Jimbo jipya la Bentiu,Sudan Kusini na Askofu wa kwanza Carlassare
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Jumatano tarehe 3 Julai 2024, Baba Mtakatifu amechagua Jimbo la Bentiu (Sudan Kusini), lenye eneo lililotengwa kutoka Jimbo la Malakal, ndani ya Jimbo Kuu la Juba, na kumteua Askofu wake wa kwanza, Askofu Christian Carlassare, M.C.C.J., ambaye hadi uteuzi huo ni Askofu wa Rumbek.
Askofu Christian Carlassare, M.C.C.J., alizaliwa Schio, Jimbo la Vicenza (Italia), tarehe 1 Oktoba 1977. Alifanya Taaluma yake Takatifu katika Taasisi ya Wamisionari wa Comboni mwaka 2003 na akapewa daraja la Upadre tarehe 4 Septemba 2004.
Mwaka 2005, alitumwa kwa utume Sudan Kusini, alishika nyadhifa zifuatazo: Paroko msaidizi , Mhamasishaji wa Miito na Mkurugenzi wa kozi elekezi kwa Wamisionari wa Comboni, Mjumbe wa Sekretarieti ya uhuishaji wa ufundi stadi na mafunzo ya kimsingi, Mkuu wa Masimsionari wa Wamisionari wa Comboni, Makamu wa Kanda yaa Wamisionari wa Comboni nchini Sudan Kusini. Kuanzia 2020 hadi 2021 alikuwa Makamu wa Jimbo la Malakal. Tarehe 8 Machi 2021 alichaguliwa na Baba Mtakatifu kuwa Askofu wa Rumbek na kuwekwa wakfu tarehe 25 Machi 2022.
Takwimu za majimbo mawili:Malakal na Bentiu
1. Takwimu za Jimbo la Malakal, baada ya kuligawa:
Ukubwa |
200.164 km2 |
Watu: |
2.972.114 |
Wakatoliki: |
920.537 |
Parokia: |
14 |
Mapadre wa Jimbo: |
14 |
Mapadre watawa: |
9 |
Waseminari: |
7 |
Taasisi za kitawa za wanaume: |
1 |
Taasisi za Watawa wa kike |
3 |
2. Takwimu za Jimbo jipya la Bentiu:
Ukubwa: |
37.836 km2 |
Wakazi: |
1.131.886 |
Wakatoliki: |
621.643 |
Parokia: |
7 |
Mapadre wa Jimbo: |
7 |
Mapadre watawa: |
4 |
Waseminari: |
10 |
Tasisi za kitawa za kiume: |
2 |
Taasisi za watawa wa kike: |
- |