Tafuta

2023.08.04 Papa akiungamisha wakati wa Siku ya vijana duniani huko Lisbon,Ureno. 2023.08.04 Papa akiungamisha wakati wa Siku ya vijana duniani huko Lisbon,Ureno.  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Idara ya Toba ya Kitume:Rehema Kamili ya Siku ya IV ya Mababu na wazee Ulimwenguni

Mnamo tarehe 28 Julai 2024 katika fursa ya Siku ya IV ya Babu na Wazee Duninai,Idara ya Toba ya Kitume imetoa maelekezo kuhusu watakaopokea Rehema Kamili na zaidi wale wote watakaoshiriki katika matukio mbali mbali yatakayofanyika ulimwenguni kote kwa ajili ya Rehema Kamili ambapo inaweza kutumika hata kwa ajili ya kuombea roho zilizoko Toharani.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Katika fursa ya Siku ya IV ya Babu na Wazee Ulimwenguni, Idara ya Toba ya Kitume  imetoa Tamko  lililotiwa saini na Kardinali Angelo de Donatis, Muungamishi Mkuu  na Askofu Krzysztof Jozef Nykiel, Askofu  wa Velia, Mhudumu Mkuu wa Idara ya  Toba ya Kitume(Penitenzieria Apostolica) ambapo tamko hilo linafafanua kuwa:  “ili kuweza kukuza ibada ya waamini na kutunza wokovu wa roho, Idara ya Toba ya Kitume kwa mujibu wa taaluma zinazohusishwa nayo na Baba Mtakatifu Francisko, kwa Mapendo ya Mungu, kwa kupokea hivi karibuni maombi ya wawakilishi wake,  Kardinali wa Kanisa Katoliki la Roma, Kevin Joseph Farrell, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Walei, Familia na Maisha, katika fursa ya Siku ya IV ya Babu na wazee Ulimwenguni  kwa mwezi Julai, ambayo  mwaka huu, inaongozwa na tema:  “Katika uzee wangu usinache”(rej. Sal 71,9).

Namna ya kujongea katika sakramenti ya kitubio

Kwa wahusika wa Kanisa, Tamko hilo linaruhusu kwa wema Rehema Kamili, kwa utaratibu wa hali za kawaida kama  (sakramenti ya kitubio, kupokea ekaristi na sala kwa nia ya Baba Mtakatifu) kwa babu, wazee na waamini wote ambao kwa kuchochewa na roho ya kweli ya toba na upendo, mnamo tarehe 28 Julai 2024, katika fursa ya Siku ya IV ya Babu na Wazee Duninai, watashiriki katika matukio mbali mbali na ambayo yatafanyika ulimwenguni kote kwa ajili ya kupata Rehema Kamili na ambayo inaweza hata kutumika kwa ajili ya kuombea roho zilizoko Toharani. Idara ya Toba ya Kitume inaruhusu vile vile kutoka Rehema Kamili katika siku hiyo kwa waamini ambao wanajikita muda wao unaofaa,  kutembelea ndugu wazee wenye kuhitaji au walio katika shida(kama vile wagonjwa, watu walio peke yao na walemavu…).

Wale ambao hawawezi kutoka nyumbani

Kwa wazee wagonjwa pamoja na wale wanaowasaidia na wale wote ambao, kwa kushindwa kuondoka nyumbani kwa sababu kubwa, wataweza pia kupata Rehema Kamili ili mradi wamejitenga na dhambi yoyote na wanakusudia kutimiza masharti matatu ya kawaida, haraka iwezekanavyo, ambapo wataungana kiroho katika majukumu matakatifu ya Siku hiyo, huku wakisali na kushirikisha machungu na mateso ya maisha yao kwa Mwenyezi Mungu, hasa wakati wa sherehe mbalimbali zikirushwa kupitia vyombo vya habari.

