Carlo Acutis na G.Allamano ni miongoni mwa watakao tangazwa watakatifu!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Wakati wa Mkutano wa Baba Mtakatifu na Kardinali Marcello Semeraro, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Kuwatangaza Wenyeheri na Watakatifu, tarehe 23 Mei 2023 Papa ameridhia: muujiza unaohusishwa na maombezi ya Mwenyeheri Giuseppe Allamano, Padre na Mwanzilishi wa Shirika la Kimisionari la Consolata; alizaliwa Castelnuovo Don Bosco (Italia) tarehe 21 Januari 1851 na kufariki mjini Turin (Italia) tarehe 16 Februari 1926; - muujiza unaohusishwa na maombezi ya Mwenyeheri Carlo Acutis, Mlei; alizaliwa tarehe 3 Mei 1991 huko London (Uingereza) na alikufa tarehe 12 Oktoba 2006 huko Monza (Italia) kwa sababu ya saratani ya damu. Masalia yake yako Assisi.
Muujiza unaohusishwa na maombezi ya Mtumishi wa Mungu Giovanni Merlini, Kuhani na aliyekuwa Mkuu wa Shirika la Wamisionari wa Damu Azizi; alizaliwa Spoleto (Italia) tarehe 28 Agosti 1795 na kufariki huko Roma (Italia) tarehe 12 Januari 1873;-
Kifodini cha Mtumishi wa Mungu Stanislaus Kostka Streich, kuhani wa jimbo; alizaliwa tarehe 27 Agosti 1902 huko Bydgoszcz (Poland) na kuuawa kwa chuki kwa sababu ya imani yake tarehe 27 Februari 1938 huko Luboń (Poland);
Kifo cha kishahidi cha Mtumishi wa Mungu Maria Maddalena Bódi, Mlei; alizaliwa tarehe 8 Agosti 1921 huko Szgliget (Hungaria) na kuuawa kwa chuki kwa imani tarehe 23 Machi 1945 huko Litér (Hungaria);
Fadhila za kishujaa za Mtumishi wa Mungu Guglielmo Gattiani, Ndugu Mdogo Mkapuchini(OFMcap); alizaliwa tarehe 11 Novemba 1914 huko Badi, kijiji kidogo cha manispaa ya Castel ya Casio (Bologna) na alikufa huko Faenza (Italia) mnamo 15 Desemba 1999;
Fadhila za kishujaa za Mtumishi wa Mungu Ismael Molinero Novillo, anayejulikana kama Ismael wa Tomelloso, Mei; alizaliwa tarehe 1 Mei 1917 huko Tomelloso (Hispania) na alikufa huko Zaragoza (Hispania) tarehe 5 Mei 1938;
Fadhila za kishujaa za Mtumishi wa Mungu Enrico Medi, Mlei; alizaliwa tarehe 26 Aprili 1911 huko Porto Recanati (Italia) na alikufa huko Roma (Italia) mnamo 26 Mei 1974.
Zaidi ya hayo, Baba Mtakatifu Mkuu aliidhinisha kura nzuri za Kikao cha Kawaida cha Mababa wa Kardinali na Maaskofu kwa ajili ya kutangazwa kwa Mwenyeheri Emanuele Ruiz na Waandamani 7 wa Shirika la Ndugu Wadogo, na Francis, Abdel Mooti na Raffaele Massabki, Walei, waliouawa kwa sababu ya Imani yao huko Damasco (Siria) kati ya tarehe 9 na 10 Julai 1860.
Wakati huo huo katika mkutano huo waliamua kuitisha Baraza ambalo pia litahusu kutangazwa watakatifu kwa Wenyeheri: Giuseppe Allamano, Marie-Léonie Paradis, Elena Guerra na Carlo Acutis.