Kard.Parolin:Kanisa la Lebanon litunze uhai wa kuishi pamoja
Na Adriana Masotti na Angella Rwezaula – Vatican.
Kardinali Pietro Parolin, akiwa ziarani huko Lebanon kuanzia tarehe 23 hadi Alhamisi 27 Juni 2024, ambayo ilikuwa zaidi ya kidiplomasia na vile vile ya kibinadamu aliadhimisha hata Misa huko Beirut, katika Kanisa la Mtakatifu Yosefu pamoja na washiriki wa Jumuiya ya Shirika la Kijeshi la Malta, ambalo mwaka huu linaadhimisha miaka 40 tangu kuanzishwa kwake. Katika mahubiri yake alikumbusha maneno ya Mbatizaji katika makutano kwenye ukingo wa Yordani: “Yeyote aliye na nguo mbili, mgawie asiye na kitu; na aliye na chakula, na afanye vivyo hivyo”, ili kusisitiza kwamba angalieni ambaye hana chochote ndiye anayeonyesha'kazi ya Shirika la Kijeshi nchini Lebanon, lililoathiriwa na mgogoro mkubwa wa kiuchumi na kisiasa.
Shirika la kijeshi la Malta linatokana na kundi la Wahudumu wa Hospitali ya Mtakatifu Yohane wa Yerusalemu, ambao lengo lao lilikuwa ni kuwasaidia mahujaji katika Nchi Takatifu kwa kutoa wito wa kushuhudia Injili ya Kristo ambapo hata leo kama mtu mmoja mmoja na kama Kanisa la Lebanon, pia katika maisha ya umma. Na kwa mantiki hiyo Katibu wa Vatican anayo matumaini ya kufanyika kwa uchaguzi wa haraka wa rais ili kuleta utulivu nchini. Ziara hii inafafanuliwa kama ziara ya urafiki na uaminifu, na ni wazi pia inajumuisha programu ya kidiplomasia, ikizingatiwa kuwa Vatican inaitazama kwa makini Lebanon ambayo imekuwa katika mgogoro wa kisiasa kwa miaka mingi na bila rais tangu 2022, kwa hakika, angetaka kusafiri kwenda nchini humo mwaka wa 2022, jambo ambalo halikufanyika, na mwaka 2020, baada ya mlipuko katika bandari ya Beirut, Papa alimtuma Kadinali Parolin mwenyewe kama mjumbe wake maalum huko Beirut na wakati huo huo Papa aliongoza Siku ya Maombi kwa ajili ya Kuombea ncgi ya Lebanon.
Elizabeth furaha na shukrani
Kwa maana hiyo akitoa mahubiri yake kuhusu Injili ya Luka ya kuzaliwa kwa Yohane Mbatizaji katika sehemu ya Injili ya siku hiyo, Katibu wa Vatican alifafanua wahusika watatu wakuu: Elizabeti, Zekaria na Yohane. Kwa njia hiyo alisisitiza juu ya furaha ya mama na shukrani kwa Bwana kwa utimilifu wa ahadi yake. “Lazima tuwe mashahidi wa furaha hii na shukrani kwa sababu sisi pia tumetambua wokovu unaotoka kwa Kristo. Katika ulimwengu unaozidi kuandamwa na dhambi, wivu, migawanyiko, migogoro na ukosefu wa msamaha, furaha ya Kikristo, ambayo ni zaidi ya furaha ya kupita, inakuwa muhimu zaidi.”
Zakaria anatambua ukuu wa Mungu
Baadaye alitazama Zakaria, ambaye mwanzoni hakuamini habari kwamba mke wake angezaa mtoto wa kiume, lakini basi aliweza kutambua ukuu wa Mungu. Kardinali Parolin alisema kuwa: “Inatia moyo kujua kwamba ikiwa hatuko tayari kuitikia mapenzi ya Bwana, yeye ambaye anatufahamu kwa karibu anajua jinsi ya kutumia njia ili kutupa furaha yake.”
