Baraza la kawaida la Makardinali watakutana kwa kura ya watakatifu wapya 15
Vatican News
Kwa mujibu wa Mhadhimishaji wa Liturujia za kipapa, Jumatano tarehe 19 Juni 2024, amebainisha kuwa Jumatatu tarehe Mosi Julai 2024 saa 3.00 kamili asubuhi katika Ukumbi wa Mikutano katika Jumba la Kitume mjini Vatican, Baba Mtakatifu Francisko ataongoza liturujia ya Masifu na Baraza la Kawaida kwa umama kwa ajili ya kupiga kura kuhusu watakaotangazwa kuwa watakatifu kama wafuatao: mwenyeheri Manuel Ruiz López na Wanzake saba wa Shirika la Ndugu Wadogo na Francesco, Mooti na Raffaele Massabki, Waamini Walei wafiadini.
Giuseppe Allamano, Padre na mwanzilishi wa Mashirika ya Kimisionari ya Watawa wa kike na kiume wa Consolata; Marie-Léonie Paradis (zamani aliitwa Virginie Alodie), Mwanzilishi wa Shirika la Watawa Wadogo wa Familia Takatifu, Elena Guerra, Mwanzilishi wa Shirika la Wa Oblata wa Roho Mtakatifu(waitwao Watawa wa Mtakatifu Zita);na hatimaye Carlo Acutis, mwamini Mlei.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa mhadhimishaji Mkuu wa liturujia za kipapa alibainisha kuwa Makardinali wakazi au walioko Roma katika siku hizi za Baraza la Makardinali wanaoombwa kukutana saa 2.30 katika Ukumbi wa Mikutano kwenye Jumba ya Kitume, tayari wamevaa mavazi husika.