Tafuta

2024.07.16 Mama Maria wa Mwamba huko Calabria 2024.07.16 Mama Maria wa Mwamba huko Calabria   (Copyright © 2024 Nostra Signora dello Scoglio. Powered by Fondazione Madonna dello Scoglio)

Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa kuhusu Mama Yetu wa Mwamba

Kulingana na sheria mpya,Baraza limeweka hadharani uamuzi chanya unaohusiana na matunda ya kiroho kufuatia matukio yaliyofafanuliwa na mtokewa Cosimo Fragomeni,huko Calabria.Askofu wa Jimbo anahimizwa kuthamini thamani ya kichungaji na kuendeleza uenezaji wa pendekezo la kiroho na sala.

Vatican News

“Katika ulimwengu tunamoishi, ambamo watu wengi sana hutumia muda wa maisha yao bila kurejea kupita kiasi, mahujaji wanaokaribia Hekalu la Mwamba ni ishara yenye nguvu ya imani,” aliandika Kardinali Victor Manuel Fernández, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa wakati akijibu swali kutoka kwa Askofu Francesco Oliva wa Jimbo la Locri-Gerace, katika Barua ya tarehe 3 Juni 2024  kuwa “inathibitisha kizuizi cha Nihil” kilichopendekezwa na Padre kuhusu matukio yanayozunguka kuhusu Madhabahu ya Jimbo  ya Mama Yetu wa Mwamba (Madonna dello Scoglio") huko Mtakatifu Domenica ya Placanica, Calabria nchini Italia

Utambuzi wa uzoefu wa Roho

Ilikuwa mnamo  tarehe 11 Mei 1968, ambapo inasemekana kuwa Bikira Maria  alionekana kwa mara ya kwanza na Cosimo Fragomeni, mkulima mnyenyekevu mwenye umri wa miaka 18. Kulingana na Kanuni mpya iliyochapishwa na Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa ya tarehe 17 Mei iliyopita iliyokumbushwa na Kardinali Fernández, katika barua yake (nihil obstat) kuwa “haipaswi kueleweka kama idhini ya tabia isiyo ya kawaida ya jambo hilo”  badala yake kama utambuzi wa uzoefu wa kiroho uliopendekezwa mahali patakatifu. Kwa hiyo, Askofu wa jimbo anahimizwa kuthamini thamani ya kichungaji na kuendeleza uenezaji wa pendekezo hili la kiroho, ikiwa ni pamoja na hija, mikusanyiko na mikutano ya maombi, huku waamini wakipewa mamlaka ya kushikilia matukio haya kwa busara.”

Mahali pa kukutana na huruma za Mungu

Kulingana na Cosimo, aliyetokewa kwa tokeo la kwanza mnamo 1968, ni kwamba ulitangulia mwanga kutoka katika mwamba wa mchanga uliokuwa karibu na nyumba ya kijana huyo, ambao ulirudiwa kwa siku nne zilizofuata. Katika jumbe zilizoripotiwa na Cosimo, Mwenyeheri Bikira alitoa wito kwa ajili ya uongofu na sala, huku akionesha hamu ya kuona eneo la Calabria likigeuzwa kuwa kituo kikuu cha kiroho ambapo watu wangeweza kukutana na huruma ya Mungu. Cosimo alisafisha eneo lililokuwa karibu na mwamba, akatengeneza tuta na kuchimba mchanga kutengeneza sehemu ya kuweka sanamu ya marumaru ya Maria, iliyonunuliwa huko Carrara, (sehemu moja ya matengenezo ya sanamu za marumaru).

Kutoka katika Kanisa rahisi hadi madhabahu ya jimbo

Na mapema eneo hilo likawa mahali pa mahujaji kutoka Italia yote na hata nje ya nchi. Mwanzoni, palikuwa na Kikanisa kidogo, lakini kutokana na ongezeko la mahujaji lilichochea ujenzi wa madhabahu kubwa. Wakati huohuo, mnamo mwaka wa 1987, Cosimo akawa Mfranskani wa utawa wa Tatu(Franciscan tertiary). Tarehe 7 Desemba 2008, Askofu Giuseppe Fiorini Morosini wa wakati huo wa Locri-Gerace, aliamuru kwamba ukweli wa ibada ya Mama wa Mwamba uwekwe chini ya uangalizi wa kichungaji wa Askofu wa jimbo. Kunako tarehe 22 Mei 2013, wakati wa Katekesi ya Papa  Francisko katika Uwanja wa Mtakatifu Petro, mjini Vatican Ndugu Cosimo akifuatana na Askofu Morosini, alimwomba Baba Mtakatifu Francisko kubariki jiwe la msingi la Madhabahu ya “Scoglio" yaani "mwamba” iiliyokuwa inaendelea kujengwa. Miaka mitatu baadaye, tarehe 11 Februari 2016, Askofu mpya Francesco Oliva, wa Locri-Gerace, alipandisha hadhi ya mahali pa ibada kuwa Madhabahu ya Jimbo kwa kuliweka  jina la “Mama Yetu wa Mwamba.” Mwaka uliofuata, mnamo  tarehe 10 Julai 2017, alikabidhi uchungaji wake kwa Wamisionari wa Uinjilishaji.

