Tafuta

Askofu mkuu Christophe Zakhia El-Kassis Balozi wa Vatican nchini Yemen na mwakilishi wa Vatican wa Kitume kwenye Visiwa vya Kiarabu. Askofu mkuu Christophe Zakhia El-Kassis Balozi wa Vatican nchini Yemen na mwakilishi wa Vatican wa Kitume kwenye Visiwa vya Kiarabu. 

Askofu mkuu Christophe Zakhia El Kassis Balozi wa Vatican Yemen na Visiwa vya Kiarabu

Askofu mkuu Christophe Zakhia El Kassis alizaliwa tarehe 24 Agosti 1968 hukoLebanon. Tarehe 21 Mei 1994 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre na kuwa ni sehemu ya Kanisa la Wamoriniti wa Beirut. Alijiendeleza na hatimaye, kufaulu kutunukiwa shahada ya uzamivu katika Sheria na Taratibu za uendeshaji wa kesi mahakamani! Wakati wa maadhimisho ya Jubilei kuu ya Miaka 2000 ya Ukristo, tarehe 19 Juni, akaanza utume wake katika masuala ya diplomasia ya Kanisa.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amemteuwa Askofu mkuu Christophe Zakhia El Kassis kuwa ni Balozi mpya wa Vatican nchini Yemen pamoja na kuwa ni Mwakilishi wa Vatican kwenye Visiwa vya Kiarabu. Askofu mkuu Christophe Zakhia El Kassis anaendelea kuwa ni Balozi wa Vatican kwenye Umoja wa Falme za Kiarabu. Itakumbukwa kwamba Askofu mkuu Christophe Zakhia El Kassis alizaliwa tarehe 24 Agosti 1968 huko Beirut, nchini Lebanon. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikuhani, tarehe 21 Mei 1994 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre na kuwa ni sehemu ya Kanisa la Wamoriniti wa Beirut. Alijiendeleza na hatimaye, kufaulu kutunukiwa shahada ya uzamivu katika Sheria na Taratibu za uendeshaji wa kesi mahakamani! Wakati wa maadhimisho ya Jubilei kuu ya Miaka 2000 ya Ukristo, tarehe 19 Juni, akaanza utume wake katika masuala ya diplomasia ya Kanisa.

Yemen ni nchi ambayo imearhirika sana kwa vita
Yemen ni nchi ambayo imearhirika sana kwa vita

Tangu wakati huo, akabahatika kutekeleza dhamana na utume wake kwenye Balozi za Vatican nchini Indonesia, Sudan, Uturuki na baadaye katika kitengo cha mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa mjini Vatican. Baba Mtakatifu Francisko tarehe 24 Novemba 2018 akamteuwa kuwa Balozi wa Vatican nchini Pakistan na kumpandisha hadhi ya kuwa ni Askofu mkuu na hatimaye, akawekwa wakfu kuwa Askofu mkuu tarehe 19 Januari 2019 na Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican. Tarehe 22 Julai 2024, Baba Mtakatifu Francisko akamteua kuwa ni Balozi wa Vatican nchini Yemen pamoja na Visiwa vya Uarabuni.  Ni bingwa aliyebobea katika lugha ya: Kiarabu, Kifaransa, Kiitalia, Kiindonesia, Kihispania na Kijerumani, matendo makuu ya Mungu, zawadi ya Roho Mtakatifu kwa waja wake!

Balozi Yemen
23 July 2024, 15:14