Sanaa:“Msalaba wa Furaha” wa Mimmo Paladino kwa Siku ya Watoto Duniani!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Msalaba mkubwa na picha za utamaduni wa Kikristo, zaidi ya mita 4 kwenye juu na wa kipekee kwa aina yake, ni kazi ya msanii na mwalimu wa Transavantgarde ya Kiitaliano, Mimmo Paladino, iliyoundwa kwa ajili ya Siku ya kwanza ya Watoto Duniani. Tukio hilo litafanyika tarehe 25 na 26 Mei mbele ya Papa Francisko na karibu watoto elfu 70.
“Ni heshima kubwa kwangu kuunda “Msalaba wa Furaha” wa kwanza katika historia -alisema Paladino kwamba kazi hiyo inalenga moja kwa moja kwa watoto, kwa sababu wao ni wahusika wakuu wa kweli wa tukio hilo. Kwa hiyo katika usanii huo unapatikana vipengele vya historia na utamaduni wa Kikristo vinavyowakilishwa, lakini pia madokezo ya hadithi, kwa lengo la kuchochea mawazo yao hasa watoto na yetu.
Msalaba, uliotengemezwa katika takriban mwezi mmoja wa kazi, utafichuliwa kwa washiriki wakati wa sherehe za ufunguzi wa Siku ya Watoto Duniani, Jumamosi tarehe 25 Mei, kwenye Uwanja wa Olimpiki mjini Roma. Kisha kazi hiyo italetwa kwenye Uwanja wa Mtakatifu Petro, mjini Vatican wakati wa kuhitimisha tukio hilo tarehe 26 Mei 2024 na sherehe ya Ekaristi inayotarajiwa kuongozwa na Baba Mtakatifu Francisko.
Siku ya Watoto Duniani inayotarajiwa sana na Baba Mtakatifu Francisko, inafadhiliwa na Baraza la Kipapa la Utamaduni na Elimu na kuratibiwa na Padre Enzo Fortunato (OFMconv)kwa ushirikiano na Aldo Cagnoli, Jumuiya ya Mtakatifu Egidio na Chama cha Auxilium. Bado inawezekana kujiandikisha kwenye tovuti rasmi ya tukio www.giornatamondialedeibambini.org- www.worldchildrenday.org.