Tafakari ya wanawake watatu ilikuwa katikati ya kazi ya C9
Vatican News
Tafakari si juu ya wanawake tu bali pamoja na wanawake kuhusu nafasi yao katika Kanisa. Ni mada iliyoakisi tafakari ya Baraza la Makardinali washaru (C9) hasa Jumantatu tarehe 17 Juni 2024, katika siku ya kwanza kati ya siku mbili za kazi iliyomalizika tarehe 18 Juni, wakati mwanamke watawa na walei wawili waliingilia kati na mfululizo wa ripoti mbele ya Papa na Makadinali washauri C9.
Mtawa na profesa wawili
Kwa mujibu wa Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Vatican, katika taarifa iliyotolewa alasiri Juni 18, iliripoti kwamba waliozungumza tarehe 17 Juni ni Sr. Linda Pocher, FMA, profesa wa Taalimungu katika Kitivo cha Usaidizi cha Kipapa, ambaye alianzisha mada na akifuatiwa na Valentina Rotondi, profesa wa SUPSI huko Lugano na mtafiti katika Idara ya Sosholojia na Chuo Kikuu cha Nuffield Oxford na katika kituo cha NeuroMI cha Chuo Kikuu cha Bicocca cha Milano, na Donata Horak, profesa wa Sheria ya Kanoni, katika Mafunzo ya Kitaalimungu ya Alberoni huko Piacenza, inayohusishwa na Chuo Kikuu cha Kipapa cha Angelicum.
Hatua za wageni
Katika ripoti yake, tunasoma katika maelezo ya Ofisi ya Vyombo vya habari kuwa “, Profesa Rotondi alionesha maono ya uchumi kama utunzaji na usimamizi mzuri katika muktadha wa uhusiano wa kina kati ya vizazi, wakati kwa upande wake Donata Horak aliakisi pingamizi kadhaa, kama vile haki na haki ya huruma yenye uwezo wa mashauriano na uwezo wa kimaadili, kanuni ya daraja la juu na kikanisa, ushirika, demokrasia na kielelezo cha kifalme, katika muktadha wa kutafakari kwa mapana juu ya Sheria ya Kanoni.
Ambongo: kuna akina mama Kanisani wa kustahiki
Uingiliaji kati huo pia uliibua mazingatio kutoka kwa makadinali waliohudhuria na wawili kati yao, mwishoni mwa C9, walitaka kuakisi vyombo vya habari vya Vatican baadhi ya vipengele vilivyojitokeza kwenye mada wakati wa Mkutano huo. Kardinali Fridolin Ambongo Besungu, Askofu Mkuu wa Jimbo la Kinshasa alisema kwamba tarehe 17 Juni ilikuwa ni mara ya nne ya majadiliano kuhusu nafasi ya mwanamke katika Kanisa. “Hapa makanisani zaidi ya nusu ya watu wanaoshiriki katika sherehe hizo ni wanawake, lakini tunapoona majukumu waliyonayo ni wachache,” Alisema. Baada ya mikutano yote hii, alisema, imekuwa “wazi kwetu kwamba majukumu haya lazima kukua lakini si kwa maana ya kijeshi lakini kwa sababu tu, kama Papa alivyosema, “Kanisa ni mwanamke” na kuna umama ambao lazima uthaminiwe katika jumuiya ya kikanisa.
Gracias: Uongozi wa kike una fursa nyingi za maendeleo
Kardinali Oswald Gracias, Askofu mkuu wa mji mkuu wa Bombay nchini India, alikubaliana juu ya umuhimu wa jukumu ambalo lazima liongezwe. “Ninatoka India na katika maeneo mengine wanawake hawathaminiwei, wao ni 'daraja la pili', na kwa sababu hiyo Kanisa linafanya kazi kuwapa nafasi sahihi katika familia, katika jamii, katika siasa.” Idha kwa kuongeza alisema “Katika Kanisa, katika Sheria ya Kanuni yenyewe "kuna uwezekano mkubwa" kwa wasifu wa uongozi wa kike katika Kanisa na uzoefu wangu umenionesha "mara nyingi" kwamba wanawake waliweza kushughulikia masuala kwa "mtazamo ambao wanaume hawakuwa nao. kuzingatiwa". Na nina "tumaini kubwa" kwamba haya yote yatakua.
Pia katika C9 ni ulinzi wa watoto na migogoro duniani
Kwa hiyo siku mbili 17 na 18 Juni zilifanyika kazi ya Makardinali washauri wa Papa (C9) na ripoti ya Kadinali O'Malley wakfu, ilieleza maelezo kutoka Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Vatican, kwa mitazamo iliyofunguliwa na kazi ya Tume kwa ajili ya Ulinzi wa watoto wadogo katika kulinda mambo” na Kadinali Gracias mwenyewe, ambaye alichunguza "shughuli na njia ya uendeshaji wa mikutano ya maaskofu". mizozo ikiendelea." Kikao kijacho cha Baraza kitafanyika mwezi Desemba 2024.