Askofu Mkuu Jacques Assanvo Ahiwa Jimbo kuu la Bouaké, Pwani ya Pembe
Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko tarehe 25 Julai 2024 amemteuwa Askofu Jacques Assanvo Ahiwa kuwa Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Bouaké, Pwani ya Pembe “Côte d’Ivoire.” Kabla ya uteuzi huu, Askofu mkuu Jacques Assanvo Ahiwa alikuwa ni Askofu Msaidizi wa Jimbo kuu la Bouaké. Askofu mkuu mteule Jacques Assanvo Ahiwa alizaliwa tarehe 6 Januari 1969 huko Jimbo kuu la Abidjani, Pwani ya Pembe. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi tarehe 13 Desemba 1997 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre kwa ajili ya Jimbo Katoliki la Grand-Bassam.
Baba Mtakatifu Francisko tarehe 5 Mei 2020 akamteuwa kuwa Askofu Msaidizi wa Jimbo kuu la Bouaké, Pwani ya Pembe na hatimaye, akawekwa wakfu kuwa Askofu msaidizi wa Jimbo kuu la Bouaké. Tarehe 16 Februari 2024, Baba Mtakatifu Francisko akamteuwa kuwa Msimamizi wa Kitume wa Jimbo kuu la Bouaké. Na ilipogota tarehe 25 Julai 2024, Baba Mtakatifu Francisko akamteuwa kuwa kuwa Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Bouaké, Pwani ya Pembe “Côte d’Ivoire.” Anatarajiwa kusimikwa rasmi tarehe 14 Septemba 2024.