Tafuta

2024.06.18 Papa ameinua Jimbo la Ndola kuwa jimbo Kuu na kumteua kuwa Askofu Mkuu Benjamin Phiri aliyekuwa wa jimbo hilo hilo. 2024.06.18 Papa ameinua Jimbo la Ndola kuwa jimbo Kuu na kumteua kuwa Askofu Mkuu Benjamin Phiri aliyekuwa wa jimbo hilo hilo. 

Jimbo la Ndola,Zambia limeinuliwa kuwa Jimbo Kuu

Baba Mtakatifu ameliinua Jimbo la Kikanisa la Ndola (Zambia), lenye majimbo ya Kabwe na Solwezi kuwa Jumbo Kuu na amemteua Askofu Benjamin Phiri,ambaye hadi uteuzi huo alikuwa ni Askofu wa Jimbo la Ndola,kuwa Askofu Mkuu wa Jimbo kuu hilo jipya.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Jumanne tarehe 18 Juni 2024 ameinua hadhi ya  Jimbo la Kikanisa la Ndola (Zambia), lenye majimbo ya Kabwe na Solwezi, kuwa Jimbo Kuu na akamteua Askofu  Benjamin Phiri, aliyekuwa  ni Askofu wa Jimbo la Ndola, kuwa Askofu Mkuu wa Jimbo hilo hilo kuu.

Takwimu ya Jimbo  Kuu Jipya la Kikanisa la Ndola liko katikati mwa Zambia. Linaenea zaidi ya kilomita za mraba 32,000. Kuna Wakatoliki 1,920,580, kati ya wakazi 3,223,400 (59.6%), wanaohudumiwa  katika parokia 84. Katika jimbo hilo kuu jipya kwa sasa litakuwa na  mapadre 187 (106 wa jimbo na 81 wa mashirika). Watawa wa kiume  151 na watawa wa kike 340 pia wanashiriki katika uchungaji. Kuna waseminari katika seminari kuu 143 pia Jimbo kuu linatumia huduma ya makatekista wengi. Jimbo jipya la Kikanisa la Ndola litakuwa na wasaidizi wa jimbo la Kabwe na Solwezi.

Takwimu kamili:

Majimbo

Ndola

Kabwe

Solwezi

Ukubwa wake (Km²)

32.000

63.574

125.826

Wakazi

3.223.400

1.203.610

1.134.160

wakatoliki

1.920.580

191.060

107.035

Parokia

84

32

40

Mapadre wa Kijimbo

106

32

30

Mapadre wa Kitawa

81

80

-

Watawa kime

151

112

-

Watawa wa Kike

340

96

76

Waseminari

143

31

39

Wabatizwa

5.446

4.200

2.084

18 June 2024, 16:13