatuachi peke yetu na kupitia maombi yetu tunamshukuru na kumsifu Bwana kwa uwepo wake wa kudumu maishani mwetu. Na katika mkutano wenu na kujitolea kwenu kila siku kama washiriki wa Utoto wa Kimisionari, kila siku mnatafuta kuimarisha urafiki wenu na Yesu na kuleta upendo wake kwa wote. Tuna hakika:tunataka kuwa marafiki wa Yesu! Kwa sababu ya hili, wakati wa Juma Takatifu tujishughulishe kukaa pamoja Naye, kushikamana Naye.

Yesu alipoingia Yerusalemu “Watu wengi wakatandaza nguo zao njiani, na wengine wakatandaza matawi ya majani waliyoyakata mashambani, wakipiga kelele, “Hosana! Mbarikiwa yeye ajaye kwa jina la Bwana! -10). Siku chache baadaye Yesu alishiriki karamu ya mwisho pamoja na mitume wake. Kisha Yesu aliishi na kujionea peke yake huzuni ya Mateso. Lakini leo sisi, kama wanafunzi wake, kama wanafunzi wake wamisionari, tunajitolea kukaa pamoja Naye, katika umoja na Mungu na pamoja na Maria. Katika juma hili Takatifu maombi yetu, maombi yetu rahisi ya kila siku yatakuwa katika moyo wa Yesu.

Watoto wapendwa wamisionari, tunajitolee kujibu wito wetu, kujibu urafiki na uaminifu wa Mungu kwa maombi yetu, kuwa na Yesu. Kusikiliza na kusoma Neno la Mungu, Injili, tunaweza kuona upendo wa ajabu ambao Mungu anao kwetu; tunaweza kuona jinsi anavyotutunza. Kwa hiyo, tunajibu kupitia maombi yetu kwa moyo wa Yesu, tukiandamana Naye kupitia mateso na hivyo kufikia pamoja Naye furaha ya ufufuko, kushiriki na kila mtu kwamba Yeye ameshinda kifo. Ninawaalika mkae macho na ujasiri pamoja na Yesu, macho na moyo wazi kwa matukio ya Mateso, kwa maneno yake, kwa matendo yake na kwa ukimya wake. Daima kuwa tayari kutoa ushuhuda wa imani yetu Kwake.

Bila hofu ya kutofanikiwa, anatupenda hata kama tunaogopa, hata kama hatuwezi kufanya tunachotaka. Hebu tukae pamoja na Yesu, bila kukata tamaa kwa kile kinachotokea, lakini daima tukiwa na uhakika katika ahadi yake. Tuwe pamoja na Yesu anayeteseka hadi mwisho. Tukumbuke kwamba wakati wa utume wake, Yesu daima alikaribisha watoto na sasa ni zamu yetu ya kumkaribisha. Tuombe pamoja na Yesu ili tuwe hodari dhidi ya uovu. Hebu tumtazame Yesu Aliyesulubiwa na Kufufuka ili tumjue na kuwa shahidi wake. Watoto wapendwa wamishonari, ninawatakia ninyi nyote, wazazi na wahuishaji wenu, kwa mapadre na watawa ninawatakia JumaTakatifu yenye matunda na Pasaka yenye furaha!

Ujumbe kwa watoto wa kimisionari katika fursa ya Juma Takatifu
26 March 2024, 10:03