Tafuta

2024.05.20 Mkutano wa uwakilishi wa Congamano la Ekaristi Takatifu Kimataifa(IEC 2024) litakalofanyika huko Quito. 2024.05.20 Mkutano wa uwakilishi wa Congamano la Ekaristi Takatifu Kimataifa(IEC 2024) litakalofanyika huko Quito. 

Kongamano la Ekaristi huko Quito,Amerika ya Kusini:sauti ya udugu kwa Kanisa

Toleo la 53 la tukio la kimataifa lililopangwa kuanzia tarehe 8 hadi 15 Septemba 2024 nchini Ecuador lenye mada:“Udugu wa Kuponya Ulimwengu” liliwasilishwa katika Ofisi ya Habari ya Vatican.Askofu Mkuu Espinoza Mateus:“Itatangazwa kwa kila mtu kwamba udugu ndiyo njia pekee inayowezekana ya kuunda na kujenga ulimwengu mpya.”

Osservatore Romano

Kongamano la Ekaristi Takatifu litakalofanyika huko Quito nchini Ecuador lazima "sauti hiyo yenye lafudhi ya Amerika Kusini kwa Kanisa lote ulimwenguni isikike": kwa hiyo, itakuwa “sauti ya matumaini inayojitangaza yenyewe kutoka katika bara hili la matumaini.” Hivi ndivyo alisema Msalesian Alfredo José Espinoza Mateus, Askofu mkuu wa Quito na rais wa Kamati ya eneo hilo, wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuwasilisha Kongamano la 53 la Ekaristi la Kimataifa (Iec 2024).

Mkutano wa kikanisa utafanyika katika mji mkuu wa Ecuador, kuanzia tarehe 8 hadi 15 Septemba, kwa mada “Udugu wa kuponya ulimwengu - Ninyi nyote ni ndugu (Mt 23, 8)". Mkutano huo, aliongeza kiongozi huyo  pia utajaribu kuwa "sauti ya kinabii ambayo itatangaza kwa kila mtu kwamba udugu ndio njia pekee inayowezekana ya kuunda na kujenga ulimwengu mpya". Akizungumzia mada hiyo, askofu mkuu alisisitiza kwamba haiwezi kukataliwa kuwa kuna majeraha mengi duniani; lakini - aliuliza - tunawezaje kuwatazama ndugu na dada zetu wanaoteseka? Hivyo mwaliko wa kutafakari kama tunaweza kusikiliza sauti za wale wanaolilia majeraha yao na kuwaponya, na kuwa "wamisionari wa Ekaristi" wa udugu.

Askofu Mkuu Espinoza Mateus alikumbuka, kuwa Baba Mtakatifu Francisko, anatualika kuota kama ubinadamu mmoja, "kama watoto wa nchi hii ambayo inatuhifadhi sisi sote, kila mmoja na utajiri wa imani yake", kila mmoja kwa "sauti yake, ndugu na dada wote" . Alisema, hii ndiyo maana kubwa ya bunge. Kwa hakika, Ekaristi inaongoza "kuwa wajenzi wa udugu". Kongamano hilo litatufanya tufahamu kikamilifu kuwa "wamisionari wa Ekaristi ya udugu". Baadaye, Padre Juan Carlos Garzón, katibu mkuu wa Kongamano, alisisitiza kwamba mada hiyo inaibua andiko la Fratelli tutti na sanjari na maana ya kikanisa ya Ekaristi, « chanzo cha ushirika kwa wale wanaoiadhimisha, pamoja na utume wake wa kufanya kazi ya uponyaji ya Kristo katika majeraha ya ulimwengu." Waraka huu wa kimsingi, alisema, ulitungwa na Tume ya Kitaalimungu ya Kongamano la Ekaristi Takatifu na Kamati ya Kipapa ya Makongamano ya Kimataifa ya Ekaristi, kwa lengo la kuangazia “kiini cha Ekaristi katika maisha ya Kanisa” na “kuhimiza kuimarisha kiteolojia, upyaisho wa kiroho na wema wa Kanisa fulani".

Hatimaye, Montfortian Corrado Maggioni, Mwenyekiti wa Kamati ya Kipapa ya Kongamano la Kimataifa la Ekaristi, alirejea historia ya matukio haya ya Kikanisa.  "Wazo la kuwaita watu kutoka nchi mbalimbali kwenye kongamano ili kuadhimisha Ekaristi na kutafakari umuhimu wake wa kikanisa na kijamii - alieleza - lilikuwa na nia ya tangu mwanzo ya kufufua ufahamu kwamba uwepo wa Kristo kati yetu. na kupitia kwetu ni moyo wa Kanisa na utume wake." Kwa hakika, inahusu Makanisa yote, kila parokia, katika nchi zote. Kwa kweli, alisema, akikusanyika kwa Ekaristi, "pamoja na hisia tofauti, tamaduni, historia, licha ya tofauti za lugha, labda na majeraha bado wazi kutokana na uhasama wa kindugu", inamaanisha kulenga "chachu pekee inayoweza kutia chachu historia ya mwanadamu, na kuifanya unga mpya wa Ufalme wa mbinguni". Asili ya kimataifa ya kongamano, alisisitiza, "inadhihirisha umoja wa Fumbo la Ekaristi ambalo linaunda kila mtu aliyebatizwa, katika hali yake ya maisha, kama kila familia ya Kikristo, jumuiya ya kidini, parokia, dayosisi".

Mji wa Quito kwa hiyo "utavaa na kupanua hema zake ili kuwa mwenyeji, katika Kongamano la 53 la Ekaristi, wajumbe kutoka Makanisa mbalimbali dulimwenguni, kote hasa kutoka Amerika ya Kusini". Wakati huo huo, uteuzi wa Kardinali Kevin Farrell, Mwenyikiti wa Baraza la Kipapa la Walei, Familia na Miahsa kama Mwakilishi wa Baba Mtakatifu katika maadhimisho hauo ya Kongamano la Ekaristi huko  Quito ulichapishwa.

21 May 2024, 18:07