Tafuta

Kikanisa cha Sistine mjini Vatican. Kikanisa cha Sistine mjini Vatican.  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Kitabu:Miaka 50 ya sanaa ziliozopita na sasa kuanzia 1973-2023!

Kitabu chenye kichwa:“Sasa 50:Mkusanyiko wa Sanaa iliyopitia na ya Kisasa ya Makumbusho ya Vatican 1973-2023.Chimbuko-Historia–Mabadiliko,”kinafuatilia historia ya makusanyo madogo zaidi ya kipapa:kati ya tamaduni na uvumbuzi. Uwasilishaji wa kazi hiyo utakuwa tarehe 20 Juni 2024 alasiri

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Nyumba za Makumbusho ya Vatican, itawasilisha kitabu chenye kichwa: “Miaka 50 50:Mkusanyiko wa Sanaa iliyopita  na ya Kisasa ya Makumbusho ya Vatican 1973-2023. Asili-Historia - Mabadiliko. Tukio hilo litafanyika Alhamisi tarehe 20 Juni 2024, saa 11.30 jioni, katika Chumba cha Mikutano cha Nyumba ya Makumbusho ya Vatican. Mada hiyo  itatambulishwa na Barbara Jatta, Mkurugenzi wa Makumbusho ya Vatican, na kuona ushiriki wa Elisabetta Cristallini, Profesa wa Chuo Kikuu cha Tuscia, na Giuseppe Appella, mwanahistoria wa sanaa na mkosoaji.

 Zaidi ya hayo, wahariri wa kitabu hicho  Micol Forti, Francesca Boschetti na Rosalia Pagliarani watakuwepo. Kitabu hicho, kinataka kuadhimisha miaka 50 tangu kuzaliwa kwa Mkusanyiko wa Sanaa ya zamani  na ya Kisasa ya Makumbusho ya Vatican, ikirejea historia yake kuanzia kwenye hotuba iliyotolewa na Papa Paulo VI katika Kikanisa cha Sistine mjini Vatican tarehe 23 Juni 1973, kwenye hafla ya uzinduzi wa Mkusanyiko(https://www.vatican.va/content/paul-vi/it/speeches/1973/june/documents/hf_pvi_spe_19730623_collezione-arte-religiosa.html).

Tukio la kihistoria ambalo Papa Francisko alitaka kulirudia mwaka 2023 sanjari na kumbukumbu ya miaka 50 tangu kufunguliwa kwa Mkusanyiko huo, kwa kuwakutanisha tena wasanii katika Kikanisa cha Sistine ili kusisitiza umuhimu wa uhusiano, kati ya Kanisa na wasanii, ambayo yeye mwenyewe alifafanua kuwa asili na Maalum(https://www.vatican.va/content/francesco/it/speeches/2023/june/documents/20230623-artisti.html).

Kuanzia mkutano kati ya Papa Paulo VI na ulimwengu wa sanaa, kitabu hiki kinachambua uhusiano kati ya Sanaa na Imani, iliyounganishwa kwa miaka mingi wakati wa mapapa mbalimbali, na kinasimulia maendeleo ya Mkusanyiko wenyewe: mabadiliko ambayo yameathiri njia juu ya maonyesho ya miongo, maonyesho mengi, ushiriki katika semina na mikutano muhimu, pamoja na ukuaji mkubwa wa ununuzi. Historia ambayo katika mfululizo uliobainishwa wa matukio humpelekea msomaji kugundua mageuzi ya ajabu ya mkusanyiko mdogo zaidi wa Makumbusho ya Vatican yenye sifa tangu kuzaliwa kwake kwa uwiano kati ya utamaduni na uvumbuzi.

Nyumba ya Makumbusho Vatican na Kitabu

 

18 June 2024, 17:23