Tafuta

2024.03.06 Makata ya Kitume Vatican:Hwa ni wanawake wa kwanza waliopata shahada mjini Vatican kuanzia  1929 ina baadaye.Picha ni ya mwaka 1936. 2024.03.06 Makata ya Kitume Vatican:Hwa ni wanawake wa kwanza waliopata shahada mjini Vatican kuanzia 1929 ina baadaye.Picha ni ya mwaka 1936. 

Vatican:Maadhimisho ya miaka 95 ya wafanyakazi wa kwanza wasomi wa kike

Mnamo 1929 Maktaba ya Kitume ya Vatican iliajiri kikundi cha wanawake vijana wenye digrii za udaktari kwa kuashiria mwanzo wa sura za kike mjini Vatican.Uzoefu wao ulikuwa mzuri,lakini mpango huo ulimalizika miaka 12 tu kutokana na Vita vya Kidunia vya pili.Leo hii zaidi ya asilimia 50 ya wafanyakazi katika Maktaba ya Vatican ni wanawake na wengi wao wana vyeo vya uongozi.

Na  Gudrun Sailer na Angella Rwezaula - Vatican

Yote haya na safari ya kwenda Marekani mnamo mwaka wa 1927. Kwa karibu miezi mitatu, Eugène Tisserant alisafiri ili kupitia maktaba muhimu zaidi nchini Marekani ambapo ilikuwa sio kwa ajili ya kusoma, ingawa ilimjaribu sana. Padre Mfaransa na mtaalamu wa mambo ya mashariki, mwanachuoni (“Mwandishi”) katika Maktaba ya Kitume ya Vatican, aliyebarikiwa kwa shauku kubwa katika uvumbuzi, alijaribu kuhakiki mabadiliko makubwa katika mazoea ya maktaba ambayo yalikuwa yamefanyika Amerika Kaskazini. Tisserant alirudi na mpango wa kuoanisha Maktaba ya Kitume ya Vatican inayoheshimika na kanuni zinazomlenga mtumiaji: upangaji, huduma ya marejeo, utaratibu uliorahisishwa wa kuagiza, hifadhi iliyopangwa vizuri na chumba kikubwa cha kusomea. Hii ilijumuisha hazina salama ya vitabu adimu na miswada na ufikiaji wa wasomi kama hapo awali  na zaidi ya hapo. Tisserant alilenga kuleta matumizi kwa Vatican na kuiingiza katika enzi ya kisasa ya maktaba.

Wanawake kama wasimamizi wa maktaba: Avant-garde nchini Marekani

Angalizo lingine lililotolewa na Padre mwenye elimu ya juu katika maktaba za Amerika lilikuwa ni kuwepo kwa wanawake. Wanawake wenye elimu wanaofanya kazi katika maktaba. Hili lilikuwa halijasikika jijini Vatican. Hata hivyo, 1929 ulikuwa mwaka wa uvumbuzi katika mji wa Vatican. Mikataba ya Lateran ilimhakikishia Papa uhuru wa eneo la Italia na hivyo kuibua ukuaji wa ujenzi na utitirishaji  wa uvumbuzi ambao haukuwa umeonekana jijini Vatican tangu kipindi kile cha cha kuzaliwa upya.

Ubunifu ambao uliendana sana na ladha ya msomi Papa Pio XI; kwa jina la Ratti mwenyewe ambaye alikuwa Mkuu wa Maktaba ya Vatican katika miaka yake ya ujana. Kwa hiyo alisema: “Sasa ndiyo kwa mabadiliko yote na ndiyo kwa msaini wa kwanza au wanawake vijana”  kama walivyoitwa - kwenye maktaba yake katika mchakato wa kisasa. Msomi wa kwanza wa kike kufika Vatican alikuwa mwanasiasa wa zama za kati wa Ufaransa Jeanne Odier mnamo Oktoba 1929. Raffaella Vincenti, Katibu wa kwanza mwanamke wa Maktaba ya Vatican, ambaye ameshika nafasi hiyo ofisini tangu 2012, ambaye alitoa muhtasari wa tukio hilo kwamba: “Kwa jumla, kulikuwa na wanawake 24. Waliajiriwa kwa miaka mingi na kufanyia kazi orodha ya maandishi. Tunajua kwamba wengi wao walipata digrii zao kutoka Chuo Kikuu cha La Sapienza, Roma na wengine pia kutoka Shule ya Vatican ya Sayansi ya Maktaba, ambayo Papa Pio XI aliifungua mnamo 1934, kwa bahati pia matokeo ya safari ya Eugène Tisserant kwenda  huko Marekani.”

Mfuko wa Msaada wa Taasisi ya Marekani

Mfadhili huyo pia alitoka Marekani, yule yule ambaye alikuwa amesaidia sana kufadhili safari ya Tisserant kwenda nje ya nchi. Mfuko wa kufikiria unaoendelea  bado Carnegie Endowment for International Peace, wa (Dhamira ya amani ya kimataifa, ulioanzishwa mnamo 1910 na mfanyabiashara wa chuma Andrew Carnegie, ulisaidia katika ujenzi wa Ulaya baada ya Vita vya Kwanza vya Kidunia. “Mfuko ulisaidia shughuli za kiutamaduni hasa, kwani ulizingatiwa kuwa muhimu kwa ajili ya  upya,” kwa mujibu wa maelezo ya  Raffaella Vincenti. Waamerika waliona uwezekano fulani katika kuifanya Vatican kuwa ya kisasa na ushawishi wake kwa ulimwengu wa wasomi wa Ulaya. Kutokana na ukweli kwamba wasimamizi wa maktaba wa kike hawakuwa tena nadra nchini Marekani, inaweza kuwa sababu mojawapo kwa nini fedha za taasisi ya Marekani sasa zilikuwa zikiwanufaisha wanawake waliohitimu katika maktaba ya Papa kwa mara ya kwanza.

