Tafuta

2024.05.27 Kardinali Parolin aliadhimisha misa katika kumbu kumbu ya Siku ya 61 ya Afrika Kimataifa. 2024.05.27 Kardinali Parolin aliadhimisha misa katika kumbu kumbu ya Siku ya 61 ya Afrika Kimataifa.   (Vatican Media)

Kard Parolin:Watu wapewe vipaumbele kuliko mali na Afrika imejaa ubinadamu!

Kardinali Parolin aliadhimisha Misa kwa ajili ya Siku ya 61 ya Afrika Duniani katika Basilika ya Mtakatifu Maria Mkuu jijini Roma,mbele ya mabalozi na mapadre wengi wa Afrika.Katibu wa Vatican alisema kuwa Bara la Afrika lina uwezo na rasilimali za kukabiliana na changamoto hizo lakini lazima kuwaweka mbele na ustawi wao kuliko mali na madini.

Na Stanislas Kambashi na Angella Rwezaula - Vatican.

Afrika ni nchi ya matumaini licha ya changamoto zake nyingi. Ni Bara ambalo linaweza kugeuzwa kuwa bara la haki na amani.  Hayo yalisema na Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican wakati wa mahubiri yake kwenye misa aliyoingoza, Jumatatu tarehe 27 Mei 2024 katika fursa ya kuadhimisha Siku ya 61 ya Afrika ambayo hufanyika kila tarehe 25 Mei ya kila mwaka. Maadhimisho hayo yaliwaleta pamoja makumi ya Waafrika katika Kanisa kuu la Mtakatifu maria Mkuu, Roma, ambako balozi wa kwanza wa Afrika mjini Vatican alipumzishwa. Hata hivyo katika afla hiyo pia alizungukwa na maaskofu wengine, akiwemo Askofu Mkuu Fortunatus Nwachukwu, Katibu Mkuu wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji, Askofu Mkuu  Rolandas Makrickas, Mwakilishi wa Baba Mtakatifu katika Kanisa Kuu la Bikira Maria Mkuu, Mapadre wengi wa Kiafrika pia walishiriki. Vilevile maadhimisho hayo ni katika kuheshimu Balozi wa kwanza wa Kiafrika aliyeidhinishwa Vatican , António Manuel N'vunda, aliyezikwa kwenye moja ya makaburi yaliyomo kwenyer Kanisa Kuu hilo mnamo Januari 1608.

Ibada ya Misa ya katika fursa ya kuadhimisha miaka 61 ya Siku ya Afrika
Ibada ya Misa ya katika fursa ya kuadhimisha miaka 61 ya Siku ya Afrika

Kwa njia hiyo misa ilitanguliwa na heshima ya kuweka shada mbili za maua na wanadiplomasia wa Kiafrika kwenye kaburi la Papa Paulo V, katika Kikanisa cha Paulo na kwenye kaburi la Balozi huyo António N'Vunda lililoko chini ya Kanisa Kuu hilo. Katika mahubiri yake, Kardinali Parolin, awali ya yote, alieleza utajiri mwingi ambao bara la Afrika limesheheni: kiroho, kibinadamu, kiutamaduni na asili. Kisha alizungumzia juu ya maendeleo yaliyofikiwa na changamoto zinazolikabili bara hilo, hasa kuhusu amani na maendeleo.

Misa katika fursa ya miaka 61 ya Siku ya Afrika
Misa katika fursa ya miaka 61 ya Siku ya Afrika

Akirejea maneno ya Papa Benedikto wa kumi na sita katika Waraka wa Kitume wa  Africae Munus, wa baada ya Sinodi kuhusu Kanisa Barani Afrika katika huduma ya upatanisho, haki na amani, Katibu wa Vatican alikumbuka historia chungu ambayo imekwamisha kwa kiasi kikubwa maendeleo ya Afrika, ikiwa ni pamoja na makovu ya mapambano ya kidugu, utumwa na ukoloni mamboleo  unaoendelea kwa namna nyingi. Zaidi ya kila kitu, aliendelea kusema kuwa kuna sababu nyingi za matumaini na shukrani. Afrika inadumisha furaha ya kuishi, bado kuna wengi waliozaliwa, familia ni ya thamani kubwa, imejaa mali nyingi za wanadamu, maadili ya kiakili na kiutamaduni ambayo lazima yahifadhiwe. Ulimwengu unahitaji Afrika,” Kardinali alisema. “Afrika inachukua nafasi muhimu katika moyo wa diplomasia wa Vatican.

