Kard.Parolin:kama kungekuwa na ufunguzi Papa pia angeenda China!
Na Salvatore Cernuzio na Angella Rwezaula – Vatican.
Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican alisema “Wakati kwa sasa unaonekana kuwa mapema lakini ikiwa kungekuwa na uwazi kwa upande wa Wachina, Papa pia angeenda mara moja hadi China, nchi ambayo ameonesha shukrani na heshima kubwa kwa watu wake, historia yake, utamaduni.” Alisisitiza tena hamu ya Papa Francisko ya kutaka siku moja kusafiri hadi nchi kubwa na maarufu ya Asia. Ni katika mazungumzo ya alasiri, Alhamisi tarehe 20 Juni 2024 katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Urbaniana katika uwasilishaji wa kazi inayohusu Kardinali Celso Costantini na China - Mjenzi wa daraja kati ya Mashariki na Magharibi, iliyohaririwa na mwanahistoria Monsinyo Bruno Fabio Pighin na kuchapishwa na Na nyumba ya Marcianum.
Kongamano la Urbaniana kwa mara ya pili
Kwa mara nyingine tena, mwezi mmoja baada ya Kongamano la Urbaniana kuhusu miaka mia moja la Concilium Sinense, ambalo Kardinali Costantini mwenyewe alikuwa mhamasishaji, mkuzaji na mwandaaji, Kardinali Parolin alijikuta akiibua sura ya mjumbe wa kwanza wa kitume nchini China ambaye aliweka misingi ya mazungumzo ambayo moja ya matunda, baada ya miongo kadhaa, yaliweza kuzingatiwa kutiwa saini kwa Mkataba na Vatican juu ya uteuzi wa maaskofu, uliotiwa saini kwa mara ya kwanza mnamo 2018 na kisha kupyaishwa mara mbili mnamo 2020 na 2022. Ni Makubaliano hayo ambayo Kardinali Parolin alikumbuka katika mazungumzo mafupi na waandishi wa habari kando ya mada hiyo, ambapo akiulizwa maswali alisema: “Tunazungumza na China kama tumekuwa kwa muda, tunajaribu kutafuta taratibu bora pia za utekelezaji wa Mkataba huo uliyotiwa saini wakati huo na ambao utapyaishwa mwishoni mwa mwaka huu,” alijibu maswali ya wanahabari.
Heshima ya Papa kwa watu wa China
Maneno ya Papa yalirejea pia mwishoni mwa Katekesi wakati akitoa salamu kwa chama “Marafiki wa Kardinali Celso Costantini”, alichukua fursa hiyo kutuma salamu “kwa watu wapendwa wa China. Siku zote tunawaombea watu hawa waungwana, jasiri sana, ambao wana utamaduni mzuri kama huu,” Alisema Baba Mtakatifu Francisko. Kwa maoni ya Kardinali Parolin, alisema: “Papa kiukweli ana shukrani kubwa na hakuna uhaba wa fursa za kuelezea kwa watu wa China na taifa la China. Labda kwa sababu yeye ni Mjesuit, kwa hiyo ana urithi wote wa zamani. Hakika zote ni hatua zinazotusaidia kuelewana zaidi na zaidi, ili kukaribiana zaidi na zaidi, tunatumaini kwamba safari hii inaweza kusababisha hitimisho chanya.”
Safari inayowezekana ya Papa kwenda China
Lakini pia labda kwa safari inayowezekana safari ya kwanza na ya Papa kwenda China. Katika hatua hii Kardinali alijibu kwa tahadhari: “Hakika Papa yuko tayari kwenda China, kwa hakika anatamani kwenda China. Haionekani kwangu kuwa hadi sasa masharti yapo kwa hamu hii ya Papa kutimia. china iko karibu na mioyo yetu.” Kisha Parolin alisisitiza upendo wake kwa China katika hotuba yake katika Ukumbi Mkuu wa Urbaniana alisema: “Tunaipenda na kuienzi China, watu wake, utamaduni wake, mila zake, juhudi inayofanya hivi sasa. China iko karibu sana na mioyo yetu, iko karibu na mioyo ya Papa Francisko na washirika wake.”
Mbinu ya Costantini leo hii ni mwelekeo unaofuatwa
Akiendelea Kardinali Parolin alifuatilia picha ya Costantini, akikumbuka historia (kama vile wakati mjumbe wa kitume alipokwenda kwa Pius XII mnamo 1946 kuomba kuingiza jina la askofu wa Kichina kwenye Baraza la Makardinali kwa makardinali wapya 32, ambapo jina lake lilijumuishwa) na kusifu juhudi, kazi na sadaka za Kardinali katika kueneza mwanga wa Injili nchini China na zaidi ya yote, kuhamasisha Kanisa lililokuzwa.” Costantini ndiye aliyesisitiza kuundwa kwa Concilium Sinense ya Shanghai mwaka 1924, ambayo ilikuwa ni msukumo wa kinabii kwa Mtaguso mkuu wa Pili wa Vatican na kuweka misingi ya Kanisa la China ambalo mwaka 1963 lilikuwa na maaskofu 23, licha ya upinzani wa taasisi nyingi za wamisionari nchini China. “Maaskofu hawa walifuatilia mwongozi wa urithi wa kitume kwa maaskofu wa sasa,” Parolin alisema.
Kwa njia hiyo: “Mbinu ya Costantini katika mahusiano kati ya Vatican na Nchi kubwa ya Asia leo hii ni mwelekeo unaofuatwa pia na Papa Francissko, alisema katibu wa Vatican. Mwongozi ambao ulipata matokeo katika Barua ya Papa Benedikto XVI ya 2007 kwa Wakatoliki wa China na kuhitimishwa na Makubaliano ya muda yaliyotiwa saini huko Beijing mnamo 2018 kwa uteuzi wa maaskofu, ambapo sifa za muda inaonesha kuwa ni hatua ya kuanzia. Imethibitishwa mara mbili katika miaka ya hivi karibuni, imepata utekelezaji muhimu katika kesi madhubuti,” alisema Kardinali Parolin. Matukio chanya yaliyorekodiwa kufikia sasa yanatupatia matumaini kwamba makubwa zaidi yatafuata. Kufuatia Makubaliano hayo maaskofu wote katika nchi ya China, wako katika ushirika kamili na Kanisa la Petro”, alisisitiza Kardinali aidha alieleza matumaini kwamba “mazungumzo na mchakato ulioanzishwa na Wakatoliki wa China utaendelea kukuza maelewano zaidi chini ya uongozi wa wachungaji wao, kwa ushirika kamili na Papa ambaye ametoa uthibitisho mwingi wa upendo wake kwa watu hao wakuu.”