Stempu na Muhuri maalum wa Posta kwa uzalishaji kuhusu miaka 160 ya Msalaba Mwekundu Italia
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Katika kuadhimisho miaka 160 tangu kuanzishwa kwa chama cha Msalaba Mwekundu Italia, imetolewa toleo jipya la pamoja la Stempu na Muhuri maalum wa posta kwa uzalishaji kwa Vatican, Italia, Jamhuri ya Mtakatifu Marino na Shirika la Kijeshi la Malta ambapo kwa pamoja wanaadhimisha fursa hiyo ya shirika hili kubwa zaidi la kibinadamu duniani.
Asili ya Shirika la Msalaba Mwekundu
Asili ya Shirika la Msalaba Mwekundu ni kwa sababu ya mfadhili wa Uswiss na mjasiriamali Henry Dunant, ambaye kufuatia vita vya umwagaji damu vya Solferino mnamo 24 Juni 1859, alikasirishwa na ukosefu wa utunzaji uliotolewa kwa askari waliojeruhiwa waliotelekezwa kwenye uwanja wa vita, alikusanya wanaume na wanawake kutoa msaada wa maji, chakula na matunzo. Mpango huo ulihamasisha kuzaliwa kwa Harakati la Kimataifa la Msalaba Mwekundu.
Kufuatia Mkutano wa Geneva wa 1863, Jumuiya mbalimbali za kitaifa za Msalaba Mwekundu zilizaliwa, ikiwa ni pamoja na lile la Italia, lililoanzishwa huko Milano mnamo tarehe 15 Juni 1864 na Daktari Cesare Castiglioni kwa niaba ya “Kamati ya Chama cha Italia kwa ajili ya misaada ya waliojeruhiwa na wagonjwa katika vita.” Alama ya shirika, ni msalaba mwekundu kwenye msingi mweupe, ilichaguliwa mnamo 1864 kama heshima kwa Shirikisho la Uswiss, likibadilisha rangi za bendera yake. Katika miaka hii 160 ya historia ya Msalaba Mwekundu Italia imeunganishwa na historia ya Italia: “katika wakati mzuri, katika matukio makubwa, katika majanga ambayo yameathiri taifa lakini pia katika hali halisi ya ndani.” Mamilioni ya watu wanaojitolea na maelfu ya wafanyakazi hufanya kazi bila kuchoka, kila siku, kuleta misaada na usaidizi kwa maeneo yaliyoathiriwa na majanga ya mazingira, yaliyoharibiwa na migogoro, kuokoa na kupendelea wahamiaji, walio wa mwisho na walio hatarini zaidi, waaminifu kwa kauli mbiu popote kwa mtu yeyote”.
Tarehe 6 Aprili 2024, Baba Mtakatifu alikutana na waendeshaji na watu wa kujitolea wa Shirika la Msalaba Mwekundu Italia na kutoa shukrani zake kubwa kwao kwa kujitolea kwao mara kwa mara “kwa kuchochewa na kanuni za ubinadamu, kutopendelea, kutoegemea upande wowote na kujitolea [...] ishara inayoonekana kwamba udugu inawezekana. Haya ndiyo matakwa ya Baba Mtakatifu: “Msalaba Mwekundu daima kubaki kuwa ishara fasaha ya upendo kwa ndugu usio na mipaka, iwe kijiografia, kiutamaduni, kijamii, kiuchumi au kidini,”alisema Papa.