2024.03.28 Kuanzia kilio cha uchungu cha mtume Petro ambaye baada ya kumkana Bwana mara tatu alijitambua makosa ndivyo mapadre wanaombwa kufanya hivyo. 2024.03.28 Kuanzia kilio cha uchungu cha mtume Petro ambaye baada ya kumkana Bwana mara tatu alijitambua makosa ndivyo mapadre wanaombwa kufanya hivyo.  (Vatican Media) Tahariri

Zawadi ya machozi kwa wale walio mbali

Tunachapisha tahariri ya Mwariri wetu Mkuu Tahariri wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano Dk.Andrea Tornielli kuhusiana na mahubiri ya Baba Mtakatifu siku ya Alhamisi kuu 28 Machi 2024 katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican:”Maneno ya Papa katika Misa ya Krisma na ushuhuda wa Wakristo."

Na Andrea Tornielli

“Bwana haombi hukumu za dharau kwa wale wasioamini, lakini upendo na machozi kwa wale walio mbali.” Baba Mtakatifu Francisko ameanza Ibada ya Juma Takatifu kwa kuongoza Ibada za Juma Takatifu katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro na kutoa mahubiri ya machozi. Kuanzia kwenye kile “kilio cha uchungu” cha mtume Petro, ambaye baada ya kumkana Bwana mara tatu katika ua la nyumba ya makuhani wakuu, alikutanisha kwa dakika chache na macho ya huruma ya Yesu akiwa katika minyororo na akakabili kukumbatiwa na Yesu kwa msamaha na akatambua dhambi yake.

Papa Francisko alizungumza na ndugu zake mapadre, katika adhimisho lililowekwa wakfu kwa namna ya pekee kwa ajili yao. Lakini maneno yake yanaweza kupanuka na kutufunika sisi sote. Mbele ya kukabiliwa na hali za maisha na misimamo ya wale wasioamini, ya wale wanaobishana nasi, lakini pia hata mbele ya hisia tofauti za ndugu zetu katika imani, ni mara ngapi hukumu za dharau, za uhakika hutiririka kutoka mioyoni mwetu. Wakati mwingine hukumu za dhihaka, sio tofauti sana na zile zilizofanywa kuvuma chini ya msalaba. Inatosha kwanza kutazama “ndani ya nyumba” ili kutambua hatari hii. Inatosha kuutazama ulimwengu wa mitandao ya kijamii na blogu zinazodai kuwa za Kikristo, hata kama ni za kawaida tu, ili kutambua kile ambacho kinakwenda kinyume na kiinjili na ushuhuda ambao unatokea kupitia mtazamo wa wale wanaopinga migawanyiko, upinzani, kuwadhihaki wale ambao kimsingi makosa yao ni kufikiria vinginevyo.


Tukipanua mtazamo wetu, tunawezaje kutofikiria juu ya bahari ya chuki ambayo inaachiliwa na kulishwa na vita, ugaidi na vurugu zinazoendelea kudai waathirika wasio na hatia. Wakristo ni wafuasi wa Mwanadamu aliyeumbwa na Mungu ambaye alituomba tuwapende hata adui zetu. Mungu asiyehitaji ubaguzi wetu na hukumu za dharau kwa wengine, lakini anayejidhihirisha kwa kutukumbatia tunapokuwa na uwezo wa kulia na kupenda, tunapojiruhusu kutawaliwa na mateso ya wengine, tukiibuka kutoka katika mapovu ya kutojali, tunapowapenda walio mbali na wakati tunawaombea, badala ya kulalamika; tunatoa machozi kwa ajili ya  wale walio nje ya kile tunachoamini kuwa ni boma la wenye haki, waliookoka, wema, walio  na “mahali”, wale wanaoamini tayari wanajua kila kitu na kwa hiyo hawatarajii chochote tena.

Kwa Papa Fransisko aliwaambia mapadre  kuwa: “Hali ngumu tunazoona na uzoefu, ukosefu wa imani, mateso tunayogusa, kwa kugusa moyo uliovunjika usiamshe uthabiti katika mabishano, lakini uvumilivu katika huruma. Jinsi gani tunavyohitaji kuwa huru kutokana na ukali na kashfa, kutoka katika ubinafsi na tamaa, kutoka katika ukaidi na kutoridhika, kumwamini na kujikabidhi kwa Mungu, kutafuta ndani yake amani ambayo inaokoa kutoka katika kila dhoruba! Hebu tuabudu, tuombe na tulie kwa ajili ya wengine: tutamruhusu Bwana kufanya maajabu.”

Katika mkesha wa kurudiwa kwa sadaka  ya Golgotha, Wakristo, wenye dhambi waliosamehewa, hujifunza kutokana na machozi ya Petro kujitambua kuwa hivyo. Na kwa kujifungulia upendo ulio huru na usio na masharti ya Msulibiwa, wanajifunza kupendana na hivyo kuwa mashuhuda wa huruma katika ulimwengu usiosamehe; mashuhuda wa umoja katika ulimwengu wa mgawanyiko; mashuhuda wa amani katika ulimwengu ambamo jeuri na vita vinaonekana kuenea. Wanajifunza kuwa mashuhuda wa tumaini ambalo halitokani na uwezo wao na ujuzi wao, bali juu ya uhakika wa kile kilichotokea usiku wa Pasaka katika kaburi lile la Yerusalemu.

28 March 2024, 18:21