Nchi Takatifu: mtazamo wa Nyumba ya Galilaya huko Tiberiade Nchi Takatifu: mtazamo wa Nyumba ya Galilaya huko Tiberiade 

Mkutano wa Roaco:mtazamo wa Nchi zinazoteseka na vita!

Kuanzia tarehe 24 hadi 27 Juni 2024 kutakuwa na mkutano wa 97 wa Mwaka wa amba ni Mkutano wa Kazi za Msaada wa Makanisa ya Mashariki(ROACO).Utakafanyika katika Ukumbi wa Mikutano ya Nyumba Kuu ya Shirika la Wajesuit.Kati ya mada ni pamoja na kuakisi hali ya Nchi Takatifu,kupitia michango ya Mjumbe wa Kitume wa Yerusalemu.

Vatican News

Baraza la Makanisa ya Mashariki limetoa taarifa kuwa kuanzia tarehe 24 hadi 27 Juni 2024 kutakuwa na mkutano wa  97 wa Mwaka wa Mkutano wa Matendo ya Kaziyza Msaada wa Makanisa ya Mashariki(ROACO,) utakaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano ya Nyumba Kuu ya Shirika la  Wajesuit, jijini Roma. Kwa njia hiyo Jumanne tarehe 25 Juni 2024 majira ya  saa 2.30, asubuhi, Kardinali Claudio Gugerotti, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Makanisa ya Mashariki na Rais wa ROACO, anatarajia kuongoza Ibada ya Misa Takatifu kwa ajili ya uzinduzi wa mkutano huo, ambapo katikati ya misa hiyo watawakumbuka wafadhili walio hai na wafu na watasali kwa ajili ya amani, huku wakimkabidhi Bwana, kwa maombezi ya Mama wa Mungu, Nchi ambazo zinateseka kwa sababu ya vita, huku wakiungana katika mikutano iliyomo katika ratiba yao

Katika kipindi cha kwanza wataakisi hali katika Nchi Takatifu, kupitia michango ya Mjumbe wa Kitume, Yerusalemu, Askofu mkuu Adolfo Tito Yllana, Msimamizi wa Nchi Takatifu na na  Mlima Sayuni, Padre Francesco Patton (OFM,) na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Bethlehem, Ndugu Hernan Santos (FSC); habari inayohusiana na Mkusanyo wa sadaka  wa 2023 Pro Terra Sancta pia itashirikishwa. Katika kikao cha mchana, Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu wa Uhusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa, ataingilia kati kwa kuwasilisha muhtasari wa hatua ya kidiplomasia ya Vatican katika hali ya sasa, akimaanisha Ukraine, Mashariki ya Kati na Ethiopia. Hapo pia  mwelekeo utahamia eneo la Karabakh, kutokana na ripoti ya Gevork Saroyan, Mkuu wa Huduma ya Kijamii wa Mama Vatican,   Etchmiadzin na Mwakilishi wa Upatriaki Mkuu na Wakatoliki wa Waarmenia Wote H.H. Karekin II.

Jumatano tarehe 26 Juni 2024  ratiba ni kutafakari mada: “Utunzaji wa kichungaji wa Wakatoliki wa Mashariki wanaoishi nje ya Eneo ya Kanda: changamoto na uwezekano wa leo. “Wazungumzaji watakuwa ni Borys Gudziak, Mkuu wa  Wakatoliki wa kigiriki kutoka Ukraine huko Philadelphia;  Frank Y. Kalabat, Askofu wa Wakaldayo wa Detroit; Mchungaji Éric Millot, Mkurugenzi wa Ofisi ya Uhamiaji na Utume wa Baraza ya Maaskofu wa Ufaransa; Askofu  Antoine Audo, wa Wakaldayo wa Aleppo; Daoud Boutros Tayeh, Katibu Mkuu wa Baraza la Kichungaji la Upatriaki wa  Maronite ya Jounieh. Kardinali Mario Zenari, Mjumbe wa Kitume nchini Siria, pia atazungumza kuripoti kuhusu maendeleo ya mradi wa "Hospitali Huria".

Kazi itahitimishwa na Kamati ya Uongozi mwishoni mwa Mkutano Mkuu, ili kupanga uteuzi wa siku zijazo. Mkutano wa pamoja na Baba Mtakatifu umepangwa asubuhi ya Alhamisi tarehe 27 Juni 2024. Mbali na wasemaji, kutakuwapo na wawakilishi wa Mashirika ya Kikatoliki ambayo ni sehemu ya ROACO, Wakuu na Viongozi wa Ukanda wa Makanisa ya Mashariki, baadhi ya Wawakilishi wa Kitengo cha Mahusiano cha  Sekretarieti Vatican, Baraza la Kipapa la Uhamasishaji wa Umfaragha ya kazi, itakuwapo na hivyo mahojiano hayatatolewa.

21 June 2024, 18:04