Tafuta

2024.06.13 Washiriki wa Mkutano wa wakuu wa Vyama vya waamini, Harakati za kikanisa na Jumuiya Mpya. 2024.06.13 Washiriki wa Mkutano wa wakuu wa Vyama vya waamini, Harakati za kikanisa na Jumuiya Mpya.  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Sinodi na utume,mkutano wa wasimamizi wa harakati huko Vatican!

Zaidi ya wawakilishi 200 wa vyama vya waamini, ukweli wa kikanisa na jumuiya mpya walikusanyika kwa ajili ya tukio lililoandaliwa na Baraza la Kipapa la Walei, Familia na Maisha.Katika Ufunguzi wa Kardinali Farrell alisema:Sinodi haitekelezwi kwa kuingiza wanaume na wanawake walei katika mahali pa mamlaka ya Kanisa;kinyume ni lazima itumike kwa pamoja na kutafuta njia pamoja kwa msukumo mpya wa utume wa uinjilishaji wa Kanisa.

Osservatore Romano

Tukitafakari mada ya sinodi ya kimisionari tunaomba upendo ambao ni zawadi ya Roho Mtakatifu kwa sababu katika mahusiano yetu binafsi, katika familia zetu, katika jumuiya zetu za kikanisa, daima tuna upendo wa dhati kwa ndugu ambao Bwana ameweka pembeni yetu. Alisema hayo Kardinali Kevin Farrell katika mkutano wa wakuu wa Vyama vya waamini, Harakati za kikanisa na Jumuiya Mpya. zinazohamasishwa na Baraza la Kipapa la Walei, Familia na Maisha (DLFV) uliofanyika Alhamisi tarehe 13 Juni 2024. Ukumbi mpya wa Sinodi mjini Vatican ambapo pia walihutubiwa na Papa Francisko. Maneno yake yalijidhihirisha katika Altare ya  Kanisa kuu la Mtakatifu Petro, ambapo Kardinali aliongoza Misa Takatifu iliyotangulia Hotuba ya Papa  katika ufunguzi rasimi.

Mkutano wa wakuu wa vyama vya kikanisa
Mkutano wa wakuu wa vyama vya kikanisa

Katika mahubiri hayo, Kadinali Farrell alitoa maoni yake kuhusu masomo ya siku hiyo, huku akisisitiza hasa jinsi ambavyo Yesu alivyoweka "sharti la lazima la kuingia katika Ufalme wa mbinguni: kuwa na haki iliyo kuu kuliko ile ya waandishi na Mafarisayo.” Hiyo kiukweli, licha ya kuwa mwangalifu sana, walifikiria karibu tu juu ya uhusiano na Mungu; kwa hiyo haki yao ilizingatia mwelekeo wa upande mmoja wa upendo,(wima) lakini wakipuuza uhusiano na wengine, ambao ni mwelekeo wa usawa. Kuhusiana na hilo, Kardinali Farell aliongeza kusema “Yesu anataja mitazamo mitatu inayotutenganisha na ndugu yetu: kumkasirikia, kumwita ‘mpumbavu’, kumwita ‘kichaa.’ Inahusisha, kama wengi daraja za maendeleo za hukumu: kumfukuza ndugu wa mtu kutoka kwako mwenyewe kwa hasira; kuzingatia mawazo yake ya thamani kidogo; kujidai kuingia ndani ya kilindi cha dhamiri yake, ukifikia hata kudharau uhusiano wake na Mungu, ukiuona kuwa wa uwongo, wa kijuujuu tu na unafiki”

Kardinali Farell akizungmza mbele ya Papa
Kardinali Farell akizungmza mbele ya Papa

Na, Kardinali Farrell kwa hiyo alisema.  “Yesu anatamka maneno haya alipokuwa akitoa maoni yake juu ya amri ya tano: “usiue na hivyo kuweka wazi kwamba “mtu anaweza “kumuua” ndugu yake ndani yake mwenyewe, yaani, si kimwili, bali kiroho.” Kumdharau jirani na kumhukumu bila kukata rufaa ni kukiuka amri ya tano, tayari ni “kuua” ndugu wa mtu ndani ya moyo wake. Hivyo mwaliko ni ule wa “kwenda zaidi ya haki ya Mafarisayo, wa kushinda utengano kati ya ibada ya Mungu na mahusiano na wengine.” Uwasilishaji huu ulipokelewa na wawakilishi zaidi ya mia mbili wa mashirika mia moja kati ya 117 ya kimataifa ya waamini, ya kibinafsi na ya umma, na mashirika mengine yenye hadhi ya  kisheria, ambayo Baraza la Kipapa la  Walei, Familia na Maisha lina uwezo wa moja kwa moja wa kusindikiza maisha na maendeleo yao.

Papa akizungumza katika mkutano huo
Papa akizungumza katika mkutano huo

Mwishoni mwa misa, washiriki wa mkutano walikutana katika Ukumbi mpya wa Sinodi na   Papa na baadaye kwa shughuli, iliyoletwa na  Kevin Kardinali Farrell. Baada ya salamu hasa Jumuiya ya Magnificat, muungano wa mwisho katika mpangilio wa matukio kupokea kutambuliwa kwa kipapa, Kardinali Farrell alionesha mada ya siku hiyo. “Changamoto ya sinodi kwa ajili ya utume akieleza zaidi ya yote kwamba Mtaguso mkuu hautekelezwi kwa kuwaingiza wanaume na wanawake walei, katika mahali pa mamlaka ya Kanisa, au kwa kuunda vyombo vipya vya kuonesha kwamba “wanahusika zaidi katika michakato ya kufanya maamuzi. Sio hata suala la kujaza na wao tupu wa parokia, majimbo, vyama na harakati. La sivyo  tungeishia kuwa kasisi walei, kama Papa anavyoonya mara nyingi. Sinodi, na ushirika unaohamasishwa katika Kanisa, lazima utumike, ili kutembea pamoja kweli kweli kwa walei na wachungaji, kwa karama na taasisi za kikanisa na kutafuta pamoja njia ambayo Roho anaonesha kuendeleza mbele, kwa msukumo mpya na  utume wa uinjilishaji wa Kanisa,” alihitimisha Kardinali  Farrell.

Walikuwa wapatao 200 wakuu wa vyama vya waamini vya kikanisa na harakati
Walikuwa wapatao 200 wakuu wa vyama vya waamini vya kikanisa na harakati
15 June 2024, 16:29