Wakati wa ziara ya ya Kichungaji mjini Vatican ya maaskofu wa Senegal(2022). Wakati wa ziara ya ya Kichungaji mjini Vatican ya maaskofu wa Senegal(2022).  (Vatican Media)

Papa amemteua Padre Valter Manga kuwa Askofu wa Ziguinchor,Senegal

Papa amemteua kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Ziguinchor nchini Senegal,Padre Jean Baptiste Valter Manga,wa jimbo hilo hilo,ambaye hadi uteuzi huo alikuwa ni makamu Gambera wa Seminari Kuu ya Notre Damehuko Brin na Paroko Msaidizi wa Parokia ya Mchungaji mwema ya Enampore.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Alhamisi tarehe 20 Juni 2024, Baba Mtakatifu Francisko amemteua kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Ziguinchor nchini Senegal, Padre Jean Baptiste Valter Manga, wa jimbo hilo la  Ziguinchor, ambaye hadi uteuzi alikuwa ni makamu Gambera wa Seminari Kuu ya Mama Yetu huko Brin na Makamu Paroko wa  Parokia ya Mchungaji Mwema, Enampore.

Wasifu wake

Mheshimiwa Padre  Jean Baptiste Valter Manga, wa Jimbo la  Ziguinchor, alizaliwa mnamo tarehe 18 Juni 1972 huko Oussouye (Senegal). Baada ya mzunguko wa masomo ya  Falsafa katika Seminari ya Falsafa ya Brin (1993-1995), aliendelea na Taalimungu katika Seminari Kuu ya Sébikhotane (1995-2000). Alipata Leseni katika Taalimungu  ya Kibiblia kutoka Chuo cha Bernard, jijini Paris, Ufaransa,  mwaka 2009, na Shahada ya Uzamivu katika ethnolojia na anthropolojia Chuo cha Masomo ya Juu katika Sayansi Jamii (EHESS) huko  Paris, Ufaransa mnamo mwaka wa 2015. Mhemishimiwa Padre Manga alipewa daraja la Upadre mnamo tarehe 20 Desemba 2000.

Nyadhifa nyingine

Mheshimiwa Padre Manga alishika nyadhifa nyingine kama vile kuwa : Profesa wa Hisabati na Sayansi Asilia katika seminari ndogo ya Ziguinchor na Mkuu wa Tume ya Miito (2000-2006); Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Benedikto wa Nema (2015-2021); Profesa katika Seminari Kuu ya Brin na katika Chuo Kikuu cha Assane Seck cha Ziguinchor (2015 hadi uteuzi wake); Padre wa Parokia ya Nyassia(2021-2023); Katibu Mkuu wa Ofisi ya Utunzaji wa hazina ya Kichungaji wa Jimbo na anayehusika na Mafunzo yanayoendelea ya Mapadre (2021 hadi uteuzi wake); tangu 2023 amekuwa Makamu Gambera Seminari Kuu ya Notre Dame huko Brin na Paroko wa Parokia ya Mchungaji Mwema huko Enampore.

Askofu Mpya wa Jimbo la Ziguinchor, Senegal
20 June 2024, 17:32