Vijana katika safari kwa Ujasiri na Matumaini
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Katika Makao makuu ya Ubalozi wa Ureno unaowakilisha Vatican, tarehe 19 Juni 2024 litafanyika tamasha la muziki, usiku lililoandaliwa na Taasisi ya Yohane Paulo II la Vijana, ambacho ni chombo muhimu cha Baraza la Kipapa la Walei Familia na Maisha ambalo kwa zaidi ya miaka thelathini limesaidia kuandaa Siku za Vijana Duniani na shughuli za Ofisi ya Vijana ya Jimbo. Tukio hilo lilitokana na matumaini ya Halmashauri ya Wakurugenzi kufuatilia mkutano uliofanyika Oktoba 2022 jiji ni Vatican, wakati wa maandalizi ya kuelekea Siku ya Viajana (WYD)huko Lisbon 2023(:https://www.fondazionegiovani.va/2022/10/).
Katika mkutano huu wa pili, utakaosimamiwa na mtangazaji wa Kipindi cha ‘A Sua Immagine’ (katika Televisheni ya Baraza la Maaskofu Italia),Lorena Bianchetti, Mfuko huo unalenga kutafakari pamoja na wafuasi na marafiki walioalikwa, juu ya nini kinaweza kufanywa kwa dhati na kwa pamoja, ili kukuza uchungaji wa Vijana wa Kikatoliki ulimwenguni na kuunga mkono mipango ambayo inalenga kuhusisha vijana katika mipango madhubuti, katika nyanja zao za masomo na kazi, kwa jicho kuelekea Siku ya Vijana Duniani (WYD) ijayo huko Seoul 2027.
“Kutoa heshima kwa ahadi yetu ya kusaidia vijana na Siku za Vijana Duniani, kufungua jioni tulitaka wasanii wawili vijana kutoka Bendi ya Vijana Ulimwenguni kucheza kipande kutoka utamaduni wa muziki wa Ureno (kukumbuka Lisbon 2023), kipande kutoka kwa kazi ya Italia (kwa heshima ya Jubilei ya Vijana 2025) na ile ya kiutamaduni ya kipande cha Kikorea (WYD huko Seoul 2027)”, alisema Rais wa Mfuko huo, wa Vijana, mwanasheria Daniele Bruno.
Ratiba ya hafla hiyo iliwezekana shukrani kwa ukarimu wa fadhili wa Mheshimiwa Domingos Teixeira de Abreu Fezas Vital, Balozi wa Ureno anayewakilisha nchi yake Vatican na Shirika la Kijeshi la Malta, pia ni pamoja na uwasilishaji wa jarida lililochapishwa na Mfuko huo wa Siku ya Vijana Ulimwenguni ambalo limesasishwa kwa muundo na yaliyomo na ya Mijadala ya Mkutano wa Utunzaji wa kazi Uumbaji, ambao ulifanyika wakati wa siku ya vijana Duninia (WYD) ya 2023 huko Lisbon. (https://www.fondazionegiovani.va/2023/08/).
Kwa kuhitimisha jioni hiyo, kutakuwa ni uingiliaji wa muziki wa Giovanni Caccamo, mwimbaji na mtunzi wa nyimbo wa Italia, anayetambuliwa kimataifa, ambaye atawasilisha mradi wake wa Parola kwa vijana, uliooneshwa katika kumbi mbalimbali za kitaasisi, pamoja na Seneti ya Jamhuri ya Italia na pia Ikulu ya Umoja wa Mataifa huko, New York, Marekani, katika toleo lake la kimataifa lenye jina la Maonyesho ya mabadiliko ya Vijana na ya baadaye. Ni shindano la mawazo, linalolenga vijana kutoka ulimwenguni kote ili kuunda ilani ya kiutamaduni ya mabadiliko, juu ya mada kama vile amani, ushirikishwaji na maendeleo endelevu.