Tafuta

2024.06.17 Kitabu kuhusu Michezo ya Amani kikiwa na dibaji ya Papa Francisko. 2024.06.17 Kitabu kuhusu Michezo ya Amani kikiwa na dibaji ya Papa Francisko. 

Dibaji ya Papa ya katika Kitabu kuhusu"Michezo ya amani.Roho ya Olimpiki!

“Katika wakati mgumu wa kihistoria tunaoshuhudia,Michezo ya Olimpiki na Michezo ya Walemavu huko Paris ni fursa ya amani.Nikikumbuka thamani ya makubaliano ya Olimpiki - yaliyopendekezwa na Umoja wa Mataifa - matumaini yangu kwamba michezo inaweza kujenga madaraja, kuvunja vizuizi,kukuza uhusiano wa amani.”Ni maneno yaliyomo katika dibaji ya Papa Francisko katika kitabu: "Michezo ya Amani.Roho ya Olimpiki na ya Michezo ya walemavu.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Katika maneno ya  Papa Francisko kkwenye dibaji yake juu ya  Kitabu chenye kichwa: “Michezo ya AmanimRoho ya Olimpiki na Paralimpiki”  ameandika kuwa:  “Katika wakati mgumu wa kihistoria tunaoshuhudia, Michezo ya Olimpiki na Michezo ya Walemavu huko Paris ni fursa ya amani. Nikikumbuka thamani ya makubaliano ya Olimpiki - yaliyopendekezwa na Umoja wa Mataifa - matumaini yangu ni kwamba michezo inaweza kujenga madaraja, kuvunja vizuizi, kukuza uhusiano wa amani.” Kwa njia hiyo katika dibaji ya kitabu hicho, kitakachoanza kutumika tarehe 18 Juni 2024  kwenye maduka ya vitabu ya Vatican (LEV), Papa Francisko anakumbuka kwamba:  “roho halisi ya Olimpiki na Paralimpiki ni dawa ya kuepuka kuanguka katika janga la vita na kujikomboa kwa kukomesha vurugu.”

Ulinzi na Usalama wa boti za polisi katika mto wa Seine mahali pa michezo ya olimpiki
Ulinzi na Usalama wa boti za polisi katika mto wa Seine mahali pa michezo ya olimpiki

Anaye muunga mkono Papa Francisko katika pendekezo la kutambua Olimpiki na Michezo ya Olimpiki ya Walemavu kama njia ya amani ni, kwa wahusika  85, kuanzia na: mamlaka ya juu zaidi ya michezo, wanariadha wa jana na leo ambao wameishi na wataishi uzoefu wa Olimpiki na Paralimpiki katika viwango vya juu. Miongoni mwao, sauti za mashuhuda wa matumaini ambao ni sehemu ya timu ya wakimbizi ni kama vile mwendesha baiskeli wa Afghanistan Masomah Ali Zada, mkuu wa ujumbe katika Michezo ya Olimpiki ya Paris 2024, ambaye alisisitiza umuhimu wa michezo kama ujumbe: “Kwa mwanamke, baiskeli nchini Afghanistan haizingatiwi kuwa kawaida: tunaweza hata kusema kuwa ni marufuku. Lakini ushiriki wangu katika Michezo ulionesha kuwa mchezo ni wa kila mtu, kwa sababu ni ishara ya usawa na uhuru.”

Katika  kurasa za kitabu hicho pia kuna historia ya mwanariadha wa Siria wa Timu ya Wakimbizi wa Paralympic(Michezo ya walemavu), mwenye kushika nafasi ya juu katika Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ya Rio de Janeiro 2016, ambaye ni Ibrahim Al Hussein alisema: “Mchezo  ilikuwa mpatanishi, lugha ya kawaida iliyofanya, maisha yangu ya pili kuwezekana.” Kwa njia hiyo katika dibaji ya Papa alifafanua kuwa “ shuhuda hizi kama historia  za shauku za kibinadamu za ukombozi na udugu, sadaka na uaminifu, roho ya timu na ushirikishwaji. Michezo ya Olimpiki na Michezo ya Olimpiki ya Walemavu pia ni fursa ya kukumbatia historia za wanawake na wanaume ambao wanaishi uzoefu tofauti wa kibinadamu, kiutamaduni na kidini,” aliandika Papa Francisko. Kwa mtindo huu wa udugu wa kimichezo, kitabu cha Mchezo ni amani kinajionesha kama mwongozo, ambao kila mtu anaweza kufikia ili kupata uzoefu - hata katika maisha ya kila siku - nafsi, roho, maadili na kiini cha Olimpiki na Paralimpiki.”

Mazoezi ya kuongelea wachezaji
Mazoezi ya kuongelea wachezaji

Kitabu hicho kinawasilishwa mjini Roma Jumatatu tarehe 17 Juni  2024 saa 11.00 jioni katika Uwanja wa Olimpiki, kwa kushirikisha wanariadha wa Olimpiki na Walemavu na Timu ya Wakimbizi ambao watashirikisha ushuhuda wao . Miongozi mwa washiriki ni   Kadinali José Tolentino de Mendonça, Mwenyeketi wa Baraza la kipapa la  Baraza la Utamaduni na Elimu, Andrea Abodi, Waziri wa Serikali ya Italia wa Michezo na Vijana; Marco Mezzaroma, Rais wa Michezo na Afya; Luca Pancalli, Rais wa Kamati ya Walemavu ya Italia; Silvia Salis, Naibu Makamu wa Rais wa Kamati ya Olimpiki ya Italia (CONI). Mkutano huo utasimamiwa na Alessandro Gisotti, naibu mkurugenzi wa wahariri wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano.

Ikumbukwe kitabu cha Michezo ni amani. Roho ya Olimpiki na Paralimpiki kimechapishwa na Duka Vitabu ka Vatican LEV, na  kina kurasa 192, na kitauzwa euro 17, na kuhaririwa na Vincenzo Parrinello, katika mkesha wa Ufunguzi wa  majira ya kiangazi ya michezo huko  Jijini Paris nchini Ufarasa.

Dibaji ya Kitabu katika michezo ya Olimpiki
17 June 2024, 15:53