Askofu mkuu Janusz Stanisław Urbańczyk Balozi wa Vatican nchini Zimbabwe, hivi karibuni amewasilisha hati za utambulisho kwa viongozi wa Serikali na Kanisa nchini Zimbabwe. Askofu mkuu Janusz Stanisław Urbańczyk Balozi wa Vatican nchini Zimbabwe, hivi karibuni amewasilisha hati za utambulisho kwa viongozi wa Serikali na Kanisa nchini Zimbabwe. 

Askofu Mkuu Janusz Stanisław Urbańczyk Awasilisha Hati za Utambulisho Zimbabwe

Askofu mkuu Janusz S. Urbańczyk tarehe 6 Aprili 2024 amewekwa wakfu kuwa Askofu mkuu katika Ibada iliyoongozwa na Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican akisaidiana na Askofu Jacek Jezierski wa Jimbo Katoliki la Elblag lililoko nchini Poland. Hivi karibuni Askofu mkuu Janusz Stanisław Urbańczyk amewasilisha hati zake za utambulisho kwa Rais Emmerson Dambudzo Mnangagwa wa Zimbambwe, hafla iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko tarehe 25 Januari 2024 alimteua Monsinyo Janusz Stanisław Urbańczyk kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Zimbabwe na kumpandisha hadhi na hivyo kuwa ni Askofu mkuu. Kabla ya uteuzi huu, Askofu mkuu Janusz Stanisław Urbańczyk alikuwa ni Mwakilishi wa Kudumu kwenye Ofisi za Umoja wa Mataifa zilizoko mjini Vienna, Austria. Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu Janusz Stanisław Urbańczyk alizaliwa tarehe 19 Mei 1967 huko Kraszewo, Poland. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 13 Juni 1992 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre kwa ajili ya Jimbo Katoliki la Elbag. Kimasomo alibahatika kupata Shahada ya Uzamivu katika Sheria za Kanisa. Tarehe 1 Julai 1997 alianza kutoa huduma yake katika diplomasia ya Kanisa na hivyo kutumwa nchini Bolvia, Slovakia, New Zealand, Kenya na Makao makuu ya Umoja wa Mataifa, Jijini New York, nchini Marekani. Tarehe 12 Januari 2015 akateuliwa na Baba Mtakatifu Francisko kuwa ni Mwakilishi wa kudumu wa Vatican kwenye Tume ya Nguvu za Atomu ya Umoja wa Mataifa, AIEA; Shirikisho la Ushirikiano wa Kimataifa, Usalama na Maendeleo Barani Ulaya, OSCE, Shirika la Mkataba wa Kupiga Marufuku Majaribio ya silaha za Nyuklia, CTBTO, Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Viwanda, UNIDO na hatimaye, Mwakilishi wa Kudumu kwenye Ofisi za Umoja wa Mataifa zilizoko mjini Vienna, Austria.

Askofu mkuu Janusz amewasilisha hati za utambulisho nchini Zimbabwe
Askofu mkuu Janusz amewasilisha hati za utambulisho nchini Zimbabwe

Askofu mkuu Janusz Stanisław Urbańczyk tarehe 6 Aprili 2024 amewekwa wakfu kuwa Askofu mkuu katika Ibada iliyoongozwa na Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican akisaidiana na Askofu Jacek Jezierski wa Jimbo Katoliki la Elblag lililoko Kaskazini Mashariki mwa Poland. Hivi karibuni Askofu mkuu Janusz Stanisław Urbańczyk amewasilisha hati zake za utambulisho kwa Rais Emmerson Dambudzo Mnangagwa wa Zimbambwe, hafla iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali na Kanisa. Katika mazungumzo yao, viongozi hawa wawili wamepongeza uhusiano mwema wa kidiplomasia uliopo kati ya Zimbabwe na Vatican sanjari na mchango wa Kanisa Katoliki katika ustawi, maendeleo na mafao ya watu wa Mungu nchini Zimbabwe; hususan kwenye sekta ya elimu, afya na ustawi wa jamii. Askofu mkuu Janusz Stanisław Urbańczyk, katika siku za hivi karibuni alipata pia nafasi ya kuzungumza na Baraza la Maaskofu Katoliki Zimbabwe sanjari na kuwasilisha hati zake za utambulisho kwa viongozi wa Kanisa Katoliki nchini Zimbabwe.

Hati Zimbabwe

 

20 June 2024, 14:05