Papa amemteaua Askofu wa Jimbo la Wa nchini Ghana!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko Jumatano tarehe 22 Mei 2024 amemteua kuwa Askofu wa Jimbo la Wa nchini Ghana, Padre Francis Bomansaan,M.Afr.,ambaye hadi uteuzi alikuwa makamu Mkuu wa Shirika la Wamisionari wa Afrikawajulikanao(White Fathers).
Wasifu wake
Padre Francis Bomansaan, M. Afr., alizaliwa tarehe 19 Januari 1962 huko Kaleo, katika Jimbo la Wa. Alijiunga katika Jumuiya ya Wamisionari wa Kiafrika mnamo mwaka 1983 na kumaliza mafunzo yake ya kitawa na kipadre katika nchi mbalimbali. Alifunga Nadhiri zake za Daima mnamo tarehe 7 Desemba 1990 na akapewa daraja la Upadre mnamo tarehe 27 Julai 1991. Alipata Diploma kadhaa, zikiwemo za Tasaufi ya matakatifu Ignatian, katika Kituo cha Kijesuit, Liverpool; katika mafunzo ya Kiroho na kimwili na Ushauri (M.A.), huko Chicago Marekani; katika ustadi wa ushauri wa Kiroho na kuishi kwa Jamii, katika Taasisi ya Mtakatifu Anselm, London; na Mpango wa Huduma ya Malezi ya Kitawa katika Nyumba ya huko, Dublin.
Ameshika nyadhifa zifuatazo: Padre wa Parokia katika Jimbo Kuu la Mbeya, Tanzania (1991-1993); Mkurugenzi wa Uhuishaji wa Ufundi na Mkufunzi huko Lublin, Poland (1995-1998); Mkurugenzi wa Ufundi wa Wamisionari wa Afrika nchini Ghana na Mshauri wa Kwanza wa Kanda ya Ghana na Nigeria (1999-2003); Mkufunzi na Bursar katika Chuo cha Mtakatifu Edward huko London (2004-2005); Mkuu wa Kanda ya Ghana na Nigeria (2005-2011); Mwalimu wa Manovisi katika Nchi za zinazozungumza kiingerza huko Zambia (2012-2019);Mkuu wa Kituo cha Makaribisho ya wenye kuhitaji msaada wa kupona kisaikolojia Kenya (2021-2022). Na tangu 2022 amekuwa Makamu Mkuu wa Shirika la Wamisionari wa Afrika.