Mapambo ya Maua katika Juma Takatifu katika Uwanja wa Mtakatifu Petro 2023. Mapambo ya Maua katika Juma Takatifu katika Uwanja wa Mtakatifu Petro 2023. 

Uwanja wa Mtakatifu Petro na Basilika:bustani yenye rangi nyingi kwa ajili ya Pasaka!

Kurugenzi ya Mji wa Vatican imetoa maelezo juu ya mipango ya maua kwa ajili ya Dominika ya Matawi hadi Ufufuko wa Bwana.Mapambo ya maua kutoka mji wa Sanremo na Uholanzi yanapamba katika Uwanja wa Kanisa Kuu na ndani ya Kanisa.Wafanyakazi wa Vatican wanashirikiana na wataalamu kutoka nchini Slovenia katika maandalizi ya upambaji.

Vatican News

Onesho la maua mazuri na mimea ya kupendeza kutoka Italia na Uholanzi yanapamba Uwanja wa Mtakatifu Petro na ndani ya Basilika ya Mtakatifuy Petro mwaka huu katika hafla ya Juma Kuu Takatifu 2024. Gavana wa Mji wa Vatican ametoa maelezo  kuhusu mipango hiyo  ya Siku  kuu na katika taarifa kwa vyombo vya habari, alisisitiza kwamba “wakati wa mkesha wa Pasaka, mapambo ya maua yataundwa kutokana na mchango wa maprofesa wa maua wa Kituo cha Naklo Biotechnology nchini Slovenia,” na kwamba, “katika nuru na furaha ya Kristo Mfufuka, katika maadhimisho ya Pasaka, Dominika  tarehe 31 Machi, Uwanja wa Mtakatifu Petro utakuwa ni bustani kubwa ya rangi nyingi, yenye maelfu ya maua na mimea inayowasili kutoka nchini Uholanzi. Mapambo hayo yataundwa kutokana na mchango wa ukarimu wa watengenezaji maua wa Uholanzi kwa ushirikiano wa wafanyakazi wa Huduma ya Bustani na Mazingira ya Kurugenzi ya Miundombinu na Huduma ya Gavana wa Mji wa Vatican.

Mapambo ya Pasaka mnamo 2023
Mapambo ya Pasaka mnamo 2023

Mapambo ya Mitende na Juma  Takatifu

Taarifa kwa vyombo vya habari aidha ilibainisha kuwa, katika hafla ya Diminika ya Matawi tarehe 24 Machi 2024, “Matawi ya mizeituni yatasambazwa na Jumuiya ya Kitaifa ya Miji ya Mafuta ya Mkoa wa Sardegna, iliyoratibiwa na Antonio Balenzano, mkurugenzi wa kitaifa wa Chama  hicho, wakati “mitende iliyotengenezwa itatolewa kwa njia ya Harakati ya Waneokatekumenali na kusambazwa na Ofisi ya Maadhimisho ya Liturujia za Kipapa.” Mitende maarufu iliyosukwa pia itakuwepo, iliyotolewa na kampuni binafsi Errico Grazia ya Sanremo. Kampuni ya jumla ya kilimo cha maua (Flora NL) ya Roma itaazimisha miti mikubwa ya mizeituni ambayo itawekwa karibu na sanamu za Watakatifu Petro na Paulo chini ya Uwanja wa Kanisa Kuu na obelisk. Mapambo ya maua katika Uwanja wa Mtakatifu Petro yanaandaliwa kabisa na wafanyakazi wa Huduma ya Bustani na Mazingira.

Mapambo ya Pasaka katika Uwanja wa Mtakatiu Petro na Kanisani
23 March 2024, 12:21