Tafuta

Kutoka nje kualika Kutoka nje kualika  

Kard.Tagle kwa PMS:Tafuteni njia mpya za kukaribisha wote katika karamu ya Bwana

Kardinali Tagle kwa Mashirikia ya Kipapa ya Kimisionari wakati wa Mkutano wao Mkuu ulioanza tarehe 24 hadi 31 Mei 2024,alitoa mwaliko Mei 27 kwa viongozi wakuu wa PMS kitaifa kutafuta njia mpya za kutoka nje na kuwaalika watu wote ili waje kwenye karamu ya Bwana.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Kardinali Luis Antonio Gokim Tagle, Msimamizi Mkuu wa Baraza la Kipapa la  Uinjilishaji, hivi karibuni  tarehe 27 Mei 2024 kwenye Mkutano Mkuu wa Mashirika ya Kimissionari ya Kipapa PMS uliozinduliwa mnamo tarehe 24 Mei na kuhitimishwa tarehe 31 Mei 2024 huko kwenye Nyumba ya Udugu, Sacrofano, nje kidogo ya mji wa Roma. Katika  hotuba yake ilitiwa msukumo na fumbo la kiinjili la karamu ya harusi ya mwana wa mfalme ambayo tayari ilirejewa katika Ujumbe wa Papa Francisko kwa Siku ya Utume wa Kimisionari Duniani 2024. Kardinali Tagle alisema: “Utume wa Kanisa ni kutoka nje kwenda kwenye njia panda za ulimwengu na kualika kila mtu kwenye sherehe. Mashirika ya Kimissionari ya Kipapa pia yanaalikwa kuonesha kwa ari na majiundo yao kwamba, maisha yaliyoahidiwa na Yesu ni sawa na karamu ya mwaliko na kuvutia, wakati ambapo sehemu mbalimbali za dunia wengi hawaonekani kuwa na shauku hata kusikiliza ahadi hiyo ya Injili.”

Kardinali akilijikita na Karamu ya kualika, alisema kuwa Mfalme - Yesu anatuambia katika Injili ya Mathayo kuwa alikuwa ametuma watumishi wake kwenda kuwaita wageni kwenye arusi ya mwanawe, lakini wageni hawakutaka kuja. Baadhi yao pia walikuwa wamewatukana watumishi na kuwaua baadhi yao. Kisha mfalme akaamuru watumishi watoke nje tena, ili kuwaalika kila mtu wanayekutana naye njia panda kuja kwenye arusi. Akinukuu maneno ya mara kwa mara katika mafundisho ya Papa Francisko, alitoa maoni Kardinali Tagle, kuwa Kanisa linaitwa kwenda kuwaalika watu kwenye karamu. Alitoa mwaliko kuwa usilazimishe, watu kuja. Mahubiri yetu, maombi yetu, maisha yetu ya sakramenti, kazi yetu ya upendo, mahusiano yetu, ushuhuda wetu, haya yote lazima yawe mwaliko wa kuja, kuelekezwa kwa watu wote.”

Karamu ambayo kila mtu amealikwa, lazima iwasilishwe kama kitu cha kualika, cha kuvutia.” Papa Benedict XVI, alirudia mara nyingi kwamba imani inakua kwa mvuto, sio kwa kulazimishwa,  alikumbusha Kardinali Tagle. Kwa kuongeza alisema: “Swali langu ni: Je, tunawasilisha Injili kama sherehe ya Mungu pamoja na wanadamu? tunafanya karamu kuwa ya kuvutia?”Kuhusiana na hili, Kadinali alishirikisha Mkutano Mkuu vipindi vya ufasaha vilivyochukuliwa kutoka katika uzoefu wake kama mchungaji: “Nilipokuwa bado Askofu huko Manila, mwanamke mzuri sana na jasiri aliniambia: “Mwashamu, mimi ninakwenda kwenye misa kila siku, na huko Injili ya habari njema inatangazwa. Lakini mhubiri anapoanza kueleza, 'habari njema' inakuwa 'habari mbaya'....” Habari njema, mikononi mwa watu fulani, inakuwa habari mbaya. Na unawezaje kuwaalika watu kwenye karamu wakati habari njema inapoteza ladha yake?” alitoa maoni Kardinali Tagle.

