Kard.Parolin kuhusu China:Baraza la China lilikuwa“kielelezo kwa nchi nyingi za utume!
Na Salvatore Cernuzio - Vatican
“Papa ndiye kiongozi wa kiroho wa Wakatoliki wote duniani, bila kujali utaifa wao; lakini utii huu kwa Papa haudhuru tu upendo ambao kila mtu anapaswa kuwa nao kwa nchi yake, bali unaisafisha na kuihuisha.” Maneno haya, yaliyosemwa na Askofu Mkuu Celso Costantini, Mwakilishi wa kwanza wa Vatican nchini China, zaidi ya miaka mia moja iliyopita, yanafaa sana leo hii. Marehemu Askofu Mkuu alifafanua kwamba “umoja kama huo ndiyo hakikisho bora zaidi la imani iliyokingwa dhidi ya masilahi ya nje ya kisiasa na yenye kuunga mkono tamaduni na jamii ya mahali hapo.” Askofu Mkuu Costantini alifanya kazi bila kuchoka, licha ya matatizo, ucheleweshaji, na upinzani, ili kuhakikisha kwamba Injili ya Kristo inatia mizizi katika ardhi ya China na inapatana na jamii na utamaduni wa mahali hapo.
Askofu Mkuu Costantini pia aliandaa na kuitangaza Concilium Sinense, Sinodi ya kwanza na hadi sasa ya kipekee ya Kanisa Katoliki nchini China, ambayo maadhimisho ya miaka mia moja yameadhimishwa Jumanne, tarehe 21 Mei 2024. Maadhimisho hayo yaliadhimishwa katika Kongamano muhimu la kimataifa lilioandaliwa na Chuo Kikuu cha Kipapa cha cha Urbaniana Mjini, Vatican kwa ushirikiano na shirika la habari la za Kimisionari Fides na Tume ya Kichungaji ya China. Miongoni mwa wazungumzaji wakuu katika kikao cha asubuhi alikuwa Katibu wa Vatican Kardinali Pietro Parolin.
Waamini wema na raia wema
Ulikuwa mkutano wa elimu, sio wa kusherehekea, kama Gambera wa Chuo Kikuu cha Kipapa hicho Vincenzo Buonomo alivyoelezea katika utangulizi wake, uliotanguliwa na ujumbe wa video kutoka kwa Baba Mtakatifu Francis. Haikuwa “ujenzi upya wa kihistoria wa tukio hilo, lakini tafakari ya jinsi tukio la sinodi yenyewe hutumika kama msingi na marejeo ya utamadunisho unaoletwa na ujumbe wa Kikristo, ambao unaweza kuhakikisha uwepo wa wamini bora na wakati huo huo. raia bora.” Hili ndilo wazo ambalo Papa Francisko alisisitiza katika salamu zake kwa watu wa China wakati wa Misa ya kuhitimisha safari yake nchini Mongolia, ambayo Kardinali Parolin alisisitiza katika hotuba yake. Alikumbuka jinsi Askofu Mkuu Costantini alivyoandika maneno yasiyo na shaka juu ya hili zaidi ya karne moja iliyopita. "Papa anataka Wakatoliki wa China kupenda nchi yao na kuwa bora zaidi kati ya raia. Papa anapenda mataifa yote, kama Mungu, ambaye yeye ni mwakilishi wake; anaipenda China, taifa lenu tukufu na kuu, na hailiwekei chini ya jingine lolote.”
Thamani ya Concilium Sinense leo hii
Akitazama nyuma katika historia, Kardinali Parolin alisisitiza kwamba ingawa Baraza la Shanghai lilikuwa “baraza maalum;” ilishikilia “umaana mpana zaidi wa kikanisa.” Baraza la China lilikuwa “kielelezo kwa nchi nyingine nyingi za utume ambazo, kwa kufuata mfano wake, zingejitayarisha kusherehekea sinodi zao za kitaifa katika miaka iliyofuata.” Kardinali Parolin alisema, ukumbusho wa kile kilichotokea una “thamani kubwa” hata kwa wakati huu wa Kanisa, ambalo kwa mwaliko wa Baba Mtakatifu Francisko, linajishughulisha na tafakari ya sinodi, likiwaita Watu wa Mungu “kuwajibika na wahusika wakuu katika maisha ya Kanisa.” Huu ulikuwa uzoefu ule ule ambao Mababa wa Sinodi walikuwa nao kuanzia tarehe 15 Mei hadi Juni 12 huko Shanghai. “Tunafanana na wafanyakazi wenye kiasi wanaojenga Kanisa kuu,” alisema Askofu Mkuu Costantini. “Mchoro hutolewa na mbunifu, lakini kila mmoja huleta tofali lake kwenye ujenzi mkubwa. Kwetu sisi, mbunifu ni Papa. Wafanykazi wanapita, lakini Kanisa kuu linabaki.
