Tafuta

 Siku ambayo Balozi wa Vatican nchini Ethiopia Askofu Mkuu Camilleri alipowasili Ethiopia 2019. Siku ambayo Balozi wa Vatican nchini Ethiopia Askofu Mkuu Camilleri alipowasili Ethiopia 2019. 

Papa amemteua Askofu Mkuu Camilleri kuwa Balozi wa Vatican nchini Cuba!

Jumatatu tarehe 20 Mei 2024,Baba Mtakatifu Francisko amemteua Balozi wa Kitume nchini Cuba,Askofu Mkuu Antoine Camilleri,ambaye hadi uteuzi huo alikuwa ni Balozi wa Vatican nchini Ethiopia,Gibuti na msimamizi wa Kitume nchini Somalia.

Vatican News

Baba Mtakatifu Francisko Jumatatu tarehe 20 Mei 2024, amemteua Askofu Mkuu Antoine Camilleri, kuwa Balozi wa Vatican Nchini Cuna na ambaye hadi uteuzi huo alikuwa ni Balozi wa Vatican wa Ethiopia, Gibuti na Mwakilishi wa Kitume nchini Somalia.

Camilleri alizaliwa huko Sliema, Malta, tarehe 20 Agosti 1965, kupewa daraja la upadre tangu mwaka 1991 na mhitimu wa shahadai ya Sheria na Sheria za Kanisa. alijiungia katika huduma ya kidiplomasia ya Vatican mnamo tarehe  9 Januari 1999. Katika miaka ya hivi karibuni amefanya utume wake katika Uwakilishi wa Kipapa nchini Papua New Guinea, Uganda, Cuba na katika Kitengo cha Mahusiano na Mataifa ya Sekretarieti ya Vatican, ambapo Papa Msaafu Benedikto XVI alimteua kuwa katibu msaidizi mnamo  tarehe 22 Februari 2013.

Na kunako tarehe 3 Septemba 2019, Papa Francisko alimteua kuwa Askofu mkuu wa Kanisa la Skálholt na Balozi wa kitume wa Vatican. Tarehe 4 Oktoba 2019 alipewa  Daraja la uaskofu. Tarehe 31 Oktoba iliyofuata aliteuliwa kuwa Balozi wa kitume nchini Ethiopia na Djibouti, na kuwa mwakilishi maalum wa Umoja wa Afrika (UA) na Mwakilishi wa kitume nchini Somalia. Askofu Mkuu Camilleri anajua lugha saba: Kiitaliano, Kiingereza, Kihispania, Kifaransa, Kireno, Kiromania, Kirusi.

Papa amemteua Balozi wa Vatican Nchini Cuba
20 May 2024, 16:35