Ask.Mkuu Gallgher,Ufilippini:kwa pamoja kukuza amani kwa majadiliano
Vatican News.
Rais wa Jamhuri ya Ufilippini, Bwana Ferdinand R. Marcos Jr., mkatoliki alikutana na kusalimiana na Askofu Mkuu Paulo Richardh Gallagher, Katibu wa Vatican wa mahusiano na Nchi na Mashirika ya Kimaifa alipotembelea Ikulu huko Malacañang, jijini Manila, Rais huyo wakati wa mazungumzo alisema: “Sisi sio tu nchi ya Kikatoliki, lakini nchi ya Kikatoliki sana. Tumeendelea kufanya kazi kwa ukaribu na Vatican kwa miaka mingi sana hadi sasa.
Katika ziara ya Askofu Mkuu Gallagher nchini Ufilippini tangu tarehe 1 Julai anatarajia kuwapi katika Nchi ya Kusini Mashariki wa bara la Asia hadi tarehe 5 Julai 2024. Mkutano wao ulitangazwa na Sekretarieti ya Vatican katika Account yao ya X @TerzaLoggia. Kabla ya ziara kwa Rais Marcos, mwakilishi wa Vatican alikutana pia asubuhi ya tarehe 1 Julai na Katibu wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Ufilipino Bwana, Enrique Manalo. Kwa pamoja walijadili masuala ya kawaida yanayohusu Ufilippino na Vatican.
Katika mazungumzo hayo Manalo alisema: “Ufilipino inaendelea na daima itaendelea kuunga mkono utaratibu wa kimataifa unaozingatia sheria. Tunatambua mchango wa Vatican katika kukuza amani, haki za binadamu na ushirikiano wa maendeleo duniani kote.” Kwa upande wa Askofu Mkuu Gallagher alikumbuka kwamba, Vatican inao uhusiano na nchi ya Kusini-Mashariki mwa Asia, “kutokana na mchango mkubwa sana ambao Wafilippini, kama Wakatoliki, ulimwenguni kote, kwa ustawi wa Kanisa Katoliki na wengi wa jamii zetu wanao utoa. Kwa kuongeza alisema “Wakatoliki wa Ufilipini ni wakala bora wa uinjilishaji na kuhubiri Habari Njema ya Injili.” Na alihitimisha kwa kukumbuka vipaumbele vya Vatican kwa wakati huu kuwa “ni dhahiri migogoro mingi sana ulimwenguni leo, na hitaji la kukuza amani kupitia mazungumzo na majadiliano. Na tunaamini kwamba katika mengi ya vipengele hivi Vatican na Jamhuri ya Ufilippini zina maadili sawa, maono sawa ya mambo, na kwa hiyo pengine tutaweza kufanya kazi pamoja katika siku zijazo pia.”
Mpango wa ziara ya Askofu Mkuu Gallagher nchini Ufilipino ni pamoja na kuelekea Malaybalay, katika eneo la Mindanao Kaskazini, tarehe 3 Julai 2024, ili kushiriki katika kikao cha Baraza la Maaskofu la Ufilippino. Pamoja na maaskofu, tarehe 4 Julai 2024, Askofu Mkuu Gallagher ataadhimisha Misa ya Ekaristi katika Abasia ya Kugeuzwa Sura huko Malaybalay. Hatimaye, Ijumaa tarehe 5 Julai 2024, utakuwa ushiriki katika mkutano kwenye Taasisi ya Huduma ya Kigeni, inayohusishwa na Wizara ya Mambo ya Nje, huko Manila.