Kutoka "Tume za Kigeni" hadi "Kanisa la Wamisionari"
Kardinali Parolin aidha alionesha mawazo haya katika muktadha ulioangazwa na mambo chanya lakini pia kutokuwa na usawa, yote mawili kwa sababu ya karibu uwepo wa kipekee wa mapadre wa kigeni na ushirikiano fulani wa mzunguko wa wamisionari kwa ufadhili ulioanzishwa na Utawala Mkuu wa Magharibi na njia za kichungaji kuamuliwa nayo.” Katika muktadha huo, Askofu Mkuu Costantini aliweka “mkakati” wake wa kimisionari na kidiplomasia, akiongozwa na Maximum Illud ya Papa Benedict XV, ambayo ilimpeleka kwenye “kusadikisho” kwamba anapaswa kufanya sinodi kuu ya Kanisa nchini China. Hata hivyo, kwanza, huku akitambua “sifa ya wamisionari wengi wa kigeni” ambao, kwa upendo na kujitolea, “walileta Injili China,” Askofu Mkuu Costantini alielewa kwamba kulihitaji kuwa na jitihada ya kuunganisha vizuri zaidi imani ya Kikatoliki katika maisha ya Wachina.
"Costantini aliona uharaka wa kuhama kutoka kwa dhana ya 'misheni za kigeni' hadi ile ya 'Kanisa la kimisionari'", Kardinali Parolin alisisitiza. Kwa hiyo, ilikuwa ni lazima kuendeleza kazi ya kuwaweka makasisi wazawa. Akiwa na nia hiyo, “aliunga mkono kuwekwa wakfu kwa maaskofu sita wa kwanza wa China katika 1926, na kwa kusudi lilo hilo, akaanzisha Kusanyiko la Wanafunzi wa Bwana mwaka uliofuata.” Pia alipendekeza kwa ufasaha namna za kisanii na usanifu wa Kichina, “ambazo kwazo kulezwa kwa imani ya Kikatoliki kungeweza kutokea zaidi.” Hakukuwa na uhaba wa ukosoaji na kampeni halisi ya vyombo vya habari dhidi yake, Kardinali Parolin alikumbuka. Lakini "kila mara alijibu shutuma kwa kuona mbele."
Kupyaishwa kwa makubaliano
Urithi wa Askofu Mkuu Costantini unafikia wakati wetu, ambao umeadhimishwa tangu 2018 kwa kuimarishwa kwa uhusiano wa maelewano kati ya Jimbo Kuu la Mtakatifu na Jamhuri ya Watu wa China kupitia makubaliano ya muda ya uteuzi wa Maaskofu. Ni makubaliano kwamba "sote tuna nia ya kufanya upya na pia kuendeleza baadhi ya pointi," alisema Kardinali Parolin kando ya mkutano huo. Wakati huo huo, Kadinali alionyesha matumaini yake ya kuwa na "uwepo thabiti nchini Uchina." "Hata kama mwanzoni inaweza kuchukua fomu ya uwakilishi wa papa au nunciature ya kitume, bado inaweza kuongeza na kuimarisha mawasiliano yetu. Hili ndilo lengo letu.”
