Parolin:Kuhusu silaha za Nato kwa Urusini ni hofu kwa anayejali hatima ya ulimwengu!
Na Salvatore Cernuzio na Angella Rwezaula – Vatican.
Wakati barani Ulaya linazidi kipanua wigo lake la Ndiyo, na orodha ya nchi zinazoondoa marufuku ya matumizi ya silaha za NATO kwenye eneo la Urusi linakua. Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican alizungumzia juu ya matarajio ya kutatanisha. Kwake yeye alisema kuidhinisha jeshi la Ukraine kuipiga Urusi kwa silaha zilizotolewa na nchi za Magharibi ambayo ni dhana katikati ya mkutano usio rasmi wa mawaziri wa mambo ya nje uliofanyika tarehe 30-31 Mei 2024 huko Prague, kunaweza kuongeza hali ngumu ambayo hakuna mtu atakayeweza kudhibiti tena. Kwa hiyo haya ni matarajio ya kutatanisha kweli, alisema Kardinali Parolin akiwa Milano, tarehe 31 Mei 2024 akiwa katika Maktaba ya Ambrosiana, kwenye uwasilishaji kitabu juu ya “Bernardino Nogara”, mwana benki ya Kiitaliano na mwanzilishi wa IOR, chenye kichwa: “Katika huduma ya Italia na Papa,” kilichohaririwa na Angelo Caleca. Kardinali Parolin kwa njia hiyo hakuficha wasiwasi wake kuhusu hali hizi zinazowezekana kwamba "inapaswa kuwa wasiwasi sawa,na kila mtu anayejali kuhusu hatima ya ulimwengu wetu. Hatari ni kweli.”
Ahadi ya kibinadamu ya kurudi kwa watoto wa Kiukraine
Kuhusu Vatican, katika mazingira ya mzozo wa Kiukraine inaendelea kujitolea kwake katika ngazi ya kibinadamu, hasa Kardinali Parolin alielezea kwa waandishi wa habari juu ya suala la kurudi katika nchi yao ya watoto wa Kiukreni waliochukuliwa kwa nguvu. Kardinali Pietro Parolin, kwa hiyo alithibitisha juu ya dhamira ya kibinadamu ya Vatican kwa ajili ya kurudi kwa watoto Ukraine. “Utaratibu ulianza na ziara ya Kadinali Matteo Maria Zuppi, rais wa Baraza la Maaskofu Italia (CEI,) mwaka 2023 huko Kyiv na Moscow na ambayo inaendelea sio haraka sana lakini ambayo inazaa matunda. Tunafanya kazi katika maeneo hayo, hakuna nafasi nyingine,” Alisisitiza Kardinali.
Uchaguzi wa Ulaya, utekelezaji wa demokrasia
Kisha akijibu maswali kuhusu uchaguzi ujao wa Ulaya, Kardinali Parolin alisisitiza kwamba msimamo wa Kanisa hauegemei upande wowote na kwamba hatuwezi kujieleza kwa kupendelea au dhidi ya moja au nyingine.” Hata hivyo, alisisitiza: “umuhimu wa kushiriki, kueleza kura yako, kwa sababu hii ina maana ya kutekeleza na kutekeleza demokrasia. Wakati huo huo lazima tuzingatie maadili ya wagombea ambao wako karibu, sawa na unyeti wa Kikatoliki. Ningesema kwamba hizi ndizo kanuni tunazopaswa kuzingatia kadiri tunavyohusika.”
Kuna mambo mengi ya kutia chumvi kuhusu fedha za Vatican
Hatimaye, kwa kutazama sura na kazi ya Nogara, “ Mtu wa Kanisa mwaminifu kwa Papa, kwa Vatican, ambaye aliendeleza njia mpya ya kusimamia fedha za Kanisa” Kardinali Parolin alionesha sifa zinazohitajika kwa wale ambao kazi katika uwanja wa kifedha: “Kuwa na uwezo, uaminifu na uwazi.” Katibu wa Vatican alitoa maoni, yaliyoombwa na waandishi wa habari, juu ya hali ya fedha ya Vatican. “Na ikiwa anakumbuka kwamba kulikuwa na jitihada kubwa kwa upande wa Papa kurejesha fedha katika mpangilio, ni kweli pia kwamba pia kulikuwa na chumvi nyingi juu ya fedha za Vatican, sisemi habari za uongo lakini hakika kuzidisha.”
Sadaka kwa Kanisa ni kwa manufaa ya watu
Ninaamini kwamba kazi inayofanywa na Papa inaweza kuwa ya manufaa na kuruhusu Vatican kusonga mbele kwa utulivu, hata kama ni dhahiri hali ya jumla si nzuri hasa, hasa kuhusu matoleo kutoka kwa waamin.” Matoleo ambayo huelekea kupungua, kama karibu kila mahali, hata katika kiwango cha Majimbo. Kwa mujibu wa Kardinali, kichocheo ni kile cha kuaminika zaidi kwa upande wa Kanisa, kuwa wa kuaminika na kuhisi kuwa ni wa kutegemewa. Kwa upande mwingine, “Kanisa linafanya mema mengi, hatupaswi kusahau hili. Na amini kwamba vingi katika vile mnavyotoa ni kwa ajili ya manufaa ya watu.”