Sinodi,kazi ya II ya Instrumentum laboris inaanza!
Vatican News
Waraka wa Kitendea Kazi (Instrumentum Laboris) kuelekea Oktoba 2024 ulipotumwa mwezi Desemba 2023 kwa Maaskofu wote wa duniani, Sekretarieti Kuu ya Sinodi iliomba makanisa mahalia na vikundi vya Makanisa kutafakari kwa kina baadhi ya vipengele vya Ripoti ya Muhtasari ambayo ni msingi wa mada ya Sinodi, kuanzia na swali elekezi la mchakato mzima wa sinodi: “Jinsi gani ya kuwa Kanisa la Sinodi katika utume? Katika miezi ya hivi karibuni, makanisa mahalia pamoja yametekeleza kazi yao kwa kutuma mchango wao kupitia Mabaraza ya Maaskofu, Makanisa Katoliki ya Mashariki na Mikutano ya Kimataifa ya Mabaraza ya Maaskofu.
Jumanne 4 hadi 13 Juni kikao cha maandalizi
Kwa njia hiyo kuanzia Jumanne tarehe 4 Juni 2024, kundi la Wataalimungu, wataalam wa taaluma mbalimbali (dogmatics, eklesia, taalimungu ya kichungaji, sheria za kanoni, nk), wapatao ishirini kutoka sehemu zote za dunia walifika Roma kuanza kazi ya uundaji wa hati ya kazi ya kikao cha pili cha Mkutano Mkuu wa kawaida wa XVI wa Sinodi ya Maaskofu. "Na hakuna chochote cha kubahatisha," alisema Kardinali Grech.
Kila hati lazima isomwe kwa uangalifu kwa lengo la kupendekeza mwishoni mwa mchakato maandishi ambayo yanaonesha kazi, maswali na hisia zilizopokelewa kutoka kwa msingi,” alisema Kardinali Grech. “Nimevutiwa hasa kuona ushiriki wa jumuiya nzima ya kikanisa katika mchakato huu mrefu wa utambuzi,”. Pamoja na tafakari zinazotokana na kazi ya Ripoti ya Muhtasari wa Kikao cha Kwanza, nyenzo zilizopokelewa mara nyingi pia huongeza ushuhuda halisi kuhusu jinsi makanisa mahalia sio tu yanaelewa sinodi, lakini tayari yanaitekeleza katika vitendo. Kanisa la Sinodi sio ndoto ya kutimizwa, lakini tayari ni ukweli hai unaozalisha ubunifu na mifano mipya ya uhusiano ndani ya jumuiya moja ya mahali au kati ya makanisa tofauti au vikundi vya Kanisa.” Alsisitiza Kardinali Mario Grech. Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Sinodi.
Michango ya Usg na Uisg na mapadre wa parokia
Sekretarieti Kuu ya Sinodi pia ilipokea michango kutoka kwa Umoja wa Mama Wakuu wa Mashirikia (USG-UISG) na idadi inayofaa ya uchunguzi, kutoka kwa vyombo vya kimataifa, vitivo vya vyuo vikuu, vyama vya waamini au jumuiya binafsi na watu. Chanzo kingine muhimu cha kutafakari kitakuwa ripoti zilizowasilishwa na mapadre wa parokia ya wakati wa siku tatu za kazi ya hivi karibuni mjini Roma kwa ajili ya mkutano wa Sinodi.
Uchambuzi wa kwanza
Kwa upande wake, Padre Giacomo Costa, Katibu Maalum wa Baraza la XVI alibainisha: “Bado si suala la kuandika Instrumentum laboris kwa Kikao cha Pili cha Sinodi ya Sinodi, bali kufanya uchambuzi wa awali wa mahusiano na matendo mema yanayotekelezwa na jumuiya mahalia na utambuzi wa pamoja juu ya masuala ya kitaalimungu na tafakari ili kuandaa njia ya uandishi halisi wa maabara ya Instrumentum laboris.” Kazi ya timu hii ya kimataifa, ilianza kwa mapumziko ya nusu siku ya kiroho na itaendelea hadi Juni 13. Siku zitawekwa alama kwa nyakati tofauti za kazi (mtu binafsi, katika kikao cha jumla na katika vikundi). Adhimisho la kila siku la Ekaristi na nyakati za sala ya kibinafsi zitahakikisha kwamba kazi inafanyika katika hali inayohitajika kwa utambuzi.
Hatua zinazofuata Mchakato wa kuendeleza Instrumentum Laboris utaendelea na hatua nyingine, kwani mara tu muundo wa hati ya baadaye utakapotambuliwa shukrani kwa maelezo ya nyenzo zilizopokelewa kutoka kwa wataalimungu, Baraza la Kawaida litafanya utambuzi wa kwanza wa kile ambacho kimefafanuliwa. Hatua za kuandaa waraka halisi na mfumo mpana wa uthibitishaji zitafuata hadi idhini ya Baraza la Kawaida ili kuwasilishwa kwa Baba Mtakatifu atoe idhini ya uhakika. Uchapishaji wamaandishi unatarajiwa ndani ya siku kumi za kwanza za mwezi Julai 2024. Taarifa kuhusu hili zitatolewa kwa wakati ufaao.