Kuelekea WYD huko Seoul 2027, na “Christus vivit” kujifunza kutoka kwa mwingine
Vatican News
Takriban wajumbe 300 kutoka Mabaraza ya Maaskofu kutoka nchi 110 watashiriki huko Ciampino, mjini Roma kuanzia tarehe 23 hadi 25 Mei 2024 , katika makao ya "Il Carmelo, katika Kongamano la Kimataifa la Vijana kwa kuongoza na mada: “Kwa huduma ya uchungaji wa vijana kisinodi: mitindo mipya na mikakati ya uongozi,” iliyoandaliwa na Baraza la Kipapa lwa ajili ya Walei, Familia na Maisha(DLFV). Kongamano hilo ni wakati muhimu katika kuadhimisha miaka mitano tangu kuchapishwa kwa Waraka wa Kitume wa Christus vivit, ulioandikwa baada ya Sinodi ya Vijana mnamo mwaka 2018, na ambayo Baraza la Kipapa la Walei, Familia na Maisha (DLFV) wamejikita kwa ajili ya yao mwaka 2024. Shughuli zilizotekelezwa ni pamoja na kampeni ya mitandao ya kijamii kupitia akaunti rasmi ya Siku ya Vijana Duniani na maadhimisho ya miaka 40 tangu mkutano wa kwanza wa vijana na Papa katika Uwanja wa Mtakatifu Petro mnamo mwaka 1984. Mipango hii, pamoja na matukio mengi ya kijimbo katika sehemu mbalimbali za dunia, inalenga kuimarisha huduma ya vijana na kuibua tafakuri ya kiroho miongoni mwa vijana, kuanzia ishara zilizotolewa na Waraka wa Christus vivit.
Mada za kongamano
Kongamano la Kimataifa la Kichungaji la Vijana lnajikita kwa siku tatu za mafunzo na kutafakari baadhi ya mada za mawaidha yaliyoelekezwa kwa vizazi vipya ambayo ni ya msingi kwa ajili ya huduma ya kichungaji, ikijumuisha uhusika wa vijana, sinodi, mafunzo na uandamani wa kiroho. Kila mada itashughulikiwa kuanzia utangulizi utakaotolewa na mtaalam wa masuala ya uchungaji. Mada zilizopendekezwa zitachunguzwa kwa kina katika vikundi vya kushiriki, kufuatia mbinu ya utambuzi wa kiroho iliyoanzishwa na Sandra Chaoul, wa Lebanon, mkurugenzi wa Mtandao unaosindikiza Mpango wa Uongozi wa Utambuzi. Miongoni mwa wazungumzaji ni Profesa Gustavo Fabian Cavagnari, profesa wa Uchungaji wa Vijana katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Salesian, Profesa Gustavo Fabian Cavagnari, Padre Christopher Ryan, mkurugenzi wa Kituo cha Areté cha Uongozi wa Kimisionari nchini Australia, na Brenda Noriega, kutoka Marekani, mjumbe wa Jumuiya ya kwanza ya Kimataifa. Baraza la Ushauri la Vijana (IYAB) la DLFV, lenye uzoefu mkubwa katika michakato ya kuwafunza vijana katika imani.
Mpango
Siku ya kwanza ya Kongamano itafunguliwa na kikao: “Kutoka WYD huko Lisbon 2023 hadi WYD huko Seoul 2027.” Baada ya salamu za utangulizi kutoka kwa Kadinali Kevin Farrell, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Walei, Familia na Maisha, watajikita na tafakari na tathmini ya matukio muhimu ya Siku ya Vijana Duniani huko Lisbon 2023. Wakati wa kushirikishana ambao utasherehekea mafanikio yaliyopatikana na ambao pia utafanya kama daraja kuelekea toleo lijalo la mkutano wa kimataifa wa vijana utakaofanyika Seoul mnamo 2027. Kisha, Kardinali Américo Alves Aguiar, Askofu wa Setúbal, Ureno, na Askofu Mkuu Peter Soon-Taick Chung, wa Jimbo Kuu katoliki la Seoul, watazungumza kuhusu uzoefu wao na kutoa maono ya matarajio na ubunifu kwa ajili ya mkusanyiko ujao wa vijana. Pia Watazungumzia kuhusu Jubilei ya Vijana ya mwaka 2025, iliyopangwa kuanzia tarehe 28 Julai hadi 3 Agosti, ambapo Baba Mtakatifu Francisko anawaalika vijana kutoka sehemu mbalimbali za dunia kuja Roma, akiwataka kuwa “mahujaji wa matumaini.”
Maelezo yatatolewa na Askofu Mkuu Fisichella
Kuonesha maelezo ya uteuzi huu muhimu itakuwa Askofu Mkuu Rino Fisichella, Mwenyekiti shirikishi wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Uinjilishaji, ambaye atawasilisha mipango na shughuli zilizopangwa. Kongamano hilo litakamilika Jumamosi, tarehe 25 Mei 2024, kwa uteuzi wa mara mbili: kwanza kabisa kutakuwa na Mkutano na Baba Mtakatifu Francisko asubuhi na mazungumzo ya wazi na Sekretarieti Kuu ya Sinodi na pili: mchana ambayo yatamhusisha Sista Nathalie Becquart, katibu mkuu wa Sinodi ya Maaskofu.