Tafuta

2024.05.31 Askofu Mkuu  Paul Richard Gallagher yuko Kroatia. 2024.05.31 Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher yuko Kroatia. 

Gallagher:katika ulimwengu uliofunikwa na giza,tuwe wapatanishi!

Ziara ya Katibu wa Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa huko Kroatia iliyoanza tarehe 30 Mei inaendelea.31 Mei aliadhimisha Misa kwa ajili ya sikukuu ya Mama Yetu wa Lango la Jiwe,mlinzi mtakatifu wa Zagreb.Alitoa mwaliko wa kujifunza kutokana na mkutano kati ya Maria na Elizabeth,kitovu cha Liturujia,uwezo wa kuona uwepo wa Mungu hata leo:“Kila janga mshikamano huenea na hatutazami mabomu tu yanayoanguka.”

Na Adriana Masotti na Angella Rwezaula – Vatican

Ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku tatu nchini Kroatia, Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu wa Vatican wa Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa, aliongoza Ibada ya Ekaristi Takatifu  Jioni ya tarehe  31 Mei 2024  huko Zagreb kwa ajili ya kuadhimisha Sikukuu ya Bikira Maria,  lango la Jiwe, ambaye ni Mtakatifu mlinzi wa mji mkuu wa Kroatia. Katika mahubiri ya ukumbusho huo alitumia fursa ya kuelezea uweza wa  kuifahamu kazi ya Mungu hata katikati ya magumu mengi na maangamizo ya leo hii  kama vile Bikira Maria na binamu yake Elizabeti walivyoweza kufanya, na ambao waliamini na kutumaini kabla ya kuona utimilifu wa ahadi za Mungu.

Picha ya mama chanzo cha matumaini

Askofu Mkuu Gallagher alikumbuka kwamba Sura ya Mlango wa Mawe iliyotoka katika magofu ya mlango huo, mlango wa mashariki wa mji wa kale, kufuatia moto, ilikuwa chanzo cha mshangao na kuchanganyikiwa kwa wakazi wake walioteseka na kuchanganyikiwa. “Leo duniani hakuna uhaba wa matukio ya uharibifu wa kutisha unaosababishwa na matukio ya asili, lakini pia na ujinga huo wa kibinadamu ambao Papa Francisko  ameelezea kwa muda mrefu kama 'vita vya tatu vya dunia' ambavyo vinageuka kuwa mgogoro wa kweli wa kimataifa. Hii ndiyo sababu ni muhimu kutazama picha hiyo tena.”

Maisha, zawadi kutoka kwa Mungu

Katikati ya liturujia hiyo ilifafanua juu ya  mkutano kati ya Maria  na Elizabeth, ambao wote ni mama wajawazito bila kutarajia. Akina mama ambao walivurugwa mipango yao, lakini ambayo walikaribisha kwa furaha." Alisema Askofu Mkuu Gallagher. Hata hivyo mawazo yake yaliwatazama akina mama wa siku hizi kwamba “Mama  wa Mlango wa Mawe awasindikize  wale wanawake wote wanaopokea chembechembe ya maisha mapya tumboni mwao, hata inapofika bila kutarajia na waweze kujua jinsi ya kuona kama zawadi kutoka kwa Mungu. Hii haifanyiki kila wakati katika jamii zetu, lakini kwa wamini, maisha lazima yaendelezwe na kulindwa.” Alisisitiza Katibu wa Vatican wa Mahusiano na Mataifa.

Hebu tuinuke haraka, kama Maria alivyofanya

Injili ilisema kuhusu Maria kwamba “aliinuka na kwenda haraka” kumtembelea binamu yake Elisabeti. Kwa hivyo Maria ni mfano wa Kanisa linalotoka linalotamaniwa na Papa. Na awe kielelezo kwetu pia. Bwana atupe nguvu za kuamka, kwenda, kukutana na wale wanaoteseka, wale wanaoteseka matokeo ya hatima mbaya au uovu wa kibinadamu. Hebu inuka, haraka. Hatuwezi kubaki bila kazi. Kuna hitaji la dharura la kuwafariji walioteseka, kuwatia moyo waliokata tamaa, kuwa wapatanishi.”

Mpito kutoka kifo hadi uzima

Elisabeti na mume wake Zakaria walikuwa wamengoja kwa miaka mingi kwa ajili ya zawadi ya mwana: “pengine walikuwa wameweka mioyo yao kwa amani,  wakati Bwana aliposikiliza sala yao, akitambua tumaini lao. Katika Ndiyo ya Maria kwa mapenzi ya Mungu na katika mabadiliko ya kujiuzulu kuwa furaha kwa Elizabeth, ni mantiki ya Pasaka. “Tunapojua jinsi ya kuacha mipango yetu ya kujisalimisha kwa mapenzi ya Muumba, kwa furaha au huzuni, ni fumbo la Pasaka linalofanya kazi ndani yetu na kujidhihirisha kwa nguvu zake zote,” alisisitiza Askofu mkuu.

Sio mabomu tu ulimwenguni, lakini pia mshikamano

Maria na Elizabeti walimsifu Bwana si wakati kila kitu kilitokea kulingana na matakwa yao, lakini kwa uhakika kwamba Mungu atatimiza ahadi zake. Kwa hiyo ni mwaliko kwetu kuona kazi ya Mungu tayari iko ulimwenguni, ingawa katika kiinitete.” Alisisitiza. Aidha Askofu Mkuu Gallagher kisha alitoa mwaliko wa kufumbua macho yao  kwa mfano, kwa mshikamano unaotokea kila wakati kukiwa na janga au ukatili wa kibinadamu. Hatuangalii mabomu tu  yanayoanguka na uharibifu unaoleta,” alisema Askofu Mkuu. Bwana, kama Maria wa Mlango wa Mawe anavyohifadhiwa, huwaokoa watu wema, kundi dogo, ambalo wakati mwingine huwa kubwa, kama jeshi la wale wanaohatarisha maisha yao ili kupunguza maumivu ya waathiriwa au kuzuia majanga mapya.”                                                                 

Mashahidi wa ufufuko, wajenzi wa amani

Tunahitaji mtazamo wa wahusika wakuu wawili wa liturujia ya leo hii, alisema askofu mkuu, kuona kazi ya Mungu tayari inaendelea, katikati ya 'uovu wa ulimwengu. Katika Maria wa Mlango wa Mawe, ulioitwa huko Kroatia kama Mwanzo wa ulimwengu bora, kama Mtakatifu Yohane Paulo  II alivyokumbuka alipotembelea nchi hiyo miaka 30 iliyopita, Askofu Mkuu Gallagher aliomba zawadi ya uvumilivu kwa kila mtu. “Kama vile alivyojidhihirisha kama ishara ya tumaini wakati wa msiba na atufanye sisi kuwa mashahidi wa ufufuko, licha ya kila kitu, tumsifu Mungu kwa maisha yetu kwa kuwa hata sasa, katika ulimwengu unaozungukwa na mengi  ya giza, tunakuwa mianga ya nuru na wajenzi wa amani.” Alihitimisha.

Askofu Mkuu Gallagher
01 June 2024, 11:43