Tafuta

2024.07.05 Kardinali Czerny huko Velehrad. 2024.07.05 Kardinali Czerny huko Velehrad. 

Kard.Czerny:sinodi ni njia ya pamoja ya imani,sala,kusikilizana na kutembea pamoja

Monasteri ya Velehrad nchini Czech huwa mwenyeji wa Hija ya Kitaifa ya kila mwaka ifikapo Julai,inayoandaliwa kwa hafla ya sikukuu ya Watakatifu Cyril na Methodius.Katika neno la Kardinali Czerny baada ya Misa alisema:“tunapomheshimu Mtakatifu Cyril na Methodius tunawaomba waombee Kanisa katika mchakato wa Sinodi hapa na duniani na Oktoba 2024.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Kila mwaka mwezi Julai katika Monasteri ya Velehrad ambacho ni kituo cha kiroho cha Jamhuri ya Czech  huandaa Hija ya kitaifa  katika fursa ya Watakatifu Cyril na Methodius. Na katika fursa  ya hija ya kitaifa imeadhimishwa  misa takatifu tarehe 5 Julai 2024  na baada ya misa, Kardinali Michael Czerny, Mwenyikiti wa Baraza la Kipapa la Maendeleo Fungamani ya Binadamu ametoa neno la salamu na shukrani. Amewashukuru tena kumkaribisha katia Nchi alikozaliwa na huko Velehrad. Ni furaha yake ya kururdi tena nyumbani na kuwa pamoja nao. Kardinali alimshukuru Mwashamu Askofu Okolo kwa tafakari ya kina. “Mwaka huu, tunapomheshimu Mtakatifu Cyril na Methodius, tunawaomba waombee kwa namna ya pekee Kanisa katika safari ya  Sinodi muhimu ya kisinodi hapa na duniani kote ambayo ilianza Roma mnamo Oktoba 2023 na itaendelea Oktoba 2024.” Aidha aliongeza kusema: “Nina furaha sana kushiriki kama mjumbe, na sasa nina furaha sana kuwa msafiri pamoja nanyi hapa Velehrad. Yesu anawaita wanafunzi wake, si kuwa mtu mmoja-mmoja, bali kama jumuiya. Kama hija, sinodi ni njia ya pamoja ya imani na sala, kusikilizana, kutembea pamoja, kutafuta njia yetu ya pamoja.”

Kardinali Czerny akitoa shukrani
Kardinali Czerny akitoa shukrani

Kardinali Czerny  alisema kuwa “Mtakatifu John Chrysostom alisema kwamba Kanisa ni “jina la ‘kutembea pamoja.’” Kwa hiyo, Kanisa letu Katoliki linajifunza upya jinsi ya kuwa Kanisa la wasafiri katika nyakati hizi za kisasa zinazobadilika haraka. Sinodi ni njia ya kale na mpya kwa Kanisa zima kwenda hija ikiwa ni njia ya kila siku ya kumfuata Kristo, kuwa Mwili wake, na kueneza Injili kwa ulimwengu. Watu wote wa Mungu wanahusika, na kushiriki, katika maisha na utume wa Kanisa.”

Kardinali Czerny katika Madhabahu ya Velehrad
Kardinali Czerny katika Madhabahu ya Velehrad

Baba Mtakatifu Francisko alibanisha kuwa “ anatualika kufanya njia yetu, si kushindana na kupigana dhidi ya kila mmoja, lakini kwa amani na mahujaji wengine wote wa Mungu, kama Mtaguso wa II wa Vatican unavyosema. Hapa Velehrad leo, tuombe kukuza udugu popote tunapoishi kwa kawaida. Tafadhali kuomba kwa ajili ya Sinodi hasa wakati wa Oktoba 2024. Kwa maombezi ya Mtakatifu Cyril na Methodius, Mungu awabariki sana Kanisa letu na mahujaji wake wote, tamadanu zetu za kidini zinaweza kupimwa kwa kiwango ambacho tunaweza kuishi kwa amani na wengine, mahujaji katika ardhi hii na wanaweza kukuza maelewano hayo katika maeneo ambayo tunaishi. Kila mtu binafsi, na hata zaidi kila dini, lazima kupimwa kwa kiwango cha kujitolea. Sio kujitolea katika mukhtasari, lakini kwa uthabiti: nafsi ambayo hutafsiriwa kwa kujali wengine na ushirikiano wa ukarimu nao.

Kardinali Czerny katika Madhabahu ya Velehrad nchini Czech
Kardinali Czerny katika Madhabahu ya Velehrad nchini Czech

Monasteri ya Velehrad ilianzishwa katika karne ya 13 chini ya Milima ya Chřiby. Muonekano wa sasa wa baroque ulianza ujenzi upya, kufuatia moto, mnamo 1681. Sehemu muhimu zaidi ya monasteri ni Basilika ya Kupalizwa kwa Bikira Maria na Watakatifu Cyril na Methodius, ambayo ni patakatifu muhimu zaidi katika Jamhuri ya Czech. Mnamo 1990, Kanisa la Velehrad lilitembelewa na Papa Yohane Paulo II. Kwa njia hiyo kila mwaka waamini hufanya hija ya makumi na mamia ya kilomita, kutoka sehemu zote za Jamhuri, ya Nchi hiyo kando ya njia za hija za Moravia ya Mashariki na sala katika basilika ya Velehrad ni kufunga kwa kufaa kwa hija yao.

Kwa maelezo zaidi tembelea tovuti yao:https://www.visitczechia.com/it-it/things-to-do/places/landmarks/religious-monuments/c-velehrad-cistercian-monastery-st-cyril-and-metho

05 July 2024, 18:02