Tafuta

2024.05.22 Uwakilishi wa Matokeo ya kazi ya kusikiliza na kazi ya uangalizi wa Wanawake duniani 29 Mei 2024. 2024.05.22 Uwakilishi wa Matokeo ya kazi ya kusikiliza na kazi ya uangalizi wa Wanawake duniani 29 Mei 2024.  (UMOFC)

Umofc na Wwo,Sr Ogundeph:Tunaweza kugusa maisha ya wanawake!

Uwakilishi wa Matokeo ya Uangalizi wa Wanawake duniani tarehe 29 Mei 2024,mjini Roma,utakaoongozwa na mada:Utume wa wanawake katika Kanisa la Kisinodi:Changamoto na michango inayosikiliza Roho.Mhusika wa Jumuiya ya Afrika kwa ajili ya Uangalizi huo kutoka Kenya amefafanua kwa Vyombo vya Habari vya Vatican kuhusu kazi hasa ya kusaidia wahanga wa nyanyaso za aina mbalimbali.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Jumatano tarehe 29 Mei 2024 alasiri katika Jumba la Mtakatifu Calist, jijini Roma, kutakuwapo na uwakilishi wa Matokeo ya mwisho ya Uangalizi wa Wanawake duniani (WWO) wa Umoja wa Kimataifa wa  Mashirika ya Wanawake Wakatoliki (UMOFC), ambao ni uchunguzi pekee wa Kimataifa wa Kanisa Katoliki unaojikita na sauti ya wanawake. Hafla hiyo itaongozwa na Mónica Santamarina, rais wa  Umoja wa Kimataifa wa  Mashirika ya Wanawake Wakatoliki (UMOFC), na Uangalizi wa Wanawake duniani (WWO).

Utume wa Wanawake katika Kanisa la Kisinodi

Katika sehemu ya kwanza itaongozwa na mada: “Utume wa Wanawake katika Kanisa la Kisinodi: Changamoto na michango inayosikiliza Roho,” wakati huo, Ana Martianera, mkurugenzi wa mpango wa WWO, atawasilisha baadhi ya matokeo muhimu zaidi, ikiwa ni pamoja na hatua za kwanza za “Shule ya Kisinodi ya Umofc”, na kama vile itakavyokuwa ile sehemu nyingine ya hitimisho iliyoongozwa na mada ya: "Mazungumzo katika Roho,” ambapo kupitia  njia ya mtandao (Zoom), zaidi ya watu 670 walishiriki.

Kuondoa nyanyazo na ubaguzi dhidi ya wanawake Afrika

Katika sehemu ya Pili itajikita na: “Kuondoa nyanyaso na ubaguzi dhidi ya wanawake barani Afrika, Amerika Kusini, na visiwa vya Carrabien," kwa njia ya Mtandao na  itawakilishwa na matokeo ya mipango ambayo inasaidiwa na Mfuko wa Hilton, ili kuondoa ubaguzi na nyanyaso  kwa wanawake na kukosekana kwa elimu stahiki. Ni katika muktadha huo ambapo kabla ya Mkutano huo, Vatican news ilikutana na kuhojiana na mmoja wa washiriki wa Mkutano huo na kukambaribisha.

Ninaitwa Sr Maureen Ogundeph  wa Shirika la Wasakramenti wa Bergamo nchini Italia. Ninafanya kazi Nairobi, Kenya. Nimefika hapa Roma kama mhusika Mkuu wa Jumuiya ya Afrika kwa ajili ya Uangalizi wa Wanawake Duniani kuhusu nyanyaso za aina mbalimbali.

Sr Maureen unaweza kuwaeleza wasikilizaji ni shughuli gani hasa unayojikita nayo?

Mimi kama Mhusika mkuu wa Jumuiya ya Afrika kwa ajili ya Uangalizi wa wanawake duniani kuhusu nyanyaso, niko na kazi nyingi, hasa kuhusisha ofisi mbali mbali ziliozopo Afrika. Kwa hiyo wanawake wengi wanakumbana na matatizo mengi. Mimi kama Mhusika mkuu wa Jumuiya ya Afrika ninahitaji sana na mara nyingi kazi ninayofanya kusikiliza, kukaa nao pamoja, kuongea na viongozi wao, kusikia wanahitaji usaidizi gani. Baada ya kusikia hayo yote ambayo niliyopata kutoka katika nchi tofauti, tofauti za Afrika ninatuma taarifa hizo makao makuu. Baadaye ofisi yetu ambayo ipo hapa Roma, huwa inaangalia hayo matatizo yote. Tunazungumza kuhusu haya yote, alafu tunaona jinsi gani ya kuhusika kuwasaidia hawa wanawake, kwa kuwasikiliza, kwa kuona kama tunaweza kupata jinsi ya kuwasaidia kwa namna ya maisha yao, kuelimisha na njia fotafuti tofauti. Pia kama mhusika Mkuu wa Jumuiya hii ya Afrika, nia kubwa ambayo inaa kufanya ni kujaribu kuwaleta wanawake wakatoliki pamoja na watawa wa kike ili waweze kufanya kazi pamoja.

Umoja wa Wanawake Duniani umeanza muda mrefu na sasa unafanya kazi kwa pamoja na watawa, hii ilianzaje?

Kwa miaka mingi watawa wamekuwa wakifanya kazi peke yao, na vile vile  wanawake wa kikatoliki wakifanya kivyao, lakini ni wakati wa kisinodi kama tulivyoshauriwa na Baba Mtakatifu, kufanya pamoja, kushughulika pamoja, kuamua pamoja ili  kupiga vita janga baya la nyanyaso au utumwa mamboleo. Katika hili kwa kuungana pamoja ni ukweli kwamba unazaa matunda. Kwa sababu watawa wa kike na kiume na wanawake walei wakifanya pamoja na kuwaunganisha wazee inasaidia kupata suluhisho la mizizi hii ya nyanyaso ambazo lazima zing’olewe. Kwa kuhitimisha, tumeona hili linaweza kusaidia wale ambao tunakutana nao kuwasikiliza na wao pia kuhisi kusikilizwa, kupendwa na wanaweza kujifungua kutoa matatizo yao yaliyomo moyoni mwao bila kuogopa kwa maana hakuna anyewahukumu, wanapokelewa jinsi walivyo na huo ndiyo utume mkubwa tulio nao katika ofisi yetu tuliyo nayo Kenya, Afrika na katika ulimwengu.

Kwa hiyo huko hapa  katika mkutano ambao unaanza lini?

Tunaanza mkutano tarehe 29 Mwezi huu wa Mei na mkutano huu tutapeana ripoti kuhusu hayo yote ambayo tunafanya kusaidia wanawake huko Afrika na katika Ulimwengu mzima. Pia tutaweza kuona namna ambayo tunaweza kugusa maisha yao. Ni namna gai tunaweza kuendelea na kuwasaidia kuondokana na kiwewe, wasiwasi, matatizo ambayo wamekutana nayo.

Ushuhuda wa Sr Maureen Gundeph wa UMOFC na WWO
28 May 2024, 12:31