Idara ya kitume inawaomba mapadre kusimamia suala la Toba

Na hatimaye, Idara ya Toba ya Kitume inafafanua kuwa: “Ili, katika fursa ya kupata neema ya Mungu kwa nguvu ya Funguo za Kanisa zipatikane kwa urahisi zaidi kwa njia ya mapendo ya kichungaji, Idara ya Toba  inawaomba kwa uthabiti mapadre, wenye uwezo wa kusikiliza maungamo, wajitokeze wenyewe, wakiwa tayari na moyo wa ukarimu, kwa adhimisho la Sakramenti ya Kitubio. Tamko hili ni halali kwa Siku ya IV ya Dunia ya Mababu na Wazee, bila kujali masharti yoyote ya kinyume chake.”

Rehema Kamili ni msamaha kutoka kwa Mungu

Ikumbukukwe  kwamba Rehema kamili ni msamaha mbele ya Mwenyezi Mungu wa adhabu za muda kwa ajili ya dhambi ambazo kosa lao limekwishafutwa, msamaha ambao Mkristo mwamini aliyejiweka vizuri huupata baada ya kutimiza masharti yaliyotolewa na Mama Kanisa, kwa tendo la Kanisa ambalo likiwa ni mgawaji wa ukombozi hutumia kwa mamlaka yake hazina ya malipizi ya Kristo Yesu na ya watakatifu wake.

Sehemu mbili za rehema

Rehema imegawanyika katika sehemu kuu mbili: Rehema Kamili au Rehema ya Muda kutokana kwamba inaondoa au sehemu au adhabu yote kabisa ya muda inayotakiwa kwa sababu ya dhambi. Kila mwamini anaweza kupata rehema hiyo kwa ajili yake mwenyewe au kwa ajili ya marehemu wake kama atatimiza yafuatayo: Awali, awe na nia thabiti ya kupata rehema katika kipindi kilichopangwa. Pili, apokee Sakramenti ya Upatanisho. Tatu, apokee Ekaristi Takatifu siku hiyo ya kutolewa rehema kamili. Nne; asali kwa ajili ya nia za Baba Mtakatifu. Na hatimaye atembelee Kanisa au Kituo maalumu kilichotengwa kwa ajili ya kupatiwa rehema Kamili.

Sakramenti ya kitubio ina muundo wa pamoja na binafsi

Kwa kawaida Sakramenti ya Kitubio inaweza kuadhimishwa kwa muundo wa adhimisho la pamoja, ambamo waamini wanajitayarisha kwa pamoja, wanaungama na hatimaye, wanamshukuru pamoja kwa ajili ya msamaha walioupokea. Hapo ungamo binafsi la dhambi na ondoleo la mmoja mmoja huingizwa katika Liturujia ya Neno la Mungu, utafiti wa dhamiri, maombi ya msamaha, Sala ya Baba Yetu na Shukrani hufanywa kwa pamoja, kama kielelezo cha toba na wongofu wa ndani. Hata hivyo, kunapokuwepo na hitaji zito inawezekana kutumia adhimisho la pamoja; upatanisho wa pamoja, ungamo la jumla na ondoleo la jumla. Hitaji hili linaweza kujitokeza kutokana na hatari ya kifo cha ghafla. Hapa busara ya kichungaji inahitajika.

Ungamo la mtu mmoja mmoja 

Kimsingi, ungamo la mtu mmoja mmoja na kamili, pamoja na ondoleo, ndio mtindo pekee wa kawaida, ambapo kwa waamini hujipatanisha na Mungu, Kanisa pamoja na jirani zao. Sakramenti ya Kitubio imeundwa kwa pamoja na matendo makuu matatu yanayopaswa kutekelezwa na mwenye kutubu na ondoleo la Kuhani. Matendo ya mwenye kutubu ni toba, ungamo la dhambi au dhihirisho la dhambi mbele ya Padre na kusudi la kutimiza malipizi na kazi za malipizi.

28 Julai kutokuwa itatolewa rehema kamili
18 July 2024, 16:15