Matunda dhahiri ya maisha ya Kikristo

Katika barua yake, Kardinali Fernandez anakazia kusema jinsi  ambavyo madhabahu “imevutia watu wengine wengi waamini kutoka malezi mbalimbali, hasa wale wanaoteseka na wagonjwa.” Alibainisha kwamba, “Kwa miaka mingi, mahali hapo pamezidi kuvutia mahudhurio ya wacha Mungu na mahujaji chini ya usimamizi wa Mkuu wa Kawaida ambao umesababisha shughuli kubwa ya kiroho ya sala na kusikiliza.” Kardinali Fernandez aliendelea kunukuu maneno ya Askofu Oliva, aliyeandika: “Matunda ya maisha ya Kikristo kwa wale wanaotembelea Mwamba [yaani, mahali patakatifu] yanaonekana, kama vile kuwepo kwa roho ya sala, uongofu, miito fulani, kwa ukuhani na maisha ya kitawa, ushuhuda wa upendo, pamoja na ibada yenye afya, na matunda mengine ya kiroho. Wakati wote huo, hakuna mambo hatari ambayo yametokea, wala matatizo ya uvutano dhahiri.

Ombi la Askofu Oliva

Katika barua iliyotumwa mwezi Juni, 2024 katika Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa, Askofu Oliva alikuwa amependekeza nihil obstat kama “utambuzi unaohitajika kuendelea kufanya kazi kwa njia ambayo wale wanaotembelea [Mahali Patakatifu] wapate kufarijiwa na kutiwa moyo na kuendelea, wakijua kwamba wako katika ushirika na Kanisa Katoliki.” Katika jibu lake, Kardinali Fernandez, anaandika, “Katika suala hili, Baraza hili linazingatia ripoti yenu chanya juu ya wema wa kiroho unaotendeka katika (Mahali Patakatifu), ambayo mnaiweka mtazamo daima ili kusiwe na udanganyifu wowote wa watu, faida ya kifedha isivyo stahili, au makosa mazito ya kimafundisho ambayo yanaweza kusababisha kashfa, kuwadhuru waamini, au kudhoofisha sifa ya Kanisa.”

Fernandez:Kuheshimiwa Maria katika mtazamo wazi wa kikristo

Kardinali aidha alikumbuka kwamba “heshima ifaayo kwa Maria, Mama ya Yesu, Mama wa Kanisa, na Mama yetu, lazima ioneshwe kwa njia ya kutohusisha namna zisizofaa za staha na matumizi ya vyeo vya Maria visivyofaa. Badala yake, kufanyiwa ibada kwa mtazamo wazi wa Kikristo ni muafaka, kama vile Katiba ya Kitume inavyofundisha: ‘Mama anapoheshimiwa, Mwana (...) anajulikana kwa haki, anapendwa na kutukuzwa’ (Lumen gentium, 66).Kuwepo kwa mahujaji mbele ya Bikira, ambao kwao wanakuwa kielelezo cha wazi cha huruma ya Bwana, ni njia ya kukiri kutotosheka kwao katika kutekeleza kazi ya maisha na hitaji lao la bidii na na juhudi ya  maisha, hamu kwa Mungu. Katika muktadha wa thamani kama huu wa imani, tangazo lililofanywa upya la kerygma linaweza kuendelea kuelimisha na kuimarisha uzoefu huu wa Roho,"alihitimisha Kardinali.

Waamini wanayo mamlaka ya kijitoa kwa namna ya busara

Wakati uleule wa kuchapishwa kwa barua ya Baraza la Kipapa, na agizo la Askofu wa Locri-Gerace lilitolewa, ambalo lilianzisha 'nulla osta'-'ruhusa' “kwa ajili ya thamani ya kichungaji ya pendekezo hilo la kiroho na pia kuenezwa kwake, kutia ndani kupitia safari zinazowezekana, mikusanyiko, na mikutano ya maombi.” Waamini ‘wana mamlaka ya kujitoa’ kwa namna ya busara, katika ibada yao kama ilivyoelekezwa awali. Hii, hata hivyo, haimaanishi tamko la tabia isiyo ya kawaida ya jambo hilo, na waaminifu hawalazimiki kuliamini. Ujumbe wowote zaidi kutoka kwa wale wanaohusika utawekwa wazi baada ya hukumu ya Askofu. Wakati huo huo, Askofu Oliva anaendelea kuwaalika waamini kuhudhuria sherehe takatifu iliyopangwa kwenye hekalu mnamo alasiri ya tarehe 5 Agosti 2024.

Bikira Maria wa Mwamba huko Calabria Italia

 

16 July 2024, 17:10