Yohane: mwaliko wa uongofu wa maisha
Ka upande wa Yohane, Mtangulizi wa Yesu ambaye angeweza kufafanuliwa kama mtume wa kwanza wa Yesu na wakati huo huo wa mwisho kwa manabii. Sauti yake yenye nguvu ilikuwa imetayarisha ujio wa Bwana kwa kuwahimiza watu wa Israeli kuongoka. Kwake, Kardinali Parolin alibainisha kuwa, haina maana kuwa mwana wa Ibrahimu ikiwa hutendi haki. Kwa wale waliomuuliza afanye nini ili kujiokoa, Yohana alijibu: Yeyote aliye na nguo mbili, mgawie asiye na kitu; na aliye na chakula na afanye vivyo hivyo. Uangalifu kwa maskini, wagonjwa, mateso ni nini haswa kinachoonesha uwepo wa Shirika la Kijeshi la Malta huko Lebanon, umakini ambao hauwezi kutenganishwa na tuitio fidei, ambayo ni, ulinzi wa imani, kama kauli mbiu yenyewe inakumbuka shirika : Tuitio fidei et Obsequium Paeperum.
Mgogoro mkubwa unaoikabili Lebanon
Kile ambacho Shirika la Kijeshi la Malta hutenda si huduma kwa walio dhaifu zaidi, kitu cha kibinadamu kwa sababu ni hatua ya kidini iliyojengwa juu ya imani katika Kristo ambayo inapendelea hata kidogo na, kwa kuangalia matukio ya sasa, inaendelea:Hali mbaya ya kiuchumi ya Lebanon inakuongoza kuwa mkarimu zaidi katika kukidhi mahitaji ya wahitaji zaidi, katika kujaribu kupunguza mzigo wa watu wengi, kwa matumaini ya mustakabali bora, wa haki na usawa.
Ushuhuda wa kuishi pamoja
Katika ibada,aliendelea Parolin, unaalikwa kuonesha furaha, imani na matumaini waliyopata Elizabeti na Zekaria, kuwa kama Yohana mashahidi wa Kristo na leo tuna hitaji kubwa la mashahidi wa kuaminika kwa kibinafsi, familia na kama ngazi ya Kanisa: Kwa mjibu wa Kardinali Parolin alikumbusha kuwa: Kanisa huko Lebanon lazima pia kushuhudia, kulingana na utume wake wa juu wa kuweka hai na ufanisi ujumbe wa 'kuishi pamoja', ambayo ni sifa ya Nchi ya Mierezi, pia wawe mashahidi katika ngazi ya kitaifa, kikanda na kimataifa, bila woga wa kuleta Injili ya Kristo katika maisha ya umma.
Wito wa uchaguzi wa haraka wa rais
Kuhusiana na hili, Kardinali Parolin alirejea utupu mkubwa katika eneo la kisiasa la nchi hiyo, ambalo linakosa sauti ya Rais wa Lebanon. Kutokuwepo huku kunaleta uzito mkubwa katika wakati mbaya kama huo kwa Mashariki ya Kati. Aliendelea kusema kuwa: “Kwa niaba ya Baba Mtakatifu, kwa imani na matumaini, ninarudia tena ombi hili kwa wale wote wenye wajibu, ili uchaguzi wa rais ufanyike haraka na nchi igundue tena utulivu wa kitaasisi unaohitajika kukabiliana kwa umakini na changamoto zilizopo.”
Wito wa Lebanon kuwa mwanga kwa eneo hilo
Kardinali Parolin alihitimisha mahubiri yake kwa kunukuu yale aliyoyaandika Mtakatifu Yohane Paulo wa Pili katika himizo la kitume la baada ya sinodi, Tumaini jipya kwa Lebanon ambapo alisema kwamba, kujitolea kwa kila mmoja “kwa ajili ya upendo wa Bwana na wa Kanisa lake”. ingeleta matunda kwa jamii nzima ya Lebanon. Baadaye Lebanoni, mlima wa furaha ambapo Nuru ya Mataifa, Mfalme wa Amani, ilipotokea, itaweza kusitawi tena kikamilifu; itatambua wito wake wa kuwa nuru kwa watu wa eneo hilo na ishara ya amani hiyo inatoka kwa Mungu. Matumaini ya Parolin ni kwamba “Injili ya wokovu iwe chemchemi ya nguvu, furaha na tumaini kwa wanaume na wanawake wote wa dunia hii.”