Wakati wa Misa katika fursa ya Siku ya 61 ya Afrika Kimataifa
Wakati wa Misa katika fursa ya Siku ya 61 ya Afrika Kimataifa

Ni kutokana na mtazamo huo chanya, inafaa kuadhimisha kumbukizi ya Balozi wa kwanza wa Afrika katika mahali Patakatifu, mwanzilishi wa Diplomasia ya Afrika jijini Vatican,” alisisitiza Katibu wa Vatican.  António Manuel N'Vunda alitumwa kwa Papa kuanzisha ripoti kulingana na mazungumzo na maadili ya Kikristo ambayo tayari yalikuwapo  katika Ufalme wa Congo. Baada ya safari ndefu iliyompeleka Brazili, Hispania na Ureno, alifika Roma akiwa amechoka na kufariki  kwenye siku kuu ya  Epifania  mnamo 1608. Kumbukumbu yake inakumbusha hali ya maisha ya kidiplomasia hasa kupitia kazi ya subira, na ambapo wanadiplomasia wanatafuta kuanzisha uhusiano wa kibinadamu ili kuimarisha mahusiano, kufanya kazi kwa ajili ya upatanisho, haki na amani,” Alithibtisha  Kardinali Parolin ambaye alionesha kwamba mataifa 50 ya Afrika yana uhusiano na Vatican. Vile vile alisisitiza kuwa "Afrika inachukuwa nafasi muhimu katika moyo wa diplomasia ya Vatican," kabla ya kuhitimisha na sala kwa Bikira Maria Mtakatifu ya Mtakatifu, iliyotungwa na  Mtakatifu Yohane Paulo II, katika Waraka wake wa Kitume wa Ecclesia in Africa yaani (Kanisa barani Afrika), huku akiomba kwa "maombezi ya Mama wa Mungu ili Afrika igeuzwe kuwa bara la haki na amani."

Antonio Manuel N’Vunda, Jumba la kumbukumbu la diplomasia ya Afrika

Katika neno lake la shukrani, Balozi wa Cameroon Bwana Antoine Zanga, mkuu wa mabalozi wa kundi la wakazi wa Afrika waliyoidhinishwa na Vatican alionesha kuwa Siku ya Afrika inalenga hasa kuwaleta Waafrika pamoja, kuhamasisha juu ya changamoto za bara hilp na kuifanya Afrika ijulikane kwa wengine.  Heshima iliyotolewa  kwa Nsaku Ne Vunda inalenga kushuhudia ukale wa uhusiano wa kidiplomasia kati ya Afrika na Vatican, lakini pia ni jukumu la kumbukumbu kuhamasisha vizazi vijavyo. Mapapa watatu waliofuatana wakati wa safari iliyomleta mkuu huyu wa Ufalme wa Congo hadi Vatican walikuwa ni  Papa Clement VIII, Papa Leo XI, Papa Paul V. Licha ya safari hiyo iliyojaa mitego, Manuel N'Vunda alionesha nia ya kukutana na Papa.   Kwa njia hiyo: “Na awe jumba la kumbukumbu kwetu”, ninaomba mfano wake uwatie moyo wanadiplomasia katika kutetea haki yao”, alisema hayoBalozi Antoine Zanga, ambaye pia alimtaja Papa Francisko, anayendekeza "diplomasia ya mwanadamu kwa mwanadamu na sio udhibiti wa maeneo ya madini."

Kuongeza ufahamu kuhusu nafasi ya Afrika katika ulimwengu

Siku ya Afrika Duniani kwa kawaida imekuwa ikiadhimishwa kila mwaka tangu 1963, ambayo ni tarehe ya kuanzishwa kwa Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU), ambao ulikuja kuwa Umoja wa Afrika (AU) mnamo mwaka 2002.  Ni fursa kwa wanadiplomasia kuongeza ufahamu kuhusu nafasi ya Afrika duniani. Ni kwa nia hiyo ambapo mabalozi wa kundi la wakazi wa Afrika walioidhinishwa na Vatican walitaka, mwaka huu, kukumbuka tukio la kihistoria lililotokea zaidi ya miaka 400 iliyopita, ambalo lilimulika uhusiano wa kihistoria kati ya Vatican na Bara la Afrika.

Mwanadiplomasia wa kwanza Mwafrika Vatican

Mwanadiplomasia huyu kijana mcha Mungu, mwenye adabu na mpole, alitumwa mnamo mwaka wa 1604 na Mfalme Álvaro II Mpanzu de Nimi wa Ufalme wa Congo (alibadilika  kuwa Mkristo), ambaye eneo lake wakati huo lilikuwa ndani Afrika ya kati na leo liko kaskazini mwa Angola, magharibi mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, na kusini mashariki mwa Gabon, kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia na Vatican. Mwishoni mwa safari ya hatari, ambayo alitoroka kutoka kwa wakuu na Baraza la Kuhukumu, Wazushi, Balozi huyo alifika Roma, akiwa mgonjwa na amechoka, na akakaribishwa kwa uchangamfu na Papa Paulo V.  Akiwa amewekwa mjini Vatican na kuzungukwa na madaktari bora, alifariki dunia siku chache baada ya mkutano wake na Baba Mtakatifu, ambaye alitaka kumheshimu kwa kuamuru azikwe huko katika Basilika ya Mtakatifu Maria Mkuu ambayo ilikuwa ni Basilika  yenye kuongozwa na taji la Kihispania wakati ule.

Siku ya 61 ya Afrika Duniani
Siku ya 61 ya Afrika Duniani
Kard.Parolin na Siku ya Afrika Duniani
28 May 2024, 13:40