Baba Mtakatifu Francisko tarehe 9 Julai 2024 amemteuwa Askofu mkuu Mark Gerard Miles, kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Costa Rica. Baba Mtakatifu Francisko tarehe 9 Julai 2024 amemteuwa Askofu mkuu Mark Gerard Miles, kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Costa Rica.  

Askofu Mkuu Mark G. Miles Balozi Mpya wa Vatican nchini Costa Rica

Askofu mkuu Mark Gerard Miles alizaliwa tarehe 13 Mei 1967 huko Gibralta, nchini Uingereza. Historia inaonesha kwamba, Askofu mkuu Mark Gerard Miles amekuwa ni Balozi na Askofu mkuu wa kwanza kutoka katika eneo hili la Gibralta. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 14 Septemba 1996 akapewa daraja Takatifu ya Upadre. Hii ilikuwa ni Sikukuu ya Kutukuka kwa Fumbo la Msalaba, chombo cha ufunuo wa huruma na upendo wa Mungu!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko tarehe 9 Julai 2024 amemteuwa Askofu mkuu Mark Gerard Miles, kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Costa Rica. Kabla ya uteuzi huu Askofu mkuu Mark Gerard Miles alikuwa ni Balozi wa Vatican nchini Benin na Togo. Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu Mark Gerard Miles alizaliwa tarehe 13 Mei 1967 huko Gibralta, nchini Uingereza. Historia inaonesha kwamba, Askofu mkuu Mark Gerard Miles amekuwa ni Balozi na Askofu mkuu wa kwanza kutoka katika eneo hili la Gibralta. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 14 Septemba 1996 akapewa daraja Takatifu ya Upadre. Hii ilikuwa ni Sikukuu ya Kutukuka kwa Fumbo la Msalaba, chombo cha ufunuo wa huruma na upendo wa Mungu! Ni ishara ya neema, sala, msamaha, upatanisho na matumaini. Ni kutokana na maana hii mpya, Mama Kanisa anaona fahari kuu kuimba sifa kuu za Msalaba wa Bwana wetu Yesu Kristo. Msalaba unaendelea kumfunza mwamini kwamba, hakuna mapendo kamili yasiyokuwa na mateso na matumaini ya uzima wa milele.

Costa Rica ni Washabiki sana wa Soka
Costa Rica ni Washabiki sana wa Soka

Baada ya Mwaka 1996 Askofu mkuu Mark Gerard Miles alianza maandalizi ya kujiunga na Taasisi ya Kipapa ya Diplomasia ya Kanisa na hatimaye, akajipatia Shahada ya Uzamivu katika Sheria za Kanisa. Katika maisha na utume wake wa Kidiplomasia, alipangiwa huko Equador, Hungaria na Vatican katika Idara ya masuala ya jumla kwenye Sekretarieti kuu ya Vatican. Wakati wa hija ya Kitume ya Baba Mtakatifu Francisko nchini Ufilippin na Umoja wa Mataifa kunako mwaka 2015, ndiye aliyekuwa anatafsiri hotuba za Baba Mtakatifu mubashara, kutoka katika lugha ya Kihispania kwenda katika lugha ya Kiingereza, kiasi cha kuwaacha wasikilizaji wengi wakiwa wameshika tama kutokana na umahiri wake! Tarehe 31 Agosti 2019 Baba Mtakatifu Francisko akamteuwa kuwa Mwakilishi wa Kudumu wa Vatican kwenye Nchi za Amerika “Organization of American States, OAS.” Na hatimaye, tarehe 5 Februari 2021, Baba Mtakatifu Francisko akamteuwa kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Benin na tarehe 2 Machi 2021 akamteuwa kuwa Balozi wa Vatican nchini Togo na kumpandisha hadhi kuwa Askofu mkuu na hatimaye, kuwekwa wakfu tarehe 25 Aprili 2021 na Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican.

Uteuzi Costa Rica

 

11 July 2024, 14:36