Baraza la Makardinali(C9)na Papa Francisko unaendelea
Vatican News
Mkutano wa C9 yaani Baraza la Makardinali 9 ambao ni washauri wa Baba ulioanzishwa na Baba Mtakatifu ili kumsaidia katika mpango wa mageuzi ya Kanisa la Roma na katika mamlaka ya Kanisa, unaendelea Juni 18, mbele ya Baba Mtakatifu Francisko mjini Vatican ambapo ulianza tarehe 17 Juni. Huu ni mkutano wa tatu wa mwaka 2024 baada ya ule wa mwezi Februari na Aprili iliyopita
Kazi ya Aprili
Katika kikao kazi cha mwisho mwezi Aprili, mkazo ulikuwa katika utekelezaji wa katiba ya kitume Praedicate Evangelium ya Curia Romana, juu ya matukio ya vita katika sehemu mbalimbali za dunia, hasa Mashariki ya Kati na Ukraine kwa matumaini makadinali hao washauri na Papa kwamba juhudi zinazolenga kubainisha njia za mazungumzo na amani ziongezwa. Pia katika mikutano iliyopita, washiriki wa Baraza la Makardinali hao washauri walikuwa wamejadili juu ya “"ukumu la wanawake katika Kanisa” na kusikiliza tafakari ya wanawake wawili, Sr Regina da Costa Pedro na Profesa Stella Morra.
Upyaishaji wa Baraza la Makardinali Washauri C9
Baraza la Makardinali washauri baada ya kupyaishwa muhimili wake na Papa tarehe 7 Machi 2023, limeunda na Makardinali: Pietro Parolin, katibu wa Vatican; Fernando Vérgez Alzaga, Rais wa Tume ya Kipapa ya Mji wa Vatican na Gavana tawala wa mji wa Vatican; Fridolin Ambongo Besungu, Askofu mkuu wa Kinshasa; Oswald Gracias, Askofu Mkuu wa Bombay; Seán Patrick O'Malley, Askofu Mkuu wa Boston; Juan José Omella Omella, askofu mkuu wa Barcelona; Gérald Lacroix, askofu mkuu wa Quebec; Jean-Claude Hollerich, askofu mkuu wa Luxembourg; Sérgio da Rocha, askofu mkuu wa San Salvador de Bahia. Katibu ni Monsinyo Marco Mellino, askofu mkuu wa Kipaimara. Mkutano wa kwanza wa C9 mpya ulifanyika tarehe 24 Aprili 2024.
Kuanzishwa kwa Baraza la Makardinali
Baraza hilo lilianzishwa na Baba Mtakatifu Francisko kwa hati iliyoandikwa na mkono wake mnamo tarehe 28 Septemba 2013 kwa jukumu la kumsaidia katika utawala na shughuli za Kanisa la Ulimwengu na wakati huo huo kusoma mapango wa marekebisho ya Katiba ya Curia ya Kirumi, iliyotekelezwa na katiba mpya ya kitume ya Praedicate Evangelium, yaani Hubirini Injili ambayo ilichapishwa tarehe 19 Machi 2022. Mkutano wa kwanza kabisa wa Baraza la Makardinali 9 washauri (C9) ulifanyika mnamo tarehe 1 Oktoba 2013.