Tafuta

Siku ya 64 ya Hija ya Maaskari Jeshi huko Lourdes. Siku ya 64 ya Hija ya Maaskari Jeshi huko Lourdes. 

Gallagher:Vatican imehamasisha daima fadhila za ujasiri wa amani!

Askofu mkuu Paul Gallagher,Katibu wa Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa,katika maadhimisho ya Hija ya 64 ya Askari Jeshi Kimataifa iliyofanyika huko Lourdes,Ufaransa Mei 24-26alisema:“hali ya dunia inatia wasiwasi kwa sababu watengenezaji wa silaha wanaunga mkono na mizozo ya mafuta na maendeleo ya kiteknolojia kuchangia njia inayozidi kuwa baridi na iliyojitenga kwa janga kubwa la vita.”

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Askofu mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu wa Vatican, wa Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa akiwa katika hija ya 64 ya kijeshi ya kimataifa iliyofanyika huko Lourdes kuanzia tarehe 24 hadi 26 Mei 2024 alisema kuwa “Hali ya kijiografia ni ya wasiwasi na ya mgawanyiko kiasi kwamba inakuwa vigumu sana kukuza na kupandikiza amani katika akili na mioyo ya watu.  Hasa kwa sababu watengenezaji wa silaha wanaunga mkono na mizozo ya mafuta, na maendeleo ya kiteknolojia huchangia njia inayozidi kuwa baridi na ya kujitenga kwa janga kubwa la vita. Kwa njia hiyo inahitajika Diplomasia katika huduma ya amani, ya utu wa binadamu, diplomasia ya huruma.

Inahitajika ujasiri kufanya amani kuliko vita

Katika uzinduzi, Askofu Mkuu Gallagher alizungumza katika Mkutano wa Kimataifa wa Mamlaka wenye mada: “Ndege ya Njiwa”, mbele ya viongozi wa kijeshi, kiraia na kidini kutoka duniani kote. Kwa njia hiyo alisema kuwa katika nyanja ya kimataifa, Vatican daima imekuwa ikikuza fadhila ya ujasiri wa amani huku , akionesha kipengele cha kwanza cha diplomasia ya kipapa kwamba: “ inahitaji ujasiri zaidi kufanya amani kuliko kufanya vita,  ambavyo hatima yake  daima ni kushindwa. Unahitajika ujasiri wa kuchagua mikutano badala ya makabiliano, mazungumzo badala ya vurugu, mazungumzo badala ya uadui, uaminifu badala ya unafiki.

Ni jinsi gani ilivyo muhimu utendaji wa Umoja wa Mataifa

Katibu wa  Vatican wa Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa alisema, kuwa, “akirejea juu ya mtume Paulo, Papa Francisko anatutaka tutende kwa unyenyekevu, upole na uungwana  na  hili ni somo zuri kwa wale wote ambao, kama ninyi mnahusika kila siku kwenye uwanja wa uhusiano wa kikanda, kitaifa na kimataifa.” Kuhusu diplomasia ya kimataifa, Askofu Mkuu Gallagher alitarajia kuanzishwa upya kwa Umoja wa Mataifa na kwamba “Jinsi gani ni muhimu mageuzi ya utendaji wa Umoja wa Mataifa (hasa zaidi ya Baraza la Usalama), kwa njia ya uwakilishi zaidi na kwa kuzingatia mahitaji ya watu wote! Hili linahitaji kuungwa mkono na jumuiya nzima ya kimataifa na kurejeshwa kwa moyo wa Helsinki.”( Ikumbukwe huyo ni mmoja wa waanzilishi wa Umoja wa Nchi za Ulaya).

Vatican inaandamana na mataifa katika kujenga amani na udugu kati ya watu

Akiibua kipengele cha pili cha diplomasia ya Vatican, cha utumishi wa binadamu, Askofu Mkuu  Gallagher alidokeza kwamba “nyuma ya migogoro yote hii, mivutano yote hii, hali hizi zote kubwa za kibinadamu kuna wanadamu, wenye majina na ukoo.” Kwa kumweka binadamu kuwa kitovu cha shughuli zake, diplomasia ya kipapa inatafuta kufuata wito wake na kuwa juu ya mambo yoyote yale, kushughulikia mtu yeyote anayetafuta amani, maendeleo na heshima kwa haki za binadamu.  Wajibu huu hauchochewi na wasiwasi wa muda, lakini kwa njia ya kweli wa taalimungu ya diplomasia, kama njia ya kufikia amani, upendo na udugu. Kwa sababu ya utume wake wa hali ya juu ya kutangaza Injili na kukuza tunu za haki, ukweli na wema, Vatican  kwa hivyo linaandamana na Mataifa katika kujenga amani na udugu kati ya watu binafsi, lakini pia kati ya watu. Bila upendeleo, bila maslahi yoyote ya kibinafsi, Vatican inaweza kwa urahisi zaidi kuwa mpatanishi, alisisitiza  Askofu Mkuu.

Jitihada za Vatican kwa sauti yake na kuwa dira inayoongoza dhamiri

Ikiwa huru bila kuwa na tamaa yoyote ya kisiasa, kiuchumi au kijeshi, Vatican iliweza kugeuza umoja wake kuwa nguvu, na sauti yake kuwa dira inayoongoza dhamiri kupitia majanga ya ulimwengu huu. Katika historia ya Kanisa, ya jana kama ilivyo  leo, hii kuna watu wasiohesabika - waamini, watu watawa, wanasiasa - ambao wametumia hatua zao za kisiasa au za kidiplomasia kwa niaba ya huruma”, alisema Katibu wa Vatican wa Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa huku akizama katika kipengele cha tatu cha hoja zake. “Kwa hiyo kwa Kanisa, huruma pia imekuwa jamii ya kisiasa na kidiplomasia - na ilikuwa juu ya yote Papa Francisko ambaye aliunga mkono njia hii, ambayo inatuwezesha kufikia aina ya juu ya haki kwa kutetea kile ambacho ni sawa na kulaani udhalimu. Na kisha itawezekana kujenga uhusiano wa kina wa kibinadamu na wa kijamii ili kujenga ustaarabu wa upendo na kukuza utamaduni wa kukutana.” Kwa hivyo, diplomasia ya kipapa kama ilivyokua na kama ilivyoendelezwa kwa ubunifu na Papa Francisko, inaweza kuitwa diplomasia ya huruma. Kwa kuunganisha huruma na diplomasia, Papa anathibitisha tena kanuni ya kutoegemea upande wowote na kukataa kuhalalisha mmoja au mwingine wa wapiganaji. Umoja wa kutoegemea upande wowote, ulioanzishwa karne nyingi zilizopita na watangulizi wake, kwa hivyo Papa Fransisko anatajirishwa na mwelekeo huu mpya na kwa kukataa kukumbatia nafasi ya kisiasa ya mamlaka ya kipapa.” Alihitimisha.

Askofu Mkuu Gallagher naelezea Diplomasia ya Vatican
29 May 2024, 09:42