Enea alipombeba baba yake Anchises juu ya mabega yake!
Na Alessandro Gisotti
“Hakuna historia iliyo ndogo, hakuna. Kila historia ni nzuri na inafaa, na hata ikiwa ni mbaya, ikiwa heshima itafichwa, inaweza kuibuka kila wakati.” Ilikuwa mnamo tarehe 5 Februari 2019 wakati Papa Francisko alipotamka maneno haya mwanzoni mwa mkutano na waandishi wa habari katika ndege iliyokuwa inarudi kutoka Abu Dhabi baada ya kutiwa saini ya kihistoria ya Hati ya Udugu wa Kibinadamu. Katika miaka ya hivi karibuni Papa amehimiza mara nyingi, hasa sisi wafanyakazi wa mawasiliano, kutoa nafasi kwa historia ndogo. Historia za watu, za jamii. Na anatuomba hili, hasa, tunapokabiliwa na hali ya kisasa ya uhamiaji.Hivi ndivyo idadi huwa sura, takwimu, uzoefu na hoja za kisiasa kuhusu dharura (halisi au zinazodhaniwa) kutoa nafasi kwa juhudi za kuwaokoa wengine, ambao hawawezi kuwa wageni kwetu kwa sababu wao ni wanawake au wanaume kama sisi. Hivi karibuni, historia, imeibuka ambayo inaunganishwa vyema na wito huu kutoka kwa Papa Francisko. Historia ambayo hatupati katika vichwa vya habari lakini ambayo, kiukweli, siyo ndogo kwa sababu inashuhudia heshima kubwa.
Historia ya mwanamke wa miaka 78 kutoka Afghanstan hadi Ujerumani
Ni historia ya Maryam, mwanamke mwenye umri wa miaka 78 ambaye alikimbia Afghanistan ya Wataliban (ambaye anakumbuka nchi hii tena baada ya kuondoka kwa vikosi vya kijeshi vya Magharibi) na baada ya safari ya ajabu alifika kwenye pwani ya Calabria, huko Roccella Jonica, Italia , pamoja na wahamiaji wengine 83 walioondoka kwa mashua kutoka pwani ya Uturuki. Ni nini kilimfukuza, tulimuuliza mwanamke mzee kama huyo kusafiri maelfu ya kilomita katika njia za muda mrefu, kati ya hatari elfu, na kulipa bei ya juu kwa vifungu vilivyompeleka kutoka moyo wa Asia hadi mipaka ya Ulaya? Motisha ni familia yake. Mnamo 2021, binti wa Maryam pamoja na mumewe walikimbia kutoka Afghanistan na kufika Ujerumani, na kumwacha mtoto wake wa kiume chini ya ulinzi wa bibi yake, ambaye sasa ameamua kumrudisha kwa wazazi wake.
Papa: Ndoto za wazee huongoza vijana
“Baada ya kuwasili Roccella Jonica - (linaandika Gazeti la Kusini), Maryam alionesha shukrani kwa waokoaji, lakini azimio lake la kufika Ujerumani lilikuwa lisiloweza kutetereka. Licha ya majaribio ya kumshawishi kuomba hifadhi ya kisiasa nchini Italia, alikataa na, baada ya kupata amri ya kukataliwa, aliondoka na mpwa wake kuelekea marejeo yake ya mwisho.” Kwa hiyo hakuna kilichozuia azimio la Maryam kuelekea kaskazini, kufuatia sehemu ya mwisho ya njia hii ya kuunganisha tena familia iliyogawanyika. Hii inaonekana kama vile tuko mbele ya tukio la mkesha wa Enea akikimbia kutoka kwa Troy akiwa amembeba baba yake mzee Anchises mabegani mwake. Hapa, hata hivyo, ni Anchises, au Maryam mzee, ambaye alimbeba Enea, mpwa wake mchanga, mabegani mwake. Na pia katika historia hii, vile Papa Francisko amekuwa akitukumbusha mara kadhaa kuwa "ni ndoto za wazee ambazo huwaongoza vijana na kuwasukuma mbele kufikia lengo."