Walikuwa na elimu, na walikuwa wakifanya kazi imara. “Walichaguliwa kwa sababu walikuwa wataalam katika uwanja wa maandishi na palaeography,” alisisitiza Raffaella Vincenti. “Kazi ya wanawake hawa ilikuwa kuelezea na kuorodhesha maandishi. Zaidi ya hayo, walitengeneza sheria kadhaa ili kuhakikisha uthabiti katika kurekodi.” Hili lilikuwa kazi ya maktaba yenye kudai sana. Baada ya yote, uchunguzi wa (bibliografia) wa mkusanyo mkubwa zaidi wa hati ulimwenguni ulikuwa mikononi mwa wanawake hao.

Wanawake waliofanya kazi Italia ya kifashisti

Katika nchi jirani ya Italia, wasomi wa kike walisitasita kuingia katika ulimwengu wa taaluma. Wanawake wengi wenye digrii za udaktari katika ubinadamu wakawa walimu;  laki si mara chache mwanamke katika miaka ya 1920 na 30 ya ufashisti alifikia kazi kama profesa wa chuo kikuu. Ingawa ufashisti ulikuza mtazamo wa kutowaamini wanawake - Mussolini alitaja umaarufu wa mwanamke anayefanya kazi na mashine kama vitisho viwili vikubwa kwa wanaume wa Italia katika kijitabu mashuhuri mnamo 1934 - wazo lilichukua polepole katika familia kwamba binti aliye na digrii ya chuo kikuu ambaye angekuwa bora apewe ikiwa angebaki bila kuolewa. Kwa hivyo, idadi ya wanafunzi wa kike katika vyuo vikuu wakati wa ufashisti iliongezeka kwa kasi, kwa maneno kamili na ya jamaa. Na hapa na pale, mwanamke aliye na shahada ya udaktari angeweza kupata nafasi katika mamlaka ya mambo ya kale, hifadhi ya kumbukumbu, au maktaba. Kwa hivyo, wasomi wa kike katika nchi jira ya Vaticam walikuwa wavumbuzi japokuwa  sio mapinduzi  kwa njia iliyoanzishwa ya kikanisa.

kizazi kipya cha wanawake katika huduma ya Kanisa

“Watia saini kadhaa katika Maktaba ya Vatican hawakupokea nyadhifa za kudumu; walifanya kazi kwa saa moja. Hawakuwa pia wanawake wa kwanza katika Vatican,” kulingana na kila kitu ambacho kimerekodi Vatican, ukuu huu ni wa mshonaji Anna Pezzoli mnamo 1915, na inajulikana pia kuwa watawa jijini  Vatican waliendesha semina ya urekebishaji wa mazulia ya makumbusho,  tangu miaka ya 1920. Hata hivyo, Jeanne Odier na wenzake walikuwa wasomi wa kwanza wa kike katika Mji wa Papa. Waliwakilisha kizazi kipya cha wanawake katika huduma ya Kanisa, na mfano wao ukashika kasi. Miaka mitano baadaye, mwanaakiolojia Mjerumani-Myahudi Hermine Speier alianza huduma yake kama mtunza maktaba ya picha katika Makumbusho ya Vatican, pia mwanzoni tu kama “mfanyakazi huru wa kudumu” licha ya kuwa na sifa zote. Tofauti na wenzake katika maktaba, Hermine Speier alibakia kwa muda wa kutosha kufikia cheo cha kudumu na haki ya pensheni katika mji wa Vatican, ikiwezekana akawa mwanamke wa kwanza kufanya hivyo mnamo mwaka wa 1964.

Enzi ya wasomi wa kwanza wa kike jijini Vatican ilifikia mwisho mnamo 1941. Tayari mnamo 1939, na mabadiliko kutoka kwa Pio XI hadi PioXII, mabadiliko yalikuwa dhahiri. Kwa vyovyote vile, tangazo la vita la Italia na Ujerumani dhidi ya Marekani mnamo 1941 lilikuwa na jukumu, kulingana na Raffaella Vincenti. Mawasiliano yalivunjika, na vipaumbele katika mji wa Vatican na vilevile katika Mfuko wa Marekani vilibadilika. Leo hii Maktaba ya Vatican ina karibu wafanyakazi 100, “na zaidi ya nusu yao wakiwa wanawake, na idara zetu nyingi zinaongozwa na wanawake,” alisema Bi Vincenti. Mtunzi wa kumbukumbu na mtunza maktaba wa Kanisa Takatifu la Roma, Mwenyekiti wa Maktaba ya Kitume Vatican na Makamu ni wanaume, lakini idara za hati, kazi zilizochapishwa, urejeshaji, nakala, IT, na pia sekretarieti, ambapo viunga vyote hukutana, viko mikononi mwa wanawake. “Hakika hii inatokana na ukweli kwamba wanawake wanawakilishwa zaidi katika ubinadamu, kuakisi hali ya malengo,” alisema Bi Vincenti. Uteuzi wa wasomi wa kwanza wa kike jijini Vatican katika kasi ya uboreshaji wa maktaba miaka 95 iliyopita ilikuwa tu mwanzo wa haya yote.”

Miaka 95 ya maktaba Vatican na wanawake wa kwanza kufanya kazi humo
08 March 2024, 16:36