Papa ameridhia kutangazwa kwa Wenyeheri wapya!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Wakati wa mkutano wa Baba Mtakatifu Francisko na Kardinali Marcello Semeraro, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mchakato wa kuwatangaza Watakatifu, Alhamisi tarehe 20 Juni 2024, Baba Mtakatifu ameridhia Baraza hilo kutangaza hati zinazohusu Watumishi wa Mungu kuwa Waenyeheri,wafuatao: kifo cha kishahidi cha Mtumishi wa Mungu Luigi (zamani Matteo) Palić, kwa Kialbania Paliq, wa Shirika la Ndugu Wadogo(OFM); alizaliwa tarehe 20 Februari 1877 huko Janjevo (Kosovo) na kuuawa kwa sababu ya chuki kwa imani tarehe 7 Machi 1913 huko Peje (Albania); - kifo cha kishahidi cha Mtumishi wa Mungu Giovanni Gazulli, Padre wa jimbo; alizaliwa tarehe 26 Machi 1893 huko Dajç di Zadrima (Albania) na kuuawa kwa chuki ya imani tarehe 5 Machi 1927 huko Scutari (Albania).
Fadhila za kishujaa za Mtumishi wa Mungu Isaya Columbro (zamani aliitwa: Nicola Antonio Maria), Padre wa Shirika la Ndugu Wadogo(OFM); alizaliwa tarehe 11 Februari 1908 huko Foligno (Italia) na alikufa huko Vitulano (Italia) mnamo 13 Julai 2004;- fadhila za kishujaa za Mtumishi wa Mungu Maria Costanza Zauli (zamani aliitwa Palma Pasqua), wa Shirika la Wajakazi wa Moyo Mtakatifu na Mwanzilishi wa Vijakazi vya Waabuduo Sakramenti Takatifu; alizaliwa tarehe 17 Aprili 1886 huko Faenza (Italia) na alikufa huko Bologna (Italia) mnamo 28 Aprili 1954;
Fadhila za kishujaa za Mtumishi wa Mungu Ascensión Sacramento Sánchez wa Taasisi ya Kidunia ya Kiinizi ya Cruzada; alizaliwa tarehe 15 Juni 1911 huko Sonseca (Hispania) na alikufa huko Madrid (Hispania) mnamo 18 Agosti 1946; fadhila za kishujaa za Mtumishi wa Mungu Vincenza Guilarte Alonso, wa Shirika la Mabinti wa Yesu; alizaliwa tarehe 21 Januari 1879 huko Rojas de Bureba (Hispania) na alikufa huko Leopoldina (Brazil) mnamo 6 Julai 1960.