Kanisa la lililotamadunishwa
Maneno haya yamesemwa na Kardinali Parolin pamoja na Askofu wa Shanghai, Giuseppe Shen Bin. "Tutaendelea kulijenga Kanisa nchini China kuwa Kanisa takatifu na Katoliki linalopatana na mapenzi ya Mungu, linalokubali urithi bora wa kitamaduni wa jadi wa China, na linakaribishwa na jamii ya China leo," alisema askofu huyo. Askofu wa China alitaja mambo manne kwa ajili ya sasa ya Kanisa Katoliki katika nchi yake Kwanza, alisema, “maendeleo ya Kanisa nchini China lazima yawe ya uaminifu kwa Injili ya Kristo,” na kwa hiyo kwa “imani ya Kikatoliki ya kimapokeo.” Mnamo 1949, mwaka wa kuanzishwa kwa Uchina mpya, Kanisa "sikuzote lilibaki mwaminifu kwa imani yake ya Kikatoliki, huku likijitahidi kuzoea mfumo mpya wa kisiasa." Na wakati huo, “sera ya uhuru wa kidini iliyotekelezwa na serikali ya China haikutaka kubadili imani ya Kikatoliki bali ilitumaini kwamba makasisi na Wakatoliki waaminifu wangetetea masilahi ya watu wa China na kujikomboa kutoka kwa udhibiti wa mataifa ya kigeni.”
Matatizo ya zamani
Askofu Shen Bin alikumbuka kwamba aliyekuwa Katibu Mkuu wa Baraza la Serikali wakati huo, Xi Zhongxun, alihakikisha kwamba serikali ya China haiwapingi Wakatoliki wa nchi hiyo kuwa na mawasiliano ya kidini na Vatikani, lakini hawa, lisema, "waliruhusiwa kwa sharti tu kwamba hawakuenda kinyume na masilahi ya watu wa China, hawakukiuka enzi kuu ya China, na kwamba Vatikani ilibadilisha sera yake ya chuki dhidi ya China." Askofu wa Shanghai pia alikumbuka matatizo ya zamani kati ya Kanisa na Serikali nchini China, kwa kiasi fulani kutokana na “hisia yenye nguvu ya ubora wa kitamaduni wa Ulaya” ya baadhi ya wamishonari, ambao “hata walikusudia kutumia dini ya Kikristo kubadili jamii na utamaduni wa China.” Hilo “lilipingwa bila kuepukika na hata kuchukiwa na Wachina wengi” na “kuzuia kuenea zaidi kwa Injili ya upendo miongoni mwa Wachina.”
Mapadre na walei wapende nchi na Kanisa lao
Leo, watu wa China wanapofuatilia “uhuishaji mkubwa wa taifa la China kwa ukamilifu na uboreshaji wa mtindo wa Kichina,” Kanisa Katoliki “lazima lielekee upande uleule,” alithibitisha Askofu Shen Bin, “kutofuata njia ya upotoshaji inayopatana na jamii na tamaduni za Kichina leo hii". Kwa hiyo aAliwaalika mapadre na waamini wa China “kuipenda nchi yao na Kanisa lao na kuunganisha kwa ukaribu maendeleo ya Kanisa na ustawi wa watu.” Kuhusiana na hilo, alinukuu maneno ya Papa Francisko kwamba: “kuwa Mkristo mzuri hapatani tu na kuwa raia mwema, bali ni sehemu yake fungamani.”
Wazungumzaji wawili wa kike
Wanawake wawili walikuwa miongoni mwa wazungumzaji katika mkutano huo katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Mjini Roma. Mmoja wao alikuwa Zheng Xiaoyun, rais wa Taasisi ya Dini Ulimwenguni katika Chuo cha Sayansi ya Jamii cha China, ambaye alibainisha kwamba "leo hii nchini China, kulingana na serikali, kuna majimbo 98, taasisi 9, makanisa 6,000, na waamini milioni 6, zaidi ya 8,000 ni watawa chini ya “hakikisho kamili la uhuru wa kidini.” Aidha Alionesha matumaini ya kupyaishwa kwa Mkataba kati ya China na Vatican. Baadaye, Profesa Elisa Giunipero, mhadhiri wa Historia ya Kichina katika Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Milano, Italia, alikumbuka “uvutano mkubwa na ambao mara nyingi hupuuzwa na tume za Kikatoliki nchini China na ulimwenguni kote.” "Kutoka katika Kanisa nchini China kumekuja msukumo wa mabadiliko ambayo yamelibadilisha Kanisa katika maeneo ya utume na kusaidia kufikiria Kanisa la ulimwengu wote ambalo "sio tena mbeba utamaduni wa Ulaya,"alsisitiza. Kwa hiyo “Vatican, katika uimara wake na hatua ya kusherehekea Baraza hilo ... iliweka imani yake kwa mapadre wazawa wa China." “Hii, ilisaidia sana Kanisa kustahimili matatizo katika miongo iliyofuata.” Alihitimisha.