Tafuta

Cookie Policy
The portal Vatican News uses technical or similar cookies to make navigation easier and guarantee the use of the services. Furthermore, technical and analysis cookies from third parties may be used. If you want to know more click here. By closing this banner you consent to the use of cookies.
I AGREE
Gigue
Ratiba Podcast
Askofu mkuu Gábor Pintér ameteuliwa kuwa ni Balozi mpya wa Vatican nchini New Zealand. Askofu mkuu Gábor Pintér ameteuliwa kuwa ni Balozi mpya wa Vatican nchini New Zealand.  (ANSA)

Askofu mkuu Gábor Pintér Balozi mpya wa Vatican nchini New Zealand

Askofu mkuu Gábor Pintér alizaliwa tarehe 9 Machi 1964 huko Kunszentmárton, nchini Hungaria. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 11 Juni 1988 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Tarehe Mosi, Juni 1996 akajiunga na diplomasia ya Kanisa na hivyo kutumwa nchini Haiti, Bolivia, Sweden, Ufaransa, Ufilippini na Austria. Tarehe 13 Mei 2016 akateuliwa kuwa ni Askofu mkuu na kuwekwa wakfu 15 Januari 2016 na Kardinali Pietro Parolin Katibu mkuu wa Vatican.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko tarehe 27 Julai 2024 amemteua Askofu mkuu Gábor Pintér kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini New Zealand na kabla ya uteuzi huu, Askofu mkuu Gábor Pintér alikuwa ni Balozi wa Vatican nchini Honduras. Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu Gábor Pintér alizaliwa tarehe 9 Machi 1964 huko Kunszentmárton, nchini Hungaria. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 11 Juni 1988 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Tarehe Mosi, Juni 1996 akajiunga na diplomasia ya Kanisa na hivyo kutumwa nchini Haiti, Bolivia, Sweden, Ufaransa, Ufilippini na Austria.

Askofu mkuu Gabor Pinter Balozi wa Vatican nchini New Zealand
Askofu mkuu Gabor Pinter Balozi wa Vatican nchini New Zealand

Tarehe 13 Mei 2016 Baba Mtakatifu Francisko akamteuwa kuwa Balozi wa Vatican nchini Belarus na hivyo kumpandisha hadhi na kuwa ni Askofu mkuu na hatimaye, akawekwa wakfu tarehe 15 Julai 2016 na Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican. Tarehe 12 Novemba 2019 Baba Mtakatifu Francisko akamteuwa kuwa Balozi wa Vatican nchini Honduras. Na ilipogota tarehe 27 Julai 2024, Baba Mtakatifu akamteuwa kuwa Balozi wa Vatican nchini New Zealand.

Uteuzi New Zealand
28 Julai 2024, 15:14
Prev
February 2025
SuMoTuWeThFrSa
      1
2345678
9101112131415
16171819202122
232425262728 
Next
March 2025
SuMoTuWeThFrSa
      1
2345678
9101112131415
16171819202122
23242526272829
3031