Papa amekutana na marais wa Bulgaria na Macedonia Kaskazini
Vatican News
Mikutano ya asubuhi ya Alhamisi tarehe 23 Mei 2024, kati ya Papa Francisko na, na Rumen Radev, rais wa Bulgaria, na Bi Gordana Siljanovska-Davkova, rais wa Jamhuri ya Makedonia Kaskazini.
Kwa wote walipokelewa katika Jumba la Kitume mjini Vatican kwa mikutano yao tofauti. Viongozi hao mara baada ya kukutana na Papa Francisko pia walikutana na Katibu wa Vatican, Kardinali Pietro Parolin.
Mazungumzo kati ya Papa na Radev
Papa Francisko alizungumza na Rais Radev kwa dakika 35 katika Ukumbi wa Maktaba. Wakati wa kupeana zawadi Papa alimpatia mkuu wa nchi ya Bulgaria sanamu ya shaba inayoitwa: “Mazungumzo kati ya vizazi, hati za upapa, Ujumbe wa Amani wa mwaka huu 202e, kitabu juu ya Statio Orbis ya 27 Machi 2020, kilichohaririwa na LEV. Kwa upande wake, Rais Radev alitoa Picha ya Watakatifu Cyril na Methodius kwa Papa.
Mazungumzo kati ya Rais Siljanovska-Davkova na Papa
Mazungumzo ya faragha kati ya Papa Francisko na Siljanovska-Davkova , Rais wa Jamhuri ya Macedonia pia yalichukua dakika thelathini na tano, (35) ambaye kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa msemaji wa Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Vatican, Dk. Matteo Bruni –alsisitiza na kukumbuka kuwa Makedonia ya Kaskazini ni nchi ya Mtakatifu Teresa wa Calcutta.
Wakati wa kutoa zawadi Papa Francisko alimpa rais nakala ya Picha ya shaba yenye kichwa “Karibu,” hati za upapa, Ujumbe wa Amani wa mwaka huu 2024 kitabu cha Njia ya Mslaaba ( Statio Orbis) cha tarehe 27 Machi 2020, kilichohaririwa na Nyumba ya ya Kuchapisha Viuabu Vatican (LEV.) Kwa upande wake, kiongozi wa Macedonia Kaskazini aliwasilisha kwa Papa Picha ya Bikira misaada ya mbao, ambayo ni kazi ya mafundi wa ndani.