Kipengele kingine alichojikita nacho Kardinali Tagle kilikuwa ni “Kupungua kwa kumbukumbu ya Kikristo. Kupendezwa na Kanisa  kunapungua katika sehemu nyingi za ulimwengu, ambapo hasa kati ya vijana aina yoyote ya dhamana muhimu na imani inakosekana. Imani ikikabiliwa na hali hii, suluhisho sio kufuta karamu. Kwa usahihi katika uso wa uhalisia wa ulimwengu wa sasa ni muhimu “kutoka nje ili kuwaalika kila mtu”, tukishinda tabia ya kuhutubia daima watu ambao tayari wanahusika katika kazi ya kitume ya Kanisa, au desturi ya “kuwaomba watu waje  mahali tulipo sisi.” Na kwa mtazamo wake  pia ulikuwa ni upande wa matazamio ya upeo mpya wa PMS.

Kardinali Tagle alipendekeza  kuwa kama vile watumishi katika fumbo la Kiinjili, Mashirika ya Kipapa ya Kimisionari pia yanaitwa kutafuta wageni kwa ajili ya karamu katika njia zote za maisha. Kazi yao ya kitume inapaswa kulenga “kila mtu”, kutafuta si tu “Wakatoliki waliojitoa” bali watu wote katika kitambaa halisi cha maisha yao ya kawaida. Hata Mkutano mkuu huo alisema “unaweza kutumika kupitia miundo yao na  na mbinu zao. “Tunaweza kujifunza kutoka kwa kila mmoja wetu, na pengine tunaweza kujiuliza kwa unyenyekevu: Je, miundo yetu, utendaji wetu, na njia yetu ya kufanya mambo inakuza “kutoka nje  kualika?” Kardinali Tagle pia alitaja makundi ya watu wa  kukumbuka ili kupanua upeo wa utendaji wa Mashirika ya Kimisionari ya Kipapa.  Na alitaja washawishi vijana  aliokutana nao katika Siku ya Vijana Ulimwenguni huko Lisbon (Walijiona kuwa wamisionari: waliwaalika wenzao kukaribia Injili); kwa wasanii waliohusika katika mipango ya kichungaji ya Jimbo Kuu la Manila (walikuwa picha za vijana, na walikuwa wakitafuta fursa ya kutoa ushuhuda wa imani yao), na kwa wanaume na wanawake wengi wa Ufilipino wanaohama kutafuta kazi (Papa Francisko, alipoadhimisha misa kwa ajili ya wahamiaji wa Kifilipino wanaofanya kazi, Roma, aliwaambia: “ninyi ni 'wasafirishaji wa imani.”)

Mnafika kama wafanyakazi wa kutunza na  walezi wa watoto, lakini pia mnaleta imani yenu katika nyumba na familia mnazoingia. Wafundishe watoto kusali. Bila kulazimika kuunda kazi mpya ya umisionari, na  labda tunaweza kutoa uangalifu kwa wageni wapya kwa vikundi hivi vipya ambavyo vinaweza kukuza utume wa  kuwaalika watu wengine kwenye karamu ya harusi. Kwa nji hiyo shughuli zote za PMS na shughuli zote za kikanisa zinaweza kuwa mwaliko wa karamu. Daima tukikumbuka kwamba mwaliko huo si mpango wa watu wa  Makanisa au kazi za kikanisa, bali “ni Baba ndiye aliyealika kila mtu kwenye karamu,” Kardinali Alihitimisha.

Kardinali Tagle kwa PMS
10 June 2024, 15:05