Balozi wa Vatican nchini Nigeria na São Tomé na Príncipe
Baba Mtakatifu Francisko Julai 15,2024 amemteua Balozi wa Vatican nchini Nigeria,Askofu Mkuu Michael Francis Crotty na Julai 14,alimteua Balozi wa Vatican Nchini São Tomé na Príncipe,Askofu Mkuu Kryspin Dubiel ambaye hadi uteuzi ni Balozi wa Vatican pia nchini Angola.
Vatican News
Jumanne tarehe 16 Jula 2024, Baba Mtakatifu Francisko amemteua Balozi wa Vatican Ncnini Nigeria, Askofu Mkuu Michael Francis Crotty, wa Kanisa la Lindisfarna, ambaye hadi uteuzi huo alikuwa ni Balozi wa Vatican Nchini Burkina Faso na Niger.
Balozi wa Vatican Nchini São Tomé na Príncipe
Baba Mtakatifu Francisko aidha, Jumatatu tarehe 15 Julai 2024, Baba Mtakatifu Francisko alimteua Balozi wa Vaticvan nchini São Tomé na Príncipe, Askofu Mkuu Kryspin Dubiel, wa Kanisa la Vannida, ambaye hadi uteuzi huo ni Balozi wa Vatican pia Nchini Angola.
16 July 2024, 16:41