Makao mapya ya Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Ulaya(CCEE)yahamia Roma!
Vatican News
Baada ya zaidi ya miaka hamsini, Shirikisho la Baraza la Mabaraza ya Maaskofu wa Ulaya, (CCEE,) ambayo yana lengo la kukuza na kulinda mema ya Kanisa na kuundwa na wanachama 39, ikiwa ni pamoja na Mabaraza ya Maaskofu 33 ya kitaifa yanayowakilisha nchi 45 za Kanisa katika bara la zamani, Ulaya limehamisha makao yake makuu ya sekretarieti kutoka Uswiss hadi Roma. Majengo mapya yako Jumba la Maffei, kupitia njia ya Pigna Roma ambayo yalizinduliwa na Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican. Akitoa neno Kardinali Parolin alisisitiza vipengele vyote viwili vya kiufundi vya chaguo hili ambalo alisema ni ukaribu na Papa na Mabaraza ya Kipapa ya Vatican na yale ya mahalia. Kardinali alisema: “Kumbuka kwamba ushirika wa kikanisa lazima uwe na thamani ya ulimwengu wote na unatekelezwa kikamilifu Cum Petro na sub Petro.”
Sababu ya kihistoria
Uamuzi huo, uliochukuliwa na marais wa Mabaraza ya Maaskofu wa kitaifa mnamo Novemba mwaka 2023 huko Malta na kisha kupitishwa baada ya kushauriana na Papa, Sekretarieti ya Vatican na Baraza la Kipapa la Maaskofu, alikumbusha hayo rais wa CCEE, Askofu Mkuu Gintaras Grušas, wa Vilnius, na kwamba “unazingatia mabadiliko ya hali ya sasa ya kihistoria. Wakati CCEE ilipoanzishwa, kwa hakika, Ulaya iligawanywa mara mbili kati ya mashariki na magharibi na maaskofu wa bara zima walikuwa wakitafuta mahali pa kukutana. Ofisi za sekretarieti zilianzishwa kwanza huko Chur mnamo 1971 na kisha huko Mtakatifu Gallen mnamo 1997.”
Kituo cha kumbukumbu kwa maaskofu wa Ulaya
Kardinali Parolin alieleza kwa vyombo vya habari vya Vatican, kuwa “Uhamisho huu unajibu kwanza mahitaji ya kiufundi sana. Mahali hapa ni pazuri zaidi na hujibu vyema mahitaji, lakini pia kujibu kwa maana ya kina na ya kiishara ambayo hasa ni ile ya kuweka muungano huu wa kina na Baba Mtakatifu na Kiti cha Petro katikati ya shughuli za Ulaya na Baraza la Kipapa la Maaskofu”. Kusudi ni kufanya mahali hapa kuwa “kituo cha marejeo pia kwa maaskofu wa Ulaya, ambao watakapokuja Roma wataweza kupata makaribisho hapa kwa mikutano na mawasiliano na ofisi. Na hii itaongezeka kwa kawaida kwa Jubilei.” Akiwa anaaminisha Jibilei inayokuja.
Uinjilishaji na ushuhuda wa upendo
Katika hotuba yake ya ufunguzi, aidha Katibu wa Vatican alikumbuka kwamba “asili ya Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Ulaya (CCEE) ni kuongeza ushirikiano kati ya maaskofu wa Ulaya kwa kuzingatia uzoefu wanaoishi na Mabaraza ya Vatican, inayoitwa leo kuchukua uso wa kisinodi, na ule wa Kanisa ambalo, kuanzia neno la kweli la Injili, linawafikia wanaume na wanawake wa wakati wetu. Kuakisiwa na kuungwa mkono na uwepo wa Kristo.” Hasa kwa njia ya kujitolea kuinjilisha ambayo haipaswi kamwe kukosa ushuhuda wa ukweli, hasa katika wakati wetu ambao hauonekani tena kuelewa usawa upitao wa ukweli, na kuupunguza kwa makubaliano tu ya kijamii na hisia za wakati huu. Vivyo hivyo, ushirika wa kidugu na ushuhuda wa upendo hauwezi kukosa kwa wale wanaoteseka, wanyonge na waliotengwa, waathiriwa wa tamaduni ya kutupa, ambapo kila kitu ni cha kupita kiasi, hata kile ambacho sio cha kupita kiasi kama zawadi ya maisha ya mwanadamu.yenyewe, hasa ile dhaifu na isiyo na kinga.”
Msukumo wa kiekumene kwa ajili ya amani
Ahadi ya CCEE, Kardinali Parolin inakwenda kwenye miongozo mikuu ya Ushirika wa Kikanisa, msaada wa kichungaji na msukumo wa kiekumene ili kukabiliana na changamoto kubwa za siku hizi: “Hebu tufikirie juu ya mada ya kutokuwa na dini na uinjilishaji ambayo katika Ulaya inatoa kwa namna ya kutisha. . Lakini basi pia kwa amani. Kuweza kuingiza roho ya amani katika Ulaya hii ambayo inajikuta ikiwa imegawanyika sana.”