Askofu mkuu Georg Gänswein Balozi wa Vatican Lithuania, Estonia Na Lativia
Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko tarehe 24 Juni 2024 amemtea Askofu mkuu Georg Gänswein, Kiongozi mkuu mstaafu wa nyumba ya Kipapa kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Lithuania, Estonia na Lativia. Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu Georg Gänswein alizaliwa tarehe 30 Julai 1956 huko Walshut, nchini Ujerumani. Tarehe 31 Mei 1984 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre kwa ajili ya Jimbo Katoliki la Freiburg im Breisgau lililoko nchini Ujerumani.
Baba Mtakatifu Benedikto XVI tarehe 7 Desemba 2012 akamteuwa kuwa Kiongozi mkuu wa Nyumba ya Kipapa na hivyo kumpandisha hadhi na kuwa ni Askofu mkuu. Akawekwa wakfu tarehe 6 Januari 2013. Amekua ni Kiongozi mkuu wa nyumba ya Kipapa kuanzia tarehe 7 Desemba 2012 hadi tarehe 28 Februari 2023. Tarehe 24 Juni 2024, Baba Mtakatifu Francisko akamteuwa kuwa ni Balozi mpya wa Vatican nchini Lithuania, Estonia na Lativia.