Siku ya Upendo na Papa:Sadaka ya Mtakatifu Petro 30 Juni 2024
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Kwa Kanisa Katoliki Ulimwenguni, linahamasishwa Dominika tarehe 30 Juni 2024 kutoa mchango wake mdogo kwa kadiri ya moyo unavyomtuma. Majitoleo haya kwa hakika ni alama ya ushirika na Khalifa wa Mtakatifu Petro kwa ajili ya kuwasaidia maskini na wahitaji zaidi na ni huduma muhimu sana ya Kikanisa Ulimwenguni kote.
Kwa njia hiyo: “Msaidie Papa hata wewe ili naye asaidie, kwa ishara ndogo lakini yenye thamani kubwa ambayo unaweza kuonesha upendo na imani kwa Baba Mtakatifu, katika fursa ya Siku ya Upendo kwa Papa, Dominika tarehe 30 Juni 2024. Kwa pamoja tumsaidie Papa katika utangazaji wa Injili katika majitoleo, kwa ajili ya wengine wenye uhitaji zaidi, watu, familia zenye matatizo, watu waliokumbwa na vita au wenye uhitaji wa kibidamu. Ili kufanya hivyo ingia kwenye Tovuti ya “Sadaka ya Mtakatifu Petro au“L'Obolo di San Pietro” au kwa Lugha ya Kiingereza “Peter’s Pence”.www.va na bonyeza toa mchango wako sasa:https://www.obolodisanpietro.va/it/cos-e-l-obolo/obolo-di-san-pietro.html.
Siku ya kuonesha ya upendo kwa Papa ilianzishwa 1871
Ndugu msikilizaji/ msomaji wa Vatican New, Mshikamano wa udugu wa kibinadamu una mzizi wa kina katika mfano wa Msamaria Mwema. Kwa njia hiyo “Sadaka ya Mtakatifu Petro “L'Obolo di San Pietro” au kwa Lugha ya Kiingereza “Peter’s Pence” au “Denarius Sancti Petri” ilianzishwa na Mwenyeheri Papa Pio IX mnamo tarehe 5 Agosti 1871, ili kumjengea Khalifa wa Mtakatifu Petro nguvu ya kiuchumi. Hii ni sadaka inayotolewa na waamini wote wa Kanisa Katoliki kutoka sehemu mbalimbali za Ulimwengu ambapo katika fursa ya Siku Kuu ya Mtakatifu Petro ifanyikayo kila tarehe 29 Juni ya kila mwaka, Dominika ambayo hufuata Siku Kuu hiyo, ndiyo iliweka kuonesha upendo kwa Papa.
Majitoleo katika kukuza na kudunumisha uhuru wa kuabudu,haki,amani na udugu wa kibinadamu
Lengo la majitoleo haya ni kukuza na kudumisha uhuru wa kuabudu; haki, amani na mshikamano wa udugu wa kibinadamu. Sadaka hii tangu wakati huo imekuwa ni kilelezo cha mshikamano wa huduma ya upendo na Khalifa wa Mtakatifu Petro inayopata chimbuko lake katika Maandiko Mtakatifu. “Akawajibu akiwaambia, Mwenye kanzu mbili na ampe asiye na kanzu; na mwenye vyakula na afanye vivyo hivyo,” (Lk 3:11.). Lakini toeni sadaka vile vya ndani, na tazama, vyote huwa safi kwenu,” (Lk 11: 41) na kwamba imani bila matendo imekufa. Yak 2:15-16. Ni katika muktadha huo ambapo, Baba Mtakatifu kupitia michango hii, anawakimbilia wengi wenye kupta majanga mbali mbali kama ambayo tunayona kila wakati, kukimbilia wanaoteseka na vita, wanaopata na maafa ya asili na mengine mengi. Haya yote yasingewezekana kama siyo sadaka ya waamini wenye mapenzi mema kwa ajili ya ndugu zao. Kwa njia hiyo tumsaidie Papa na ili aweze kusaidia pia. Hii inadhihirisha hisia ya kuwa wa Kanisa na upendo na uaminifu kwa Baba Mtakatifu. Ni ishara madhubuti ya ushirika naye, kama mrithi wa Mtakatifu Petro, na pia ya kuzingatia mahitaji ya wahitaji zaidi, ambao Papa huwatunza kila wakati.
Toa zawadi yako sasa:
IT: https://www.obolodisanpietro.va/it/dona.html
ENG: https://www.obolodisanpietro.va/en/dona.html
ES: https://www.obolodisanpietro.